Nzowa Godat
JF-Expert Member
- Jun 15, 2011
- 2,783
- 819
Wana Jamii Forum naomba kuwasilisha hapa mbele ya jukwaa hili
Nina mpenzi wangu kamaliza chuo now nataka nioe kabisa!! Tukiwa katika maongezi ya kawaida tu nikamdokezea
Hivi mahari yako ni kiasi gani mchumba wangu kaniambia millioni nne!!Kiukweli na mpenda sana lkn naona hio pesa nyingi japo uwezo wa kuitoa nianao Je Ndio mahari za siku hizi zilivo? Naomba ushauri wenu wana JF
Ukishalipiwa mahari 4M, unasubiria mume aendelee kukuletea perfumes na gari kama zawadi nyingine? Ndo maana hamuishi kunyanyaswa! Babangu akitaka 4M ya mahari nitamlipa mie mwanae, afu ataniskia bombani!
Babangu akitaka 4M ya mahari nitamlipa mie mwanae, afu ataniskia bombani!
Mahari inapaswa kubakia kama symbol ya heshima ya kumchukua binti wa wenyewe. Na sio biashara! Umuhimu ni kwenye kujuana pande mbili na kujenga upendo.
Mmmmh ni hivyo eee? Maana niliona humu JF ng'ombe wa kisasa wa maziwa kila mmoja anauzwa 950,000 na kuendelea hadi 1,350,000. Sasa hii ya milioni nne kupata ng'ombe 30 imenishtua na kunishangaza sana.
Hebu nieleweshe mnavyo bargain wakati wa mahari inakuwaje? Mnakuwa mna bargain ng'ombe au thamani yake?
Hivi ukilia hali kwa bodi ya mikopo vipi haiwezi kusaidia?
Sasa anayetaja mahari ni yeye au wazazi wake?
Sa unalalamika nini, kama unataka kuoa wewe toa hizo mil 4, kama huna wako wenye uwezo watamuoa.
Ila vijijini hawachukui pesa, wanataka ng'ombe kabisa.
Naomba kuuliza - sasa kwa mfano mimi YATIMA - hizo milioni 4 si inabidi nichukue mwenyewe??? SINA BABA - SINA MAMA - SINA MJOMBA WALA SHANGAZI - SIN BIBI WALA BABU
Sina hata Mama au Baba wa Hiyari - Nimekulia mitaani - nikafanya biashara ndogo ndogo - Mungu akanibariki - ikaukua kidogo - nikajua kununua mitumba - kuvaa - kusuka nywele - na NIMEPENDEZA - jamaa ndio anataka kunioa - MAHARI AMPE NANI?? SI ANIPE MIMI YATIMA AU???????????
Naomba ushauri wenu - Great Thinkers!!!!!:smile-big: