Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 277
Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha imegubikwa na Mahakimu ambao hawafuati kanuni ya kazi yao na badala yake wanaonea wananchi kwa vile wanatumia utaratibu wanaoujua wao wenyewe.
Utakuta mara nyingi hakimu wa Mahakama ya Mwanzo anatoa adhabu ya kifungo cha zaidi ya miezi 12 ambayo ni kinyume na kanuni. Rufani zinaenda Mahakama ya Wilaya na Hakimu wa Wilaya hamchukulii hatua Hakimu huyo wa Mahakama ya Mwanzo.
Mara nyingine Hakimu wa Mwanzo anapokea kesi ya Baraza la Ardhi na Nyumba na kuitolea adhabu ambayo ni kinyume cha sharia.
Aidha Hakimu ya Wilaya mara nyingi anapanga kesi na zinaahirishwa pasipo sababu yo yote na wenye kesi kusumbuka.
Tunaomba Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Arusha anusuru hali hii kwani Watanzania wanateseka pasipo sababu.