Mahakama zetu ni zaidi ya duka

Mahakama zetu ni zaidi ya duka

Mahakama kama za Karatu zimetia fora kwani ni mradi wa watumishi, kwani kugonga muhuri au kuandika samansi ni elfu kumi au zaidi. Bora hata Mahakama za Kadhi kuliko hizi za Jamhuri maana ukifika unapokelewa kwa mikono miwili ili ulipie mradi. Wapiga chapa usiombe kwani kwa nakala ya hukumu sio chini ya Shs. 20,000 bora hata Secretarial Service. Wasijili wa Mahakama okoeni raia ili haki itendeke.
 
kwan lazima uende mahakamani wakati kuna ofisi ya za mawikili nyingi tu hata buku tano unagonga muhuri bila presha..kwa mahakama zetu hizi ni soko huria..
 
tehe tehe! kwahiyo kuhonga ndo heshima, kama ndo hivyo siwaweke bayana kua tunatakiwa kuheshimu taaluma kwa gharama fulani then watoe stakabadhi! taaluma yangu je itaheshimiwa lini? au unamaslahi? acheni kutetea wizi huu, mie nililipia lkn kumbuka ni watanzania wangapi watafanya hivyo hadi lini kwa utajiri upi tulinao, UMENIKERA SANA
 
kawaida itatuppeleka mpaka wapi hii, kama ni kodi halali mbona hakuna risiti? Tunabaki kulalamikia mambo kumbe wenyewe twayaendekeza! rushwaxrushwa kila kona
 
kama hujaelewa uliza kwanza uone kama hutaeleweshwa, aliyekwambia vimepotea nani? labda kama hiyo ndiyo hulka yako nami nakusamehe bure!
 
Waombaji wa kazi tuna shughuli pevu sana, Leo tar 8, Oct nimeenda mahakama kuhakikiwa nakala za vyeti vyangu lakin huko ni wiz mtupu, nikaambiwa nakala 1 ni buku 2 nilikua nazo 5 na jamaangu alikua nazo kama 10 ikatubidi tulipie hiyo pesa, kimasihala nikauliza hela hiyo niyanini, je tunalipia uchakavu wa mihuri? nikajibiwa tunalipia cheo cha hakimu na wino/ink, nikataka kuulizia kama nitapata risiti lkn nikaacha coz niliona amenichukia kufuatia swali langu la awali. Lkn kukaa kwangu hapo kwa muda usiozidi dak 10 lile DUka/Mahakama lilikua linamake enough money. Ila ikaniuma sana coz sion mantiki ya kuhonga nami ninavyeti halisi vya elimu yangu. Kisha kama mtu anakaa miaka zaidi ya mi3 akiwa anaomba kazi mbona atakufa kwakuneemesha walioko kwenye uskani! Should we pray for them??????

Kasome the NOTARY PUBLIC AND COMMISSIONERS FOR OATH ACT CAP 12 tena imekua ammended mwaka huu, uyo aliekuambia 2000 mshukuru sana kakuonea huruma sheria imepandisha kiwango to 20000! Haya mambo yapo kisheria wacha kulalamika
 
ungeniambia mapema kuna makanjanja kkoo wapo wengi wana mihuri na hawana vyeti document buku 5 ya chai unasema wanatumia mihuri ya uridhi,
kama kuna docta feck, traffic, usalama, nk why not muhuri

Mpaka watengeneza sahihi wapo, K/koo ndo kila kitu....
 
Wakili huwa anatoa risiti? Ukipata jibu basi utaelewa kwa nini mahakama hawatoi.
 
Mahakama siku hizi hazina risiti. Kama ada ni Shs. 2,000/= utaambiwa ulipe Shs. 10,000 au 20,000 pasipo Stakabadhi ya Serikali.
 
Back
Top Bottom