Mahakama "yamgomea" Mbowe kuhusu zuio la polisi mikutano ya kisiasa

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali, anaandika Moses Mseti.

Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi.

Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba kutengua zuio hilo la polisi.

Mohammed Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo amepitia ombi lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji anayewakilishwa na mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa uamzi.

Jaji Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo kortini kitendo kilichosababisha kulitupilia mbali.

Amesema kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa wajibu maombi unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando waliweka pingamizi wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.

Jaji Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala ya kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.

“Waleta maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo katika kuleta ombi na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi halipaswi kupokelewa,” amesema Jaji Gwae.

Hata hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu maombi, walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa kuwepo na hivyo vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.

Amesema kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa kuwepo ni kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na kifungu kidogo cha vya sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika maelezo (Statements) badala ya (chember samers).

Mallya, mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea kanuni na vifungu hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia marekebisho kama Jaji Mohamed Gwae alivyoelekeza.

Chanzo: Mwanahalisi
 
Kazi sana aisee...sijui tutakimbilia wapi mwaka huu. Kila sehemu ni ubabe tu.
 
ahawo wanasheria ; wanafanya kazi utadhani waganga wa kienyeji;
nani anawalisha na nani kawakalisha mwanza mpk leo hii
 
Hao wanasheria na viongozi wa CHADEMA wajanja.Kesi wanaifungulia huko mwanza kusudi.Siku zote kesi ifunguliwe wamekula posho za kujikimu shilingi ngapi? Hawakai bure kila siku wanaingiza pesa mfukoni.Mbowe naye hayuko bungeni kama yuko huko Mwanza toka kesi ifunguliwe akisema yuko kufuatilia hiyo kesi atakuwa kaingiza pesa za kutosha.

Kuahirisha ahirisha huko kuna faida ya kipesa kwao.Leo wanakosea kifungu hiki makusudi wakijua ikienda kwa jaji atasema imekosewa wanarudi zao mahotelini kubomoa kuku wanajipa siku zingine tena za kuendelea kulipwa wakiandaa nk

Hujui kuwa kesi zingine si kesi tu bali ni miradi ya watu.Wewe unafikiri ruzuku ya chama ukitaka kuila unaila vipi si lazima ubuni mradi waweza kuwa wa kesi au huo hewa unaoitwa sambaza demokrasia nchi nzima unazunguka mwaka mzima ukisambaza kinachoitwa demokrasia hewa huku ukipata pesa kibao za posho za kujikimu.
 
Acha wivu wewe kinakuhusu nini? Acha kesi isikilizwe upya maswala ya matumizi waachie CHADEMA.
 
Hao wanasheria na viongozi wa CHADEMA wajanja.Kesi wanaifungulia huko mwanza kusudi.Siku zote kesi ifunguliwe wamekula posho za kujikimu shilingi ngapi? Hawakai bure kila siku wanaingiza pesa mfukoni.Mbowe naye hayuko bungeni kama yuko huko Mwanza toka kesi ifunguliwe akisema yuko kufuatilia hiyo kesi atakuwa kaingiza pesa za kutosha.

Kuahirisha ahirisha huko kuna faida ya kipesa kwao.Leo wanakosea kifungu hiki makusudi wakijua ikienda kwa jaji atasema imekosewa wanarudi zao mahotelini kubomoa kuku wanajipa siku zingine tena za kuendelea kulipwa wakiandaa nk

Hujui kuwa kesi zingine si kesi tu bali ni miradi ya watu.Wewe unafikiri ruzuku ya chama ukitaka kuila unaila vipi si lazima ubuni mradi waweza kuwa wa kesi au huo hewa unaoitwa sambaza demokrasia nchi nzima unazunguka mwaka mzima ukisambaza kinachoitwa demokrasia hewa huku ukipata pesa kibao za posho za kujikimu.

Ni wale waasisi wa Ufisadi Tanzania CCM wanaoweza kufikiria hivi tu Tanzania siyo wengine. Kila mahali kupiga hadi kwenye misiba yanafikiri kupiga CCM
 
hizi ni hujuma na ni mpango wa kupiga pesa haiwezekani, mawakili kama John mallya na kibatala wasitambue hiyo kanuni mpaka kosa lina bounce mahakamani! kwa maoni yangu hao mwakili wajitoe kwenye kusimamia hiyo kesi na badala yake UKAWA itafute mawakili wa kuendelea na hiyo kesi
 
Ile separations of power tunaojua iko wapi Kama kila mhimili imeshikwa na magogoni kuanzia bunge mpaka mahakama. Pamoja na hayo naamini haki itapatikana.
 
ahawo wanasheria ; wanafanya kazi utadhani waganga wa kienyeji;
nani anawalisha na nani kawakalisha mwanza mpk leo hii
Acha wajilie ruzuku,milioni 900 kwa mwezi sio mchezo lazima zitafutiwe namna bora ya kutumbuliwa
 
Mbona hili shauri lilishaamuliwa tangu wiki iloyopita na mawakili wamesharekebisha makosa? au nyie mnaishi Tanzania ipi.
 
Warekebishe hilo tatizo kisha warudishe shauri mahakamani!
Mkuu hiko kifungu kinachotakiwa kiingizwe ni dhaifu kwa kesi kama hiyo,lazima walalamikaji waoneshe wameathirika vipi kwa kuzuiwa mikutano.
Ingekuwa chadema walitaka kufanya mkusanyiko wakapika pilau na pombe wangesikilizwa kwa kuwa pilau ilichacha baada ya mkutano kufutwa
 
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali, anaandika Moses Mseti.

Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi.

Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba kutengua zuio hilo la polisi.

Mohammed Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo amepitia ombi lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji anayewakilishwa na mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa uamzi.

Jaji Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo kortini kitendo kilichosababisha kulitupilia mbali.

Amesema kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa wajibu maombi unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando waliweka pingamizi wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.

Jaji Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala ya kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.

“Waleta maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo katika kuleta ombi na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi halipaswi kupokelewa,” amesema Jaji Gwae.

Hata hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu maombi, walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa kuwepo na hivyo vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.

Amesema kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa kuwepo ni kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na kifungu kidogo cha vya sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika maelezo (Statements) badala ya (chember samers).

Mallya, mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea kanuni na vifungu hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia marekebisho kama Jaji Mohamed Gwae alivyoelekeza.

Mkuu (chember samers), ndio nini?
 
Back
Top Bottom