ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 44,142
- 50,828
Harafu Chadema wanakwambia hakuna Demokrasia Wala uhuru wa Mahakama.
Chadema ni hatari sana Kwa upotoshaji waogopwe kama ukoma.
Huyu Mhasibu akishinda kesi atareheshwa kazini na fidia Juu
My Take
Sheria za Utumishi za Tanzania zitazamwe Upya Kwa sababu mtu anaweza Kuiba na Bado akapata Haki.
=======
Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dar es Salaam imeridhia maombi ya aliyekuwa Mhasibu Msaidizi wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Pere Muganda kufungua shauri la kupinga uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi ulioidhinishwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa kuridhia kuachishwa kwake kazi.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Abdi Kagomba baada ya kujiridhisha kuwa amekidhi vigezo vya kisheria, katika maombi yake hayo ambayo pia yaliungwa mkono na wakili wa Serikali aliyeiwakilisha Serikali wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo.
“Kwa kuzingatia sababu hizo hapo juu, nimeridhika kuwa maombi (shauri) yamekidhi viwango vya kisheria kupewa ruhusa ya kufungua shauri la maombi ya mapitio”, amesema Jaji Kagomba kwa tafsiri isiyo rasmi, baada ya kujadili hoja za pande zote na kuhitimisha:
“Kwa hiyo ninatoa kibali kwa mwombaji (Muganda) kuomba amri (za mahakama) kama alivyoomba.”
Muganda alifukuzwa utumishi wa umma na Tume ya Utumishi wa Umma kwa tuhuma za kupoteza fedha za umma, uamuzi ulioungwa mkono na Katibu Mkuu Kiongozi na kuidhinishwa na Rais, Samia Suluhu Hassan.
Mwananchi