Mahakama yaisindikiza CHADEMA Ikulu

Mahakama yaisindikiza CHADEMA Ikulu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ni dhahiri sasa Mahakama,kama Mhimili wa Kutoa Haki Tanzania,imechoka kutumiwa na Serikali na chama tawala kukandamiza demokrasia nchini Tanzania.Imechoka kuwa kichaka cha hujuma juu ya demokrasia. Mahakama imechoka kuwa na Wabunge wa Mahakama na vimbelembele-makada wa kupinga hata visivyowahusu. Sasa Mahakama imeamka.

Kilichotokea kwa Yamsebo-kule Sumbawanga,Mnyika-Ubungo,Lema-Arusha Mjini,na kwa Madiwani wa Mwanza na Arusha ni ushahidi tosha. Kama CCM na Serikali yake haijui,kesi hizi zinaipaisha CHADEMA kwenda juu zaidi na kuelekea Ikulu 2015. Hebu vuta picha ya nchi hii leo baada ya Ushindi wa Lema wa CHADEMA!

Vuta picha ya Arusha na mikoa mingine atakapopita Lema kama Mbunge wa Arusha mjini.Nchi itatikisika kwa furaha na kukubalika kwa CHADEMA. CCM na vibaraka wake wanafanya kosa kubwa. Wanaifanya Mahakama iipaishe CHADEMA juu na juu zaidi kiumarufu.

Sasa wale wa M7 mtulie. CHADEMA ijipange kimkakati na kihoja luelekea Ikulu 2015.Njia imefunguka. Njia nyeupe. Eee Mwenyezi Mungu niongeze umri wa kuishi niione siku ya ukombozi wa nchi hii toka kwa hawa waliochoka kutuongoza CCM na vibaraka wao. Nakuomba sana Mwenyezi Mungu.Amina.
 
aisee uchaguzi wa Igunga lini? maana tunataka Nape na Mwigiru wakajipime nguvu upya; sijui wataenda na single gani mpya maana hii ya DR.Slaa na kadi ya CCM ime-ekispaya.

Yes vijana wa M7, tulieni rudini mjenge CDM ila kama kuna kijana ana kinyongo basi bora aachane na siasa au atafute pa kwenda mapema sababu CDM inaongozwa na nguvu za mwenyezi Mungu - ukitaka kuihujumu itakuhukumu hadharani kabla hujaweka madhara - CDM ni machozi ya watanzania maskini ambao hadi saa hii (kumi kasoro) hata UJI hawajanywa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni bora mahaka ikarudisha heshima kidogo maana watu walishaondoa imani nayo muda mrefu sana!
 
Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeennnnnnnnnnnn
Acha yatimie........tumewachoka CCM!!!
 
wameona hawana jinsi maana mahakama ya wananchi ipo hata wakichakachua hukumu bado wananchi wataendelea kuihukumu ccm tena kwa hasira zaidi!
 
Hongera lema,mungu akuongoze tena.haki ucheleweshwa tu
 
Pamoja makamanda!

Ila kazi bado kubwa mbele yetu, safari bado ni ndefu na ngumu. We've won the battle but we need to keep our focus and win the ultimate war!

Hivyo tusherehekee kidogo kwa kiasi kisha turudi uwanjani.
 
Ikulu inajitahidi kuonyesha kuwa hawaingilii uhuru wa mahakama. Kweli??
 
peopleeeeeez........yanayoendelea Arusha ni message kwa masalia na wale wote waliokaa mkao wa kukisaliti chadema....alhakini wangelifahamu kuwa Mungu ashindwi na yeyote yule....chadema si mtu bali ni ni dhamira ya kweli.....asitokee mtu akajiona yeye ni zaidi ya wengine.....ukombozi ni lazima utafikiwa ingawa njia yake si nyeupe....
 
Back
Top Bottom