ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.
Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakijitambulisha kama wapigakura.
Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Mohamed Gwae ilitupilia mbali kesi yao baada ya kukubaliana na pingamizi la wakili wa Bulaya, Tundu Lissu kuwa hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.
Chanzo: Mwananchi
Court of Appeal inasoma hukumu usiku saa 6! Makubwa haya! Vinginevyo ni vigumu kuamini tetesi hii.Mahakama ya rufaa ya Tanzania leo imetoa hukumu iliyowapa ushindi wafuasi wa Steven Wassira, mabwana Janes Ezekiel, Escietik Mayagila, Matwiga na Magambo Masato.
Kulingana na maudhui ya hukumu hiyo Bulaya hataruhusiwa kuwania tena kiti hicho, hali inayotoa picha ya Chadema kuwa na wakati mgumu kukirudisha tena kiti hicho.
litarudi kama wakitumia u ccm na ungosha.Jimbo litarudi CCM time will tell.
Hakuna lolote !
Wapiga kura ambao haki zao za msingi hazijakiukwa ( hawa walipiga kura na ccm ilikuwa na mawakala kila kituo ) hawana haki ya kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi , wasira mwenyewe aliogopa nini kufungua kesi hii ? Huyu atadhalilika hadi afumue kisukari chake nakuambia , tunajua katika hao walalamikaji yupo ndugu yake .
Mahakama ya Rufaa haibanwi na maamuzi yake. Kimantiki jiulize mwenyewe iweje upige kura yako halafu isihesabiwe, apewe ushindi mtu asiyestahili? Nadhani ni vyema mpiga kura lazima awe na haki ya kuhoji matokeo. Hii ya uzee na ujana ni nonsense, ujana si leseni ya ujinga. Ester tangu achaguliwe hajahudhuria bunge hata siku moja shida yaje eti Dr Tulia anamgomea. Kwani alikuchagua Dr Tulia? Ujana wa fujo na uzandiki unajikomoa mwenyewe. Na ubunge ni kushlndanisha sera za vyama si mtu mmoja mmoja. Bora ashindwe.Hii mahakama ya rufaa si ndo iliyozuia wananchi kufungua kesi za uchaguzi kwenye kesi ya Lema? Leo mbona wanakula matapishi yao?
Rudia umesemaje?Mahakama ya Rufaa haibanwi na maamuzi yake. Kimantiki jiulize mwenyewe iweje upige kura yako halafu isihesabiwe, apewe ushindi mtu asiyestahili? Nadhani ni vyema mpiga kura lazima awe na haki ya kuhoji matokeo. Hii ya uzee na ujana ni nonsense, ujana si leseni ya ujinga. Ester tangu achaguliwe hajahudhuria bunge hata siku moja shida yaje eti Dr Tulia anamgomea. Kwani alikuchagua Dr Tulia? Ujana wa fujo na uzandiki unajikomoa mwenyewe. Na ubunge ni kushlndanisha sera za vyama si mtu mmoja mmoja. Bora ashindwe.