Mahakama ya Rufani yaamuru Kesi ya Wasira na Bulaya isikilizwe upya

Wafuasi wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Steven Wassira wamembwaga mahakamani mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Ester Bulaya wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi yao.

Wafuasi hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Escietik Malagila walifungua kesi ya uchaguzi kupinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakijitambulisha kama wapigakura.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Mohamed Gwae ilitupilia mbali kesi yao baada ya kukubaliana na pingamizi la wakili wa Bulaya, Tundu Lissu kuwa hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Nilivyoelewa ni kuwa wafuasi wa Wassira wameruhusiwa kuendelea na kesi yao ili ianze kusikilizwa baada ya Mahakama ya rufani kutupilia mbali pingamizi la Mhe Tundu Lissu. Kwa hiyo Esther Bulaya bado ni mbunge mpaka atakaposhindwa kwenye kesi.
 
Mahakama ya rufaa ya Tanzania leo imetoa hukumu iliyowapa ushindi wafuasi wa Steven Wassira, mabwana Janes Ezekiel, Escietik Mayagila, Matwiga na Magambo Masato.

Kulingana na maudhui ya hukumu hiyo Bulaya hataruhusiwa kuwania tena kiti hicho, hali inayotoa picha ya Chadema kuwa na wakati mgumu kukirudisha tena kiti hicho.
Court of Appeal inasoma hukumu usiku saa 6! Makubwa haya! Vinginevyo ni vigumu kuamini tetesi hii.
 
Wakishindwa kesi kwenye kulipa gharama ndo wataanza kulia lia tusamehe, sisi wakulima alitulaghai yule mzee haya tusibiri.
 
Hakuna lolote !
Wapiga kura ambao haki zao za msingi hazijakiukwa ( hawa walipiga kura na ccm ilikuwa na mawakala kila kituo ) hawana haki ya kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi , wasira mwenyewe aliogopa nini kufungua kesi hii ? Huyu atadhalilika hadi afumue kisukari chake nakuambia , tunajua katika hao walalamikaji yupo ndugu yake .

Si mnaye mwanasheria mahiri kuliko wote Tanzania kwenye SACCOS yenu? Mwambieni akupatieni tafsiri ya hukumu hiyo.
 
Jimbo litarudi ccm tena atatangazwa na magari ya washawasha yakiwa nje, ffu kama kawaida kama ilivyotokea kule mtwara mpaka nilishangaa, yani kutangazwa jamaa kashinda kesi mpaka na magari ya washawasha yakiwa pembeni, nilihisi kuna dhulma ilifanyika
 
Hii mahakama ya rufaa si ndo iliyozuia wananchi kufungua kesi za uchaguzi kwenye kesi ya Lema? Leo mbona wanakula matapishi yao?
Mahakama ya Rufaa haibanwi na maamuzi yake. Kimantiki jiulize mwenyewe iweje upige kura yako halafu isihesabiwe, apewe ushindi mtu asiyestahili? Nadhani ni vyema mpiga kura lazima awe na haki ya kuhoji matokeo. Hii ya uzee na ujana ni nonsense, ujana si leseni ya ujinga. Ester tangu achaguliwe hajahudhuria bunge hata siku moja shida yaje eti Dr Tulia anamgomea. Kwani alikuchagua Dr Tulia? Ujana wa fujo na uzandiki unajikomoa mwenyewe. Na ubunge ni kushlndanisha sera za vyama si mtu mmoja mmoja. Bora ashindwe.
 
Mahakama ya Rufaa haibanwi na maamuzi yake. Kimantiki jiulize mwenyewe iweje upige kura yako halafu isihesabiwe, apewe ushindi mtu asiyestahili? Nadhani ni vyema mpiga kura lazima awe na haki ya kuhoji matokeo. Hii ya uzee na ujana ni nonsense, ujana si leseni ya ujinga. Ester tangu achaguliwe hajahudhuria bunge hata siku moja shida yaje eti Dr Tulia anamgomea. Kwani alikuchagua Dr Tulia? Ujana wa fujo na uzandiki unajikomoa mwenyewe. Na ubunge ni kushlndanisha sera za vyama si mtu mmoja mmoja. Bora ashindwe.
Rudia umesemaje?
 
Back
Top Bottom