Mahakama ya Rufaa ya Rwanda yaidhinisha kifungo ch a miaka 25 dhidi ya shujaa wa Hotel “Hotel Rwanda”

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,621
Mahakama ya Rufaa ya Rwanda Jumatatu iliidhinisha kifungo cha miaka 25 jela dhidi ya shujaa wa "Hoteli Rwanda" Paul Rusesabagina, ambaye alipatikana na hatia mwaka jana kwa tuhuma za "ugaidi", na kukataa rufaa ya upande wa mashtaka ya kuongeza adhabu ya maisha.

"Kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza, mahakama inaona kwamba adhabu yake isiongezwe, kwa sababu miaka 25 aliyopewa inalingana na uzito wa makosa yake, na mahakama inadumisha kifungo chake," alisema Jaji Francois Regis. Rukundakuvuga.

Kesi hiyo imekuwa na umaarufu mkubwa tangu Rusesabagina, 67, alipokamatwa Agosti 2020 baada ya kile alichokitaja kama utekaji nyara kutoka Dubai na mamlaka ya Rwanda.

Rusesabagina alifanya kazi kama meneja wa Hotel des Mille Collines mjini Kigali na kusaidia kuwahifadhi Wahutu na wakimbizi wa Kitutsi huko wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.

Alishutumiwa kwa kuunga mkono mrengo wenye silaha wa jukwaa lake la upinzani la Rwandan Movement for Democratic Change. Kundi hilo lilikuwa limedai kuhusika na mashambulizi ya mwaka 2018 na 2019 kusini mwa nchi ambapo Wanyarwanda tisa waliuawa.

Chanzo: Aljazeera
 
Hapa ukweli ni upi ?

Ni nani kadhibitisha kweli alikuwa anafadhili wauwaji na sio kusaidia wanaokimbia ?

Hii dunia ngumu sana sometimes ni vigumu kujua ukweli ni upi, na mara nyingi ukweli ni ule mwenye uwezo / mwenye nguvu ndio anaamua ukweli uwe upi...

Ningeshauri wale wote aliowasaidia wajitokeze, kama wapo, ili kumsaidia au kujaribu kusafisha jina lake
 
watutsi wabinafs sana hawajali ila wahutu wanahofia kubambikwa kesi za mauaj ya kimbali
 
watutsi wabinafs sana hawajali ila wahutu wanahofia kubambikwa kesi za mauaj ya kimbali
Kwahio hakuna hata mmoja hata huko ugaibuni; kwani wale walioongea na actors / directors kwenye ile Hotel Rwanda walitokea wapi

Sisemi waje waongee under the Court of Law hata kwenye insta au pembeni pempeni..., (Au wanaongea )?
 
Ndugu tuwahurumie hao mashuhuda, PK ameshaamua huyo ni mtuhumiwa, jiulize, alifikaje Rwanda?! Kimabavu, alitekwa, anafikiria anaenda Dubai sijui wapi, ndege ikamshusha Kigali!
PK kachora ramani nzima, aje nani wa kuzuia hukumu ya mchongo!?
 
Huwa nna mashaka sana na Rwanda siku PK akitutoka ni kama nayaona yale yale ya 94…..

#Pray For Rwanda
 
Back
Top Bottom