Mahakama lazima ziwe huru nchini

Erasto Malilo

New Member
Apr 11, 2023
1
0
Meseji zampa ushindi kwenye usimamizi wa mirathi

Na Mwandishi Wetu, Pwani

MAHAKAMA ya Mwanzo Mkuranga imetoa hukumu ya mirathi Na 29/2018 kati ya waleta maombi, Ashura Ndundu, Eva Nangela dhidi ya mjibu maombi Rashid Kilindo.

Katika hukumu hiyo mahakama ilitoa ushindi kwa Ashura Ndundu na Eva Nangel baada ya kujiridhisha kuwa mmoja wa waleta maombi aliendelea kupokea meseji za vitisho kupitia simu ya mkononi.

Akisoma hukumu hiyo hivi karibuni Hakimu Mkazi N Maroa wa Mahakama ya Mwanzo, Mkuranga alisema kwamba mmoja wa waleta maombi, Eva Nnagela aliendelea kupata vitisho kutoka kwa watu wanaodaiwa ni wadau wa Rashid Kilindo kwenye shauri hilo la mirathi ya marehemu Arnaldo Amadoli.

Awali kwenye kesi hiyo ya mirathi ya marehemu Amadoli yalipelekwa maombi kwa mahakama hiyo ya mwanzo kupiga msimamizi wa mirathi namba mbili, Rashid Kilindo yaliyowasilishwa na Ashura Ndundu Pamoja na Eva Nangela.

Akiwasilisha hoja yake mmoja ya mawakili wa waleta maombi, Mariamu Masandika alidai mbele ya mahakama hiyo kwamba mteja wake, Eva Nangela alikuwa akipokea meseji hizo za vitisho ikimtaka wakae mezani ili waweze kutatua matatizo katika mirathi hiyo na aliwasilisha meseji iliyokuwa na jina la Samandito Gombo.

Hukumu hiyo iliendelea kwamba waleta maombi walikuwa na sababu nne ya kutaka mahakama hiyo itengue usimamizi wa Ahmed Kilindo kusimamia mirathi ya marehemu Arnaldo Amadoli kwamba hakuwa muombaji na uteuzi wake hakuzingatia ridhaa ya warithi pamoja na mjane wa marehemu.

Pamoja na hoja zingine mawakili wa upande wa waleta maombi, ambapo ni wakili Kelvin Ngeleja na Mariamu Masandika walidai pia mbele ya mahakama hiyo kuwa uteuzi wa Rashidi Kilindo hauna maana yoyote na hajafanya kazi tangu alipoteuliwa 16/11/2019 na alikiuka baadhi ya masharti kwenye usimamizi huo.

Mahakama ya Mwanzo Mkuranga ilitoa hukumu ya Mirathi Na 29/2018 kati ya waleta maombi Ashura Ndundu , Eva Nangela dhidi ya mjibu Maombi Rashid Ahmed Kilindo kuhusu usimamizi wa mirathi ya Marehemu Arnaldo Amadoli na kutengua usimamizi wa Rashid Ahmed Kilindo kutokana na matwaka ya kanuni namba 10(1) kanuni za usimamizi wa mirathi mahakama za mwanzo GN 49/1971.

Kwa upande wake mleta maombi Namba pili, Eva Nangela alipopigiwa simu hili athibitishe kama alitumiwa ujumbe wa simu zenye vitisho na ni mara ngapi alipokea ujumbe hizo , alimtaka mwandishi wa habari hizi kumtafuta wakili wake aweze kuzungumza kwa niaba yake.

Na mahojiano ya simu kati ya mwandishi na mleta maombi namba pili yalikuwa hivi “ Nani amekupa namba yangu ya simu na je ulipata wapi nakala ya hukumu ya mahakama baada ya kujibiwa alikata simu.”

Naye mlalamikaji kuhusu ujumbe wa simu za mkononi, Bw. Samandito Gombo alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusu jina lake kutokea kwenye hukumu alishangaa na kudai kwamba yeye hauhusiki kabisa kwenye kesi na ameshtushwa sana na taarifa hizo.
 
Back
Top Bottom