Mahakama Kuu yaitaka Pride Tanzania kuilipa CRDB zaidi ya Tsh. Bilioni 12 ilizokopa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mahakama Kuu imeitaka Pride Tanzania kuilipa Benki ya CRDB zaidi ya Sh12 bilioni zilizotokana na mkopo.

Pride Tanzania ilichukua mkopo kwa jina la Promotion of Rural Initiatives and Development Enterprises Limited na ilikubaliwa ingeulipa na riba ya asilimia 17.

Uamuzi huo ulitolewa Alhamisi wiki iliyopita na Jaji L.J.S Mwandambo wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.

Kesi hiyo ilifunguliwa na benki hiyo ikimhusisha aliyekuwa mtendaji mkuu wa taaasisi hiyo, Rashid Malima na Dk William Lyakurwa kwa niaba ya Pride Tanzania. Washtakiwa hao walikutwa na makosa ya kuvunja mkataba uliowawezesha kukopeshwa fedha hizo.

Hivyo mahakama hiyo iliiamuru Pride Tanzania kuilipa CRDB Sh12,050,745,634. Riba ya mkopo huo ambayo ni asilimia 17 itaanza kuhesabiwa tangu siku kesi ilipofunguliwa hadi siku ya hukumu.

Mahakama pia imemtaka mshtakiwa (Malima), kuorodhesha nyaraka za fedha za Pride Tanzania

Chanzo; Mwananchi
 
Hiyo hela PRIDE wataipatia wapi?. Kampuni yenyewe inapumulia chini ya maji
 
Hivi haikuwa na uhusiano n mke wa malofa? Wana miradi mingi na pesa nyingi waliiba na bwanake walipe tu
 
Back
Top Bottom