Mahakama Kuu yaamuru wanaoishi mabondeni kuhama mara moja

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeamuru wakazi 91 wa eneo la Bonde la Msimbazi, Mchikichini Bagdad, waondoke mara moja katika eneo hilo na wengine 12 wasihame hadi watakapopewa maeneo mengine ya kuishi.

Jaji Zainab Mruke alitoa uamuzi huo katika kesi ya kupinga kuondoka katika eneo hilo, iliyofunguliwa na Juma Malumbo, Maulid Fundi, Aisha Saliko, Aisha Mhagama na wengine 99 dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wadai hao walikuwa wanapinga kuondolewa katika eneo hilo, linalodaiwa si salama kwa makazi, pia waliomba mahakama iwazuie mkuu wa mkoa na mkurugenzi wa manispaa, wasiwahamishe katika maeneo wanayoishi na kama watahamishwa, walipwe fidia pamoja na kupewa maeneo mengine ya kuishi.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Mruke alisema baada ya kupitia ushahidi, mahakama imethibitisha kuwa watu 12 walipewa Leseni za Makazi na Manispaa ya Ilala, hivyo siyo wavamizi kwa kuwa Manispaa yenyewe ndiyo iliwaaminisha kuwa wako maeneo sahihi na wanaruhusiwa kukaa hapo.

Alisema watu hao hawataondolewa katika maneo yao mara moja, badala yake aliiamuru Manispaa hiyo iwape muda wa mwaka mmoja wa kujiandaa kuondoka hapo na pia ihakikishe inawapatia viwanja mahali pengine.

Kuhusu wadai wengine 91, mahakama ilijiridhisha na kutamka kuwa hao ni wavamizi na ikawaamuru waondoke mara moja kwa kuwa hakuna hata mmoja mwenye leseni ya makazi, kama ilivyokuwa kwa wenzao 12.

Aliongeza kuwa wadai hao hawakufika mahakamani kutoa ushahidi wao, isipokuwa wadai wanne ambao pia walitoa ushahidi kwa mambo yao wenyewe tu, “kwa sababu hawakuleta ushahidi, hakuna jambo ambalo mahakama inaweza kuamua dhidi yao”.

Jaji Mruke alisema hakuna uthibitisho wowote kuwa wakazi hao, wanakaa katika maeneo hayo kihalali, kama wenzao 12 ambao walikuwa na leseni za makazi, hivyo alisema watu ni wavamizi na wanatakiwa kuondolewa katika eneo hilo mara moja.

Alisema kama Manispaa ya Ilala itakuwa na viwanja, iwape mahali pengine lakini na kama hailazimiki kwa namna yoyote ile kuwatafutia viwanja, kwa vile hawana haki hiyo kwa sababu ni wavamizi.

Kuhusu madai ya fidia, Jaji Mruke alisema wadai wote 103, walijenga bila idhini na hakuna hata mmoja aliyekuwa na kibali cha ujenzi, hivyo walijenga kinyume cha sheria na hawana haki ya fidia yoyote.

Chanzo: HabariLeo

====

Walatini walisema, ignorance of the law excuses not!
 
Siku zote huwa wanachelewesha tu ila kama uko sehemu mbaya utavunjiwa hata kama baada ya miaka 100
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeagiza wakazi wa Bonde la Msimbazi na Mchikichini Baghdad kuondoka maeneo huku wengine 12 wameambiwa kusubiri mpaka serikali itakapowatafutia maeneno mengine ya kujenga kwa sababu walikuwa na residence permits zilizotolewa na Manispaa ya Ilala.

Uamuzi huo ulifikiwa na Jaji Zainab Mruke baada ya pingamizi la bomoa bomoa lililowekwa na Juma Malumbo, Maulid Fundi, Aisha Saliko, Aisha Mhagama na wengine 99 dhidi ya Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Jaji Zainab alisema, Serikali hailazimishwi kisheria kuwatafutia sehemu nyingine ya kuishi kwa sababu walivamia na kuishi katika eneo ambalo sio lao kisheria.

Hukumu hii inahitimisha tambo za wakaazi wa Mabonde ya Mto Msimbazi na Mchikichimi ambao kwa sasa wanachotakiwa ni kuanza kutafuta kwa haraka sehemu nyingine ya kuishi bila kusubiri tingatinga la Mwanasheria wa NEMC,Heche saguta!

Walatini walisema, ignorance of the law excuses not!
NILISEMA HAPA KWAMBA WATAONDOKA TU NA WANACHOFANYA NI KUPOTEZA MUDA TU.
 
Sheria tumetunga wenyewe. Zisituondolee utu, ubinadamu na udugu wetu. Waondoke lakini si kwa fedheha. Wapewe muda wa kutosha kuondoka maana Serikali IPO tu hata baada ya Magufuli. Wasinyanyaswe na kudhalilishwa na magreda.
 
Kama kuna kitu nachukizwa nacho ni hili suala la mabondeni. Watanzania tumejifunza sana kuwa wajanja wajanja katika mambo ya msingi hata yanayogusa moja kwa moja maisha yetu. Kuishi eneo hatarishi halafu unaambiwa uondoke eti unaenda mahakamani!!! Ifike hatua mahakama zifanye kazi sensitive. Hawa walipaswa walipe na case charges kwa serikali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kipuuzi kama hizi. Pitisha greda wajue wataishi wapi. Kama ni kufa kwa kukosa makazi sawa. Wanakera sana. Mafuriko yakiwakumba wanataka serikali hiyo hiyo iwasaidie, huduma zingine wakikosa wanalalamika alhali fedha zinawahudumia katika mambo ya kipuuzi. BOMOA BOMOA IENDELEE HARAKA IWEZEKANAVYO.
 
Siku zote huwa wanachelewesha tu ila kama uko sehemu mbaya utavunjiwa hata kama baada ya miaka 100
Nadhani wakati kesi ikiendelea wale wajanja walipata muda mwafaka wa kutafuta sehemu nyingine ya kuishi.
 
I saw this coming, sasa sijui yule mbunge waliyekua wanambeba juu juu ataficha wapi sura yake, anyways bado there is room for appeal...
 
it is very obvious ata serikali isipowahamisha watahamishwa na mafuriko, it was just a matter of time, ila gazeti siyo source sahii sana kwa maamuzi ya mahakama, tupime lakini
 
Back
Top Bottom