Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,743
- 2,600
Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, inatarajiwa kutoa kuhusu hoja ya Mheshimiwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kuomba kujumuishwa kama mshitakiwa katika kesi inayoendelea inayohusu mgawanyo wa mali za chama Machi 3, 2026.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar, Said Issa na wenzake Maulida Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis, waliokuwa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya chama hicho, wadai wanahoji mgaanyo wa mali za chama hicho kwa Bara na Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 2 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezo wa CHADEMA, Brenda Rupia imewataka viongozi na wanachama kujitokeza kwa wingi mahakamani siku Machi 3 kwa kuzingatia uzito wa kesi hii na athari zake kwa mustakabali wa chama hicho.
Soma pia: Pingamizi kesi ya mgawanyo wa mali CHADEMA latupiliwa mbali