Mahakama kuu Kenya yatoa amri kumkamata... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama kuu Kenya yatoa amri kumkamata...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KELVIN GASPER, Nov 29, 2011.

 1. KELVIN GASPER

  KELVIN GASPER JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 962
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Mahakama kuu ya kenya jana ilitoa amri ya kukamatwa raisi wa sudan omar al bashir. amri hii ya mahakama ya kenya imepelekea serikali ya sudan kumtimua balozi wa kenya nchini sudan na kumwamuru balozi wake nchini kenya kurejea nyumba. kenya ni mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai icc.
   
 2. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Kenya kibaraka wa marekani so wametumwa mmalekani kaona mafuta pale
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,119
  Trophy Points: 280
  kenya inatumiwa na nchi za magharibi
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Kila anayetaka haki itendeke anaambiwa eti "anatumika".
   
 5. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana mheshimiwa;
  Je USA ilipovamia Iraq kwa tuhuma kuwa kuna WMD(Weapons of Mass Destruction) walizipata hizo silaha?
  Na kama hawakuzipata je hapo haki ilitendeka?
  Hatua gani UNSC ilichukua dhidi ya USA & Allies kwa kulaghai ulimwengu?

  Tatizo ni kwamba media nyingi zinaendekeza propaganda zinazotolewa na hawa wakoloni hivyo sintokulaumu kwa kuwa huenda ww pia ni katika waathirika hizo media ila jitahidi sana kutafakari kwa kina.

  Nakuombea Mwenyezi Mungu akulinde pamoja na wengine dhidi ya fikra kuwa kila linalofanywa kupitia wakoloni ni sahihi.

  Hizo ndo fikra ambazo walituplant kabla hatujaelimika, kuwa kila kitu kizuri ni cha mzungu, ndo maana utasikia mtu akisema huyu kuku wa kizungu kisa tuu ni mzuri, lakini sijawahi kusikia NZI wa kizungu hata siku moja.

  Hizi zote ni hila za kutufanya tuwaone wakoloni kuwa ni viumbe vitakatifu kabisa kumbe sisi ndo tumewazidi ndo maana binaadamu wa kwanza kabisa (Nabii Adam alikuwa mweusi).

  Tuachane kabisa na hizi fikra za "Ndio Mzee" kwa hawa wakoloni, tujitafakari kwanza na tuungane"TOGETHER WE CAN"
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh inamana kwa hilo nalo kuna haja ya kusema wametumwa??????????????
   
 7. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nani kakwambia Rangi ya Adamu alikuwa mweusi/mweupe vielelezo tafadhali.Inaonekana umeathilika kisaikolojia kama huna ushahidi wa madai yako.Na acheni kukwepa majukumu yenu kwa kisingizio cha wametumwa na marekani,huo ni uvivu wa kufikiri.
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mkubwa! Kama kuna waliobaki hawajui ulichokisema hapa basi wanahitaji tambiko asilia.
   
 9. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ainisha haki unazoziona moja-mbili- tatu!
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nini maoni yako katika hilo! Nashawishika nipate atitude capacity yako kwanza.
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  VOTER sihitaji nipate extraodinary C.V zako kufahamu unathamini utaifa wako na uafrika wako! Shortly unajiamini vile ulivyo UNAJITAMBUA na huyo above rival uliekua ukimpa hizo habari angepata kwnz semina ya KUJITAMBUA,
   
 12. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa msiojua na mnaomtetea Albashir kwa sababu ati ni mweusi..ukweli ni kwamba al bashir ni mwarabu na ameendesha attrocities(na/ama kuunga mkono uhalifu wa waarabu weupe ambao ni wengi) dhidi ya black minority huko jimbo la darfur..
  Na yeye kuna ushahidi wa kumlink moja kwa moja na ule unaomgusa kama kiongozi yani command responsibility yani yeye kama kiongozi badala ya kuwa mastermind ama kukalia kimya uhalifu dhidi ya hao wachache alipaswa kuact responsibly..
   
 13. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MAY ALMIGHTY GOD BLESS YOU

  Asante sana kwa swali zuri, kwa bahati nzuri huwa ninatabia ya kujiamini kwa kila ninachojua kwa kuwa napenda sana kujifunza/kutafiti kabla ya kuamini chochote na sinaga tabia ya kukurupuka au kufuata bendera kama unavyodhania.

  Ushahidi wa kuwa Nabii Adamu alikuwa mweusi:
  Naomba ukaangalie katika Qur'an takatifu iliyotafsiriwa na Sheikh Abdulla Saleh Al-Farsy katika Surat al-Hijr aya ya 28.

  Imeandikwa hivi:
  28:.........Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo mweusi ...ENDELEA.

  Huu ni ushahidi tosha kwa kila mwenye kufikiri, na ndo maana:
  1- Inawezekana kwa mweusi kujichubua awe mweupe (Mfano: Michael Jackson) hii ni kutokana na kuwa ngozi nyeusi ndo ngozi orijino aloumbwa nayo na Mwenyezi Mungu then after yalifuatia mambo ya biologican evolution.

  2-Lakini ni ndoto kwa mweupe kujirekebisha ngozi yake iwe nyeusi(ULIZA MA-DOCTOR NI KWANINI?)

  Natumai kama wewe ni mfatiliaji basi utakuwa umejifuza..
   
 14. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kenya yamwalika al Bashir Nairobi kuhudhuria kikao cha IGAD

  Kenya imemwalika Rais Omar al Bashir wa Sudan kuhudhria kikao cha Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo ya Afirka Mashariki na Pembe ya Afrika -IGAD- kitakachofanyika Nairobi.

  Akizungumza mjini Bujumbura, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula amesema kikao hicho kitakachoongozwa na Rais Mwai Kibaki kitajadili masuala ya amani huko Sudan na Sudan Kusini.
  Mwaliko huo unakuja kufuatia utata uliobuliwa Jumatatu na mahakama moja nchini Kenya iliyotoa hukumu ya kutiwa mbaroni Rais Hassan al Bashir wa Sudan na kukabidhiwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC endapo atafika Kenya.
  Baada ya hukumu hiyo hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilimfukuza balozi wa Kenya mjini Khartoum na kumuita balozi wake aliye Nairobi.

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula amepinga hukumu hiyo ya mahakama na kusema wizara yake itakata rufaa.
   
 15. MpigaKura

  MpigaKura JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2007
  Messages: 385
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sudan yaipa Kenya wiki mbili kubatilisha hukumu dhidi ya al Bashir

  Serikali ya Sudan imeipa Kenya majuma mawili kuwa imebatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama moja mjini Nairobi wa kukamatwa Rais Omar Hassan al Bashir iwapo atakanyaga ardhi ya nchi hiyo. El-Obeid Morawah, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan amesema kuwa, iwapo serikali ya Kenya haitakuwa imetengua hukumu hiyo ya kukamatwa Rais al Bashir baada ya wiki mbili, basi serikali ya Sudan haitakuwa na budi ila kumtimua balozi wa Kenya mjini Khartoum na kumuita balozi wake aliyeko Nairobi.

  Mgogoro huo wa kidiplomasia kati ya Kenya na Sudan ulionekana umeisha baada ya serikali ya Nairobi kutuma ujumbe wa ngazi za juu kumpoza Rais al Bashir na kumuelezea kuwa inafanya kila iwezalo kubatilisha hukumu iliyotolewa na mahakama moja nchini humo, ya kukamatwa kiongozi huyo wa Sudan atakapokanyaga ardhi ya nchi hiyo. Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya Kenya katika kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, iliyotoa kibali cha kutiwa mbaroni kiongozi huyo kwa madai ya kutenda jinai dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur.
   
Loading...