Mahakama Kenya Yaruhusu NASA Kuchunguza Mfumo wa IEBC wa ICT

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Mahakama kuu Kenya imeruhusu chama cha upinzani Kenya kuchunguza mfumo wa ICT wa IEBC jinsi illivyokuwa ikipokea matokeo. Hii ni pigo kubwa kwa Chama cha Jubilee. Uchakuaji kuwekwa hadharani kwani matokeo ya fomu 34A, 34B, 34C lazima ziendane na matokeo yaliyopo kwenye server ya IEBC . NASA wana matokeo yao za hizo fomu na IEBC wameamriwa walete hizo fomu mahakamani.
 
Kuna jambo ambalo sisi kama nchi na wananchi tunapaswa kujifunza kutoka Kenya. Maendeleo ya kweli yanahitaji demokrasia. Demokrasia ni ustaarabu. Nikipewa nichague kati ya maendeleo na ustaarabu, nitachagua ustaarabu maana waliostaarabika wana maendeleo.

Sio lazima na sisi tuuane ndipo tupeane demokrasia ya kweli.
 
Kenyatta ashindwe au ashinde still nitampa heshima yake kwanza kwa kutekeleza maombi yote ya wapinzani but again kwa kuendesha mambo kwa uwazi. Hapa kwetu mbunge wa upinzani kwenda kumpa company mbunge mwenzie tu wa upinzani kwenye jimbo lake is illegal je mambo ya kuingilia issues za TUME!?
 
Kuna jambo ambalo sisi kama nchi na wananchi tunapaswa kujifunza kutoka Kenya. Maendeleo ya kweli yanahitaji demokrasia. Demokrasia ni ustaarabu. Nikipewa nichague kati ya maendeleo na ustaarabu, nitachagua ustaarabu maana waliostaarabika wana maendeleo.

Sio lazima na sisi tuuane ndipo tupeane demokrasia ya kweli.
Sio Kenyatta mkuu ni katiba bora. Sasa hapa kwetu wanasiasa badala ya kuweka mikakati tupate katiba bora bado wanaendesha siasa ya makinikia na ndege.
 
Nakuunga mkono hoja yako kweli kabisa Sio lazima na sisi tuuane ndipo tupeane demokrasia ya kweli
 
Sio Kenyatta mkuu ni katiba bora. Sasa hapa kwetu wanasiasa badala ya kuweka mikakati tupate katiba bora bado wanaendesha siasa ya makinikia na ndege.
Mbona huku hata hiyo katiba haifuatwi! Zuio la mahakama bado watu wanabomolewa! Kenyatta anahitaji compliment zake at least anaheshimu katiba. Huku kwetu ni uchwara uchwara, katiba ya warioba ilitupwa na maccm makafiri kabisa na hutoisikia tena na huyo mbwa akiizungumzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili Tuheshimiane inabidi siku moja watu wachapane sana hakika katiba itawekwa na watu wataheshimiana milele
 
Mbona huku hata hiyo katiba haifuatwi! Zuio la mahakama bado watu wanabomolewa! Kenyatta anahitaji compliment zake at least anaheshimu katiba. Huku kwetu ni uchwara uchwara, katiba ya warioba ilitupwa na maccm makafiri kabisa na hutoisikia tena na huyo mbwa akiizungumzia

Sent using Jamii Forums mobile app
Msingi mkubwa ni katiba mpya kwani hawa majaji pamoja na jaji mkuu hawateuliwi na Rais. Kama ingekuwa katiba ya zamani Kenyatta angekuwa ameapishwa.
 
Msingi mkubwa ni katiba mpya kwani hawa majaji pamoja na jaji mkuu hawateuliwi na Rais. Kama ingekuwa katiba ya zamani Kenyatta angekuwa ameapishwa.
Katiba ya Zanzibar hapo is among the newest state constitutions in the world; yaani ni mpya kushinda hata ile ya Marekani lakini yaliyofanyika uchaguzi mkuu uliopita sote ni mashahidi. Kuwepo kwa Katiba ni jambo moja, na kuiheshimu Katiba ni jambo jingine. Akitokea kiongozi akaiheshimu kama Uhuru anavyofanya basi apewe credits zake!
 
Transparency katika uchaguzi wa Kenya uliopita ni ya kupigiwa mfano sio Afrika tu; bali duniani kote. Kila wapinzani walichotaka walitimiziwa. Uhuru Kenyatta anastahili tuzo ya "baba wa demokrasia Afrika"; yuko vizuri sana yule jamaa.

Naamini kuna vitu vinavyomsukuma Kenyatta kufanya haya yote. Ni marais wachahe sana Afrika wameweza au wanawexa kufanya haya yote. Baadhi ya vitu vinavyomsukuma ni:1. Katiba mpya iliyoleta Tume ambayo ni relatively huru na iliweka mahakama kuwa huru zaidi kuliko huko nyuma. 2. Kukoswa koswa na the Hegue 3. Ukubwa wa Nguvu ya upinzani 4. Experience ya mapigano ya uchaguzi wa miaka iliyopita ambapo kila mtu (mwansiasa) anaelewa hayuko salama binafsi na biashara zake.
 
Back
Top Bottom