calory
Member
- Apr 29, 2013
- 31
- 6
Arusha. Mahabusu zaidi 60 wanaoshikiliwa katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha, eneo la Kisongo, nje kidogo ya Arusha, jana waligoma kushuka kutoka kwenye basi la Magereza lililowapeleka mahakamani na hivyo kukwamisha kesi zao zilizopangwa kusikilizwa au kutajwa.
Mgomo huo uliozua taharuki kubwa kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ulianza mara baada ya gari lililobeba mahabusu kuwasili mahakamani hapo ambapo juhudi za askari Magereza wakishirikiana na wale wa polisi kuwasihi washuke ziligonga mwamba.
Tumechoka kunyanyaswa na kubambikiwa kesi za ujambazi na mauaji zinazotufanya tusote magereza muda mrefu. Tunamtaka jaji aje hapa tuzungumze naye. Hashuki mtu leo hadi jaji na RPC (Kamanda wa Polisi Mkoa), waje tuwaeleze tunavyobambikiwa kesi, walikuwa wakipaza sauti mahabusu hao.
Baada ya juhudi za kuwasihi washuke ili wakatoe malalamiko yao mbele ya mahakama kushindikana, basi lililobeba mahabusu hao liliondoka kwa kasi kurejea gerezani, huku askari polisi na wale wa magereza wakiimarisha ulinzi kote kuanzia mahakamani hadi Gereza la Kisongo kuhakikisha hakuna hujuma yoyote njiani.
Akizungumzia tukio hilo Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Wilbard Mashauri alikiri kushuhudia mgomo huo.