jay311
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 2,932
- 2,720
MH: RAIS MAGUFULI UNANICHELEWESHA KUVUTA SIGARA.....
katikati ya miaka ya tisini mwalimu nyerere ktk moja ya hotuba zake aliwahi kusema ' nchi hii sasa imepoteza heshima yake..
imepoteza heshima iliyokuwa nayo kimataifa naam haipo tena !! Viongozi wake wamekuwa wazembe wala rushwa, wabadhirifu wa Mali ya umma wavivu hawakusanyi kodi wezi wamepoteza uzalendo nk.. Mbele ya jumuia ya kimataifa tunadhalaurika.. baada ya siku chache tutapuuzwa!!
Mwisho wa kunukuu, !
Kipindi hicho nchi ilikuwa haikopesheki.. Serikali ilikuwa inakopa ili kulipa hata mishahara ya wafanyakazi.. (Bora ingekuwa kwa ajili ya maendeleo)
Word bank, BA, IMF nk taasisi za pesa pamoja na wafadhiri wetu wakagoma kuendelea kutukopesha au labda kutusaidia..
Serikali ilikuwa hoi pesa iko kwa watu yenyewe mekumbatia madeni tu. Wakati hali ikiwa tete hivyo serikali ilikuwa km haipo. Kipindi hiki ndipo Agustino mrema akaibuka na kupata umaarufu nkubwa kwani alionekana kama jeshi la mtu mmoja akifanya kazi wizara yake na wizara nyingine nyingi. Rais mwinyi akapagawa na "amsha amsha yake" akampa unaibu waziri mkuu nafasi ambayo haipo kikatiba. Mrema alikuwa waziri wa mambo ya ndani .
Nyerere akaandika kitabu kiitwacho "nchi yetu uongozi, na hatma ya Tanzania" labda kutokana na Giza lililotanda wakati huo!
Mwalimu nyerere ktk hotuba yake niliyoinukuu hapo juu alisema tena "zamani ktk mikutano ya kimataifa ikiwa zamu ya mtanzania kuzungumza km watu wengine walikuwa nje ya ukumbi wa mkutano basi hupigana vikumbo mlangoni kurudi ndani ili waje kusikia "madini"... Lkn cku hizi sivyo akisimama mtanzania kuzungumza watu hutumia fursa hii kwenda nje kupiga cm au KUVUTA SIGARA... (Pumba tupu wanazungumza)
Hakukuchi kunakuchaa...
Mwalimu nyerere akatupa Ben mkapa ( Mr clean) atusaidie..???!!!
Akaja na kauli mbiu "ukweli na uwazi" akaunda tume ya kuchunguza rushwa chini ya Warioba.. ripoti yake mpaka Leo haijulikani ilipo akaishia kutuziba macho kwa kumtoa kafara Mh Nalaira Kiula aliyekuwa waziri wa ujenzi (naibu) basii..
Alipokufa baba wa taifa akatubadirishia kibwagizo.. Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe" viwanda vikauzwa kile cha makaa ya mawe akananihii.. (Najua mmeelewa)
Kelele zilipozidi zikapigwa EPA bil 120 na kutuambia wavivu wa kufikiri..
Akaja Dr jakaya " kasi mpya ari mpya nguvu mpya.. Maisha bora kwa kila mtanzania..
Alipoona hali haikai sawasawa akaongeza "kasi zaidi ari zaidi nguvu zaidi (japo maono hakuna)
Richmond katiba magmash, mikataba ya dharura, (madini & gesi) vitambulisho vya taifa, ujangili, madawa ya kulevya, escrow nk mwisho wa siku deni la taifa kukua hadi kukaribia. trillion 40 toka chini ya trillion 10 miaka kumi iliyopita!
Watu wenye akili ikawa wakiona rais waliomchagua anataka kuzungumza wanatoka nje KUVUTA SIGARA...
mheshimiwa rais magufuli mi nilikuwa na bado naamini kuwa ccm ni ile ile .... Lkn jinsi ulivyoanza umenifanya nisite kwenda kuvuta sigara yangu huku nje japo imkononi mwangu...
Unanishawishi nikutazame kwanza
Nikusikilize... Umeanza shughuli unanivutia najikuta nakupa macho na masikio yangu je unamadini mkuu? Au !!? Naam MH RAIS MAGUFULI UNANICHELEWESHA KUVUTA SIGARA...
by mathew mtenga