AZUSA STREET
JF-Expert Member
- Oct 31, 2013
- 2,007
- 1,898
Kati ya vitu vinavyoniuma moyo ni serikali yetu kutegemea misaada ya wazungu. hii MCCG ambayo tumenyimwa na wamarekan limeshakuwa gumzo, wazungu wanatumia kama fimbo kutuchapia, kipindi cha kikwete walizuia misaada na kuvuruga kabisa bajeti yetu. wakati wa bajeti waliahidi kutoa misaada, tukaweka ahadi zao kwenye bajeti, wakafika katikati wakasema hatutoi misaada tuliyoahidi. huu ni unyama wa hali ya juu. ndugu yangu magufuli naomba unisikilize:
1. kama tukibana mianya yote ya ubadhilifu, tutaweza kukusanya kodi ya kutosha kuendesha nchi.
2. bandari na TRA kuwekewe task force maalumu kuchunguza uchafu wote, na kuzuia uchafu wote ili tukusanye hela.
3. watu waanze kulipa kodi, machine za EFD zianze kutumika ipasavyo.
4. makontena 5000 tu yakipita na kulipa kodi ni hela nyingi sana, angalia hayo waliyotuibia akina masamaki, hela nyingi kumbe inaweza kupatikana kama tukiwa na ulinzi mzuri kuziba mianya ya ubadhilifu.
5. bandari ya dsm, reli ya tazara na ya kati ziboreshwe.
6. USIJIKOMBE KWA WAZUNGU, usijikombe kabisa kwa wamarekani na waingereza, ninachokushauri, angalia nani yupo pamoja na wewe then ambatana na huyo (kwa caution, usiende miguu yote), kwamfano; wachina na wajapan sasaivi wanaonekana hawajatutupa mkono sana, ambatana na hao, watembelee hata nchini kwao. marekani, uingereza na hao mabepari waliokata misaada, achana nao kabisa, waweke pembeni na uonyesha kuwa umewaweka pembeni. USIJIKOMBE, usiwalambe miguu, ukiwaweka pembeni, haitapita muda watarudi wenyewe wakijibembeleza kwako. angalia mwenzio kagame alipowaweka ufaransa pembeni, walijuta wafaransa hadi rais wao akaja rwanda. usihangaike na nchi ambayo haina faida kwa watanzania.
angalia kwamfano hao wa CANADA, na wamarekani ambao wanachimba migodini kwetu ACACIA na geita etc, wanachuma sana lakini hawatoi misaada mingi kwenye nchi zetu, wewe waweke pembeni na anza kuwashughulikia.
UKITAKA NCHI YETU IHESHIMIKE, wafanya hao wazungu wajue kuwa wakija kwetu hawaji kutusaidia tu, wao pia wanapata faida nyingi toka kwetu, hivyo kama hawatakuwa na adabu watashughulikiwa vilevile.
pia, kama wamagaribi wataleta nyodo, waonyeshe kujiunga na uchina, nenda ziarani uchina, wewe kama rais ziara sio siku zote kitu kibaya, mkwere alikuwa anatoka nje ya nchi mara nyingi lakini sio kwamba kwenda nchi za nje ni kitu kibaya moja kwa moja, unatakiwa kubalance, nenda kwenye zile safari za muhimu tu. nenda china, nenda japan. andaa safari yako ya china na japan, india usienda hawana faida kwetu na hawana historia hiyo.
usifikiri kukaa bila kusafiri unapata masifa kwa watanzania waone kama unatunza pesa, kwenda nje kidogo ni kutafuta madili vilevile. sasa ona, wazungu wamezuia msaada ambao ulikuwa unategemea ungesaidia kwenye umeme, ili kuwakomesha waonyeshe kwamba sio lazima sana tuwe marafiki za wazungu, hata wachina na wajapan tunaweza kushirikiana nao. wasalaam!
Tatua mgogoro wa Zanzibar kwanza hayo mengine yatakuja yenyewe......
zanzibar haitanawiri kama bara hawajanawiri. anyway, tusiingie sana huko, lakini point uliyoitoa ni sifuri. kama wewe mzenji, rudini kwenu pemba mkatatue matatizo yenu, msitegemee tuwatatulie sisi, wenzenu kwasasahivi tunachoongea ni hapa kazi tu. na mkifanya mchezo, tutawaacha hatua nyingi sana na kisiwa chenu hicho kinachotegemea tu utalii na biashara za dsm kitakuwa makao ya popo ma wavuta unga. badilikeni.Tatua mgogoro wa Zanzibar kwanza hayo mengine yatakuja yenyewe......
Hapo ndipo utakapomjua Mzungu ni Nani, Nyerere alikoma kwa hao na akasema kabisa kuwa hata korosho wakiamua wanaweza kutupangia bei ya kuuza.
Tena aendelee kujifanya anakomaa uone katika kipindi kigumu kuwahi kutokea katika historian ya Tz itakuwa ni hiki cha Magufuli.
Nyie wengine mnajua kuandika mithamiati tu humu, Watz kwa uchumi tunawazidi Iran? Hebu jaribu kuiangalia Zimbabwe Leo ikoje? Ushauri mbovu sana huu.
Bandari wanaoleta Leo kesho wakipigwa mkwala washushe Mombasa je utakula nini? Na dhadabu yako ukiambiwa haikidhi kiwango? Acheni kasumba za kibantu.
umesema ukweli kabisa. msaada wanaotupatia wazungu, ni sawa na hela ambayo tunaweza kukusanya kwa mwezi mmoja tu hapa Tanzania. na kama tukibana mianya ya rushwa na ubadhilifu, tukawanyonga mafisadi, tunaweza kukusanya hata mara mbili yake na misaada yao tukaikataa. heshima yetu itabaki.Hao jamaa tuachane nao kabisa. Hizo hela zao ndio makusanyo ya mwezi mmoja kwa sasa.
Waambiwe Matonya keshamaliza muda wake wa uongozi. Hadi sasa angekuwa keshaemda Marekani mara tatu au zaidi.
Tatua mgogoro wa Zanzibar kwanza hayo mengine yatakuja yenyewe......
ulimwengu huu wa sasa sio kama ule wa zamani. kwasasaivi wazungu wanatuhitaji sana na tumeingiliana kibiashara kiasi kwamba nao wanaweza kuadhibiwa vilevile. and due to the rise of china, wana hofu sana, ndio maana rais wa china alipotembelea tu tanzania, marais wa marekani walikuja watatu (obama, bush, clinton) kwasababu wanajua kuwa tukiamua kuwatupa watakosa kitu fulani toka kwetu na ukanda huu. kwa miaka ya siku hizi, adhabu pekee watakayoweza kuifanya ni kutugombanisha sisi wa sisi wawapatie waasi silaha ili tupigane, ila mambo mengine hawawezi nakuapia.Hapo ndipo utakapomjua Mzungu ni Nani, Nyerere alikoma kwa hao na akasema kabisa kuwa hata korosho wakiamua wanaweza kutupangia bei ya kuuza.
Tena aendelee kujifanya anakomaa uone katika kipindi kigumu kuwahi kutokea katika historian ya Tz itakuwa ni hiki cha Magufuli.
Nyie wengine mnajua kuandika mithamiati tu humu, Watz kwa uchumi tunawazidi Iran? Hebu jaribu kuiangalia Zimbabwe Leo ikoje? Ushauri mbovu sana huu.
Bandari wanaoleta Leo kesho wakipigwa mkwala washushe Mombasa je utakula nini? Na dhadabu yako ukiambiwa haikidhi kiwango? Acheni kasumba za kibantu.
Hatuwezi kuendesha nchi kwa amri za wahisani, kesho kutwa watatwambia tumalize mgogoro wa wakulima na wafugaji ndo tupewe hela za MCC!