Magufuli tumbua jipu la wizara ya mambo ya ndani

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,199
Mheshimiwa John Pombe Magufuli, ni Rais uliyejipambanua kama mtu usiyeogopa kitu na mwenye uwezo wa kutumbua majipu. Kazi hii ulijipa mwenyewe pale bungeni mwaka jana ulipolihutubia bunge kwa mara ya kwanza. Tunakupongeza sana kwa ujasiri huo na kwa kukubali kujipa kazi ambayo kimsingi ni ngumu na yenye changamoto nyingi. Lakini kwa maslahi ya nchi yetu, na kwa ustawi wa watanzania na kwa amani ya watanzania, tunakuomba yaache kwanza majipu mengine yote, tumbua hili lililopo wizara ya mambo ya ndani.

Wizara ya mambo ya ndani kuna jipu kubwa lililooza na linanuka sana!! Inashangaza sana kwamba Mhe. Rais, hujaliona bado pamoja na kuwepo kwa harufu kali kutoka katika jipu hili.

Hivi sasa amani ya wakazi wa Dar Es Salaam imelegalega sana, wengi wetu hatulali majumbani kwetu na wengine wetu tunashindwa kutoka mapema kwenda kazini na zaidi sana, tunaogopa hata kwenda kuchukua pesa zetu benki kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujambazi na mauaji ya kutisha.

Siku za hivi karibuni kumeibuka kundi la vibaka na majambazi wanaotumia silaha, ambao wanapora magari, wanavunja nyumba na kuua watu na wanawakata mapanga wapita njia humo njiani bila sababu. Kwa mfano kuna baadhi ya maeneo ya Dar Es Salaam hivi sasa wananchi wanalazimika kukesha nje wakilinda nyumba zao na usalama wa wapita njia kutokana na vitendo vya ujambazi kukithiri. Hiyo amani uliyosema utaisimamia kwa nguvu zote wakati wa kampeni ipo wapi kama hatuwezi kulala majumbani mwetu kwa kuhofia kuuawa na majambazi?

Tangu uingie madarakani matukio ya watu kuuawa wakitoka benk kuchukua pesa zao, yameongezeka mara dufu, kiasi cha kwamba watu wanakosa amani na pesa zao halali kisa tu majambazi.

Lakini Mheshimiwa Rais, tetesi zipo nyingi sana juu ya hii hali ya ujambazi wa kuvunja majumbani mwetu na kutuua na hata huu wa magari nk. Tetesi hizi zinatokana na ukweli kwamba majambazi hawa hawakamatwi, na ukiibiwa ukaenda polisi, utaishia kutoa pesa tu pasipo kumukamata mwizi wa mali zako. Tunachojiuliza sisi wengine ni inawezekanaje kwamba waliovamia kituo cha polisi sitaki shari walikamatwa ndani ya wiki moja, halafu wale waovamia majumbani kwetu na kutuua hawapatikani? Humu kuna jipu, ambalo ni la polisi kugeuka kutuua badala ya kutulinda. Kama si wao wanahusika moja kwa moja, basi wanamahusiano ya karibu sana na majambazi. Vinginevyo wangetusaidia kumaliza hili tishio la ujambazi linalotukosesha amani wananchi.

Kwa hakika kabisa, Tanzania hivi sasa si mahali salama pa kuishi kutokana na uwepo wa genge la vibaka wanaotumia mapanga, hasa maeneo yale wanayoishi watanzania wa kawaida, wanaofanya biashara ya genge ambao hulazimika kwenda sokoni mapema sana asubuhi, wananchi wanaotumia usafiri wa daladala ambao hulazimika kutoka mapema asubuhi ili kuwahi foleni, na wananchi wasio na uwezo wa kuweka fence na gril kwenye nyumba zao.

Pia mahali hapa si salama kwa kuishi pia kwa watu ambao walijaaliwa kuwa na kitu kidogo walichokivuna kwa jasho jingi. Maana hao ndiyo wanaovamiwa na majambazi wenye silaha majumbani. Tunajiuliza silaha za moto wanazitoa wapi? Wale watu wako wanaojiita TISS wako wapi? Idara ya upelelezi ya jeshi la polisi ipo wapi? Je ni kweli wameshindwa au na wenyewe ni sehemu ya huo ujambazi?

Mheshimiwa Rais, si vibaya kujifunza kwa wenzako wanaofanya vizuri katika eneo hili. Paul Kagame akiwa mmojawapo. Itapendeza iwapo utapeleka timu ya wataalamu wakajifunze Rwanda, ili tujue wenzetu wamefanyaje katika kuukabili ujambazi. Tumechoka maisha haya ya mashaka katika nchi yetu wenyewe.
 
iNATISHA. HIZI NDIO THREAD ZENYE MAANA BADALA YA WATU WENGI HAPA KUFUNGUA THREAD JUU YA MTU!
 
Hakika mkuu hili jambo ni la maana sana na kinachonishangaza zaidi kipindi kile cha uchaguzi tulilindwa sana na jeshi letu kiasi kwamba amani ilitawala maeneo mengi, sasa najiuliza nguvu ile na magari yale na team ile imeondoka na watu wa NEC mpk baada ya miaka mingine 5 ya uchaguzi?
 
Hakika mkuu hili jambo ni la maana sana na kinachonishangaza zaidi kipindi kile cha uchaguzi tulilindwa sana na jeshi letu kiasi kwamba amani ilitawala maeneo mengi, sasa najiuliza nguvu ile na magari yale na team ile imeondoka na watu wa NEC mpk baada ya miaka mingine 5 ya uchaguzi?
Mimi hapo ndipo nisipoelewa? Maana yake ni nini hasa kutupa ulinzi wakati fulani na wakati mwingine kuuondoa. Kuna kila dalili kwamba wakati ule polisi walikuwa makini ili kuwapa nafasi wapiga kampeni kufanya kampeni nyakati za usiku bila shida. Na wakati ule wagombea wengi walikuwa wanatembea na pesa kwaajili ya kuhonga wapiga kura. Ila kusema ukweli raha ya kuishi nchini mwangu haipo kabisa. Usiku hata mtoto akirusha tu jiwe kwenye bati ya nyumba yako tayari pressure imepanda. Kwanini tunakuwa wakimbizi kwenye nchi yetu jamani?
 
Back
Top Bottom