Magufuli sasa ni kigeugeu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli sasa ni kigeugeu...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Feb 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,247
  Trophy Points: 280
  Magufuli akanusha kubomoa ofisi ya RC Dar


  na Nuru Yanga


  [​IMG] WIZARA ya Ujenzi nchini imekanusha taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kuwa Waziri John Magufuli ameagiza kubomolewa kwa jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam. Tamko hilo lilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Herbert Mrango, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
  Aidha, alisema Waziri Magufuli alifanya ziara Januari 31 mwaka huu kukagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara zinazojengwa jijini Dar es Salaam kama sehemu ya mpango wa serikali kupunguza msongamano wa magari.
  Pia alisema katika ziara hiyo Waziri Magufuli alitoa agizo la kubomolewa jengo la TANROADS ambalo limo ndani ya hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria namba 13 ya mwaka 2007 na si kubomolewa kwa jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa kama ilivyoripotiwa.
  Alisema katika hilo, Magufuli aliwataka watendaji wa TANROADS kutekeleza agizo hilo ndani ya siku tano ili kutoa nafasi kwa kituo cha daladala kilichopo maeneo ya Ubungo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,247
  Trophy Points: 280
  Kwa kiongozi mwenye utashi anapokosea anakiri kuwa amechemsha..............lakini siyo kukanusha kauli yako ambayo imenaswa kwenye na vyombo vya habari lukuki.......................................
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kama ni upanuzi wa barabara na kama jengo la tanroada limebomolewa basi na la mkuu wa moa pia livunje kwani yapo sambamba na yote ni ya serikali.Kwani huyo mkuu wa mkoa hawezi kuhamishiwa pengine?????
   
 4. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani media pia ni binadamu, unaweza kukuta kweli hata hakusema jengo la mkuu wa Mkoa livunjwe,ila chumvi tena za magazetini zinaongezea na kuonekana mzee wa watu kigeugeu.
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,424
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  Magufuli alisema yafuatayo..............
  ........TANROADS wavunje jengo lao ndani ya siku 5..........
  ........Ofisi ya mkuu wa mkoa imo ndani ya hifadhi lakini hakusema nini kifanike juu ya ofisi hiyo.............. MEDIA ZIMECHAMKA NA INABIDI ZIKIRI HIVYO
   
 6. T

  Thegreat Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  I am confused because naamini kwa moyo wangu wote kuwa nilimsikia kwa taarifa ya tv akiagiza ofisi ya RC nayo ivunjwe. Sitaki kuamini kuwa nilikuwa naota!
   
Loading...