Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,442
Wana JF nina jambo la kunena.
Tanzania tunahitaji sana wawekezaji toka nje. Tunatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya nchi yetu. Hata hivyo, kitu ambacho kinanisikitisha sana ni jinsi baadhi ya wafanyakazi toka nje wanaokuja na haya makampuni ya kigeni wanavyowanyanyasa wafanyakazi wa Kitanzania katika kampuni hizo.
Unyanyasaji huu unakuja kwa sura nyingi, kuanzia mishahara duni ukilinganisha na wafanyakazi wa kigeni, matusi na hata kupigwa, udharirishwaji wa kiwango cha juu, ubaguzi wa rangi, ukosefu wa haki za msingi za mfanyakazi, nk. Watu wanafukuzwa kazi kama mbwa bila hata kuzingatia haki zao na wala hakuna hatua zinachochukuliwa dhidi ya wadharirishaji hawa waliojivika sura za wawekezaji.
Katika tawala zilizopita, viongozi wetu wa juu waliwakumbatia sana hawa wadhalilishaji toka nje, kwa kisingizio eti walituletea maendeleo ya uchumi. Viongozi wetu walikubali hata ubaguzi wa rangi unaofanywa na makampuni haya wakati Tanzania ilikuwa kinara wa kupinga ubaguzi wa rangi katika nchi nyingine. Ilifikia hata wakati hawa wafanyakazi wa kigeni walitucheka kwamba tulijifanya tunawakomba wengine dhidi ya ubaguzi wa rangi wakati hapa kwetu wanafanya ubaguzi mkubwa kuliko huko wanakotoka na hawatafanywa chochote na yeyote! Ninaamini kwamba huko nyuma viongozi wetu walikumbatia hawa wadharirishaji toka nje kwa sababu za kifisadi, kwani si rahisi kumkemea mtu anayekupa chochote kifisadi.
Magufuli na Jenista Mhagama, tafadhali tusikubali Watanzania wanyanyaswe, watukanwe, wabaguliwe, wadharauliwe katika nchi yao wenyewe. Kuna sekta ambazo zimekubuhu katika vitendo hivi, kama mahoteli, benki, mawasiliano, viwanda na madini. Tafadhali chukueni hatua. Hatuwezi kuuza utu wa Mtanzania kwa ajili ya fedha ya wawekezaji, ikiwa tuna makaburi ya Watanzania huko Msumbiji na kwingineko ya watu waliokufa kupinga vitu ambavyo leo hii tunaletewa hapa nyumbani Tanzania na tunavikubali na tunakaa kimya. Imefikia kiwango ambacho baadhi ya hawa wawekezaji wanafanya udharirishaji ambao huko kwao wasingethubutu kuufanya. Kwa nini lakini?
Sharti la kwanza kwa muwekezaji yeyote toka nje iwe ni kuheshimu Watanzania. Kama haliwezi na aondoke na fedha yake arudi kwao, ikibidi apewe masaa 24 kuondoka nchini Tanzania.