Magufuli: Nitafuata nyayo za watangulizi wangu

Magufuli: Nitafuata nyayo za watangulizi wangu

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,464
Alisema kazi iliyofanywa na watangulizi wake, imekuwa nzuri na yenye mafanikio, hali ambayo imeifanya Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Milenia (MCC), kuipatia Sh bilioni 992.8 ili kuboresha sekta ya umeme.

Alisema licha ya kurushiwa maneno ya kejeli na matusi na wagombea wa vyama vingine, hatojibu kwa kutukana ila wakati wote atahimiza amani, umoja na mshikamano.

"Nitafanyakazi ya kuijenga Tanzania mpya yenye mabadiliko na maendeleo ya kweli, kwa kuanzia pale walipoishia watangulizi wangu.
"Pamoja na kejeli za kudai hakuna kilichofanyika, hata barabara za lami hawazioni wakati wanapita kila siku na kusafiri… ama kweli shukrani ya punda ni mateke.

"Kama hakuna kilichofanyika, leo hii MCC wangetoa mamilioni ya fedha zote hizi kwa ajili ya nchi yetu… jamani ni Magufuli tu ndiyo anaweza kuwatumikia kwa dhati na moyo wangu wote bila kubagua kwa vyama, dini wala kabila," alisema.
 
1.Huo mshiko haujatolewa, hadi tutakapoweza kupambana na rushwa Kufikia kiwango kinachovumilika next year so anadanganya uma
2.Amesahau kwamba hao viongozi aliwaponda sana wakati ananza campaign zake au hiyo stail haiuzi nayo?
 
Yaani atafuata nyayo za watangulizi wake hawa walioifanya nchi hii idharauliwe kwa kukosa maendeleo pamoja na rasilimali zilizopo? Sasa anapoiga neno MABADILIKO kumbe kaiga neno tuu na sio maana yake.
Mpeni msaada wa kisaikolojia huyu mzee, lazima atakuwa amesha changanyikiwa haelewi anasema nini.
 
Sasa ile dhana ya Magufuli for Change ameshaiacha mara hii? Alifikiri waTZ ni wa kudanganya kwamba ataleta mabadiliko huku Wakiimba kila siku kuwa CCM ni ile ile na kwamba CCM ina wenyewe? Kweli! Mwenye macho haambiwi tazama.

Sasa kama ni kuendeleza yale yale basi bora aachane na kampeni maana watanzania wote wanataka mabadiliko isipokuwa wale tu ambao wanafaidi na mfumo huu wa kinyonyaji na wizi ulioasisiwa na CCM yenyewe.

Ndo maana nasema kura zetu zote tuzielekeze kwa EL maana yuko kinyume na watangulizi waliokwisha kuwa marahisi wa nchi hii
 
Anafuata nyayo za walioifikisha tanzania hapa,sukari kilo 2000 ,petrol bei juu,dola moja 2300, shame on magufuli
 
Nimesoma gazeti la mtanzania leo nikacheka sana...eti Magufuli anasema waliomtangulia wamefanya vizuri kwahiyo na yeye atapita mlemle..

Jamani hivi hawa CCM wanatuona sisi watanzania mazumbukukuu...sijui wanatufikiriaje kwa kweli
 
...Alisema licha ya kurushiwa maneno ya kejeli na matusi na wagombea wa vyama vingine, hatojibu kwa kutukana ila wakati wote atahimiza amani, umoja na mshikamano.
"Nitafanyakazi ya kuijenga Tanzania mpya yenye mabadiliko na maendeleo ya kweli, kwa kuanzia pale walipoishia watangulizi wangu.
"Pamoja na kejeli za kudai hakuna kilichofanyika, hata barabara za lami hawazioni wakati wanapita kila siku na kusafiri…

Hapo kwenye Bold, huo uvumilivu ni wa Lowasa sio Magufuli asilani.

Halafu Magufuli anatakiwa kutofautisha kuambiwa ukweli na kutukanwa...Barabara mbovu zilizojengwa kwa kiwango cha chini kwa gharama kubwa, upotevu wa fedha kwenye wizara yake, huo ni ukweli na wala sio kejeli na matusi..ajibu!
 
kama ndio hivo aaache kushangaaa kwanini hospitalini hakuna dawa maana anajua nyayo za wenziwe asilete usanii
 
Kama ni hivyo tumekwisha!!
Nyayo zipi za kufuata yarabi toba!!
1. Kujibinafsishia makampuni ya Umma?! Kiwira etc..!
2. Kugenisha uchumi 100%!!
3. Kuvumilia mafisadi; wauza mihadarati na majangili!!
4. Kwenda kubembea Ulaya!!
5. Kujenga utawala wa kifalme?!
6. Kuchekacheka na mizaha lukuki kwenye mambo ya msingi?!
7. Kujenga na kuuza tena nyumba za serikali/!
8. Kukataa kuwalipa walimu, wastaafu na watumishi wengine badala yake kuwahonga wasanii mapesa kibao?!
9. Kuendelea kujenga shule za kata zisizo na walimu wala madawati??!!
10. Kujenga utitiri wa hospitali na zahanati zisizokuwa na madaktari,manesi wala dawa??!
11. Kusigina demokrasia?!
12. Kuimarisha chama dola?!
13. Ukatili na uvunjifu wa haki za binadamu, kutesa na kuua kila anayepaaza sauti kudai haki zao??!!ecte ecte ect etc!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.....................
GOD FORBID!!

Back
Top Bottom