Magufuli na ubomoaji wa nyumba zilizo kwenye hifadhi ya barabara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli na ubomoaji wa nyumba zilizo kwenye hifadhi ya barabara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkosikazi, May 25, 2011.

 1. nkosikazi

  nkosikazi JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Mar 11, 2010
  Messages: 354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimefuatilia kwa karibu nikagundua kuwa nchi nzima TANROADS wamekazana kuweka alama za "X" kwenye nyumba ambazo ziko karibu na hifadhi ya barabara. Gharama kubwa sana inatumika kuwapeleka technicians na engineers wa TANROADS kwenda kupima hizo barabara na hulala huko hadi wiki mbili bila kurudi kituoni wakiendelea kula allowances za night na magari yakitumia mafuta mengi kufanya shughuli hii.
  Mimi nashindwa kuelewa utashi wa Magufuli na vipaumbele vyake. Hizo hela zingetumika kwa manufaa mengine kabisa katika ujenzi wa miundombinu imara na kadhalika ikiwa ni pamoja na shule. Wakandarasi wengi hawajalipwa lakini fedha zinatumika kuweka alama za kubomoa nyumba ambazo hazitabomolewa leo wala kesho.
  kwanza sioni mantiki iliyotumika kuongeza upana wa road reserve kutoka mita 22 hadi 30, kwa sababu ipi hasa? Hata huko Ulaya nyumba hazijengwi mbali zaidi ya hapo sembuse sisi Tanzania nchi masikini? kuna haja gani ya kubomoa nyumba ya mtu kajenga mita 22 mbali ya barabara na huwezi kupanua zaidi barabara leo wala kesho? Tuliishaona Sinza ghorofa linabomolewa kwamba liko ndani ya hifadhi lakini ujenzi wa barabara hiyo ya shekilango ulilala miaka mitatu bila kujengwa na walipojenga tulidhani watapanua hiyo barabara lakini badala yake wakajenga the same single lane kwa kuongeza lami juu ya barabara!
  Hivi sasa kuna mradi wa TANROADS wa kuhamisha mawe ya kwenye highway kutoka meter 22 hadi 30 na gharama zake kwa mikoa yote Tanzania haiko chini ya Sh. 9.6billion for nothing kwa dharula ya Magufuli! Are we serious, Tanzania?
   
Loading...