Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,837
Raisi mwenye sifa kama za Magufuli wetu ni wachache sana hapa Duniani, siyo hapa kwetu Afrika tu bali hata nchi zilizoendelea kama Ulaya na Marekani (ambao ndiyo wengi wetu huwaangalia kwamba ndio mfano wa kila lililo jema hapa Duniani hivyo msinihukumu kwa kuendelea kuwatumia kama mfano tumelelewa hivyo) huwa ni mara chache sana kumpata raisi wa aina ya Magufuli!
Na sifa hii kubwa aliyoonyesha Magufuli ni ile ku-challenge Wazungu wanaita ,,status quo" yaani kuendelea kuishi kwa mazoea, nitatoa mfano mdogo sana ambao unaonyesha ni jinsi gani Raisi Magufuli ni intelligent man angalia kitendo tu cha kubadilisha namna kuazimisha siku ya Uhuru, status quo ni kwamba kwa miaka 50 iliyopita kila mwaka tumekuwa tukienda uwanja wa Taifa na kutumia mabilioni kwa ajili ya sherehe hiyo kuanzia JWTZ, dhifa ya Kimataifa mpaka shuguli zote kusimama kwa ajli ya sherehe hiyo sasa Raisi Magufuli akajiuliza swali moja ambalo ni mtu intelligent tu anaweza kujiuliza, Je, kuna haja gani ya kwenda kutumia mabilioni kusherehekea wakati watu wetu wanakufa kwa kipindu pindu? Sasa tunasherehekea nini? Ni kwanini basi tusiutumie muda huu badala ya kusherehekea tusafishe mazingira yetu ili tupambane na huu mlipuko?
Kingine ambacho kimenivutia na kumuona Magufuli wetu ni intelligent man ni pale alipokwenda soko la Samaki feri ktk kusikiliza matatizo ya wavuvi wadogo akaamuru kwamba hakuna haja ya mvuvi mdogo kulazimishwa na SUMATRA kuwa na fire extinguisher wakati ngalawa yake ya kuvulia hata engine haina kwanza yumo majini hivyo maji peke yake ni fire extinguisher sasa kwa nini mvuvi maskini aongezewe gharama kama hiyo? Sasa hapo utaona kwamba SUMATRA wamekuwa wakifwata status quo ya kwamba hiyo sheria ipo tangu ukoloni lkn hakuna mtu sumatra ambaye aliyetaka kufikiri out of the box kama hiyo sheria ina maana yoyote ile kwa mvuvi ambaye hata uwezo kununua injini ya ngalawa yake hana!
Ni sawa na swala la PF3 kwamba ukipata ajali ni lazima kwanza uende Polisi ndiyo utibiwe sasa ni kwa nini? Hii sheria iliwekwa na wakoloni kwa sababu wanazozijua wao wenyewe na ilikuwa ni kwetu Waafrika tu lkn Mzungu akiumia anatibiwa bila ya PF3 tukaichukua kama ilivyo na tunaitumia mpaka leo hii unaweza ukatoka damu mpaka ukafa mapokezi kwa sababu ya kukosa hii karatasi ya Polisi sasa ni kwanini usitibiwe halafu daktari apige simu Polisi na kukufwata hapo hosptalini?
Sasa hii ndiyo maana ya status quo tunafanya kwa sababu tumekuta watu wakifanya hivyo na hamna mwenye uwezo au uthubutu wa kubadilisha hilo na hapo ndipo uintelligent wa Magufuli wetu ulipo!
Mfano mwingine ni kwanini nikienda kulala gesti naulizwa nijaze kabila langu? ili iweje? Au ni kwa nini Polisi anauliza kabila ili nini? Kwa nini wasiulize mimi kuthibitisha uraia wangu kama ni MtanZania ama la? Kabila langu linahusu nini? Na hapa hakuna jibu ni kwa sababu tu wazungu walianzisha hivyo kwa sababu wanazozijua wao tukarithi na tunaendeleza mpaka leo hii hiyo status quo hakuna mwenye uwezo wa kuuliza kwa nini na ina umuhimu gani leo hii? na hapo ndipo Magufuli anapoingia sasa!
Sasa kama viongozi wa Dunia hii wangeweza kujiuliza swali kama la Magufuli na kuchallenge status quo basi Dunia hii ingekuwa mbali kwa mfano ni kwa nini nchi iende vitani kutumia mabilioni wakati wananchi wake hawana kazi, wengi hawawezi kulipa ada ya vyuo vikuu n.k na ndiyo maana Magufuli wetu amekuwa maarufu hata kwa Wazungu na ukisoma maaoni ya magazeti yao wengi wanasema wangependa kuwa Raisi ambaye ana challenge status quo!
Hivyo kama wewe unampinga Magufuli na kwamba hauoni anachofanya basi wewe ndiyo una tatizo na siyo Magufuli wetu, wewe ndiyo wale ambao unakataa kumtibu Mgonjwa kwa sababu hana PF3 na uko tayari kumuacha ateseka hapo, hivyo jitathmini upya maisha yako!