Magufuli na Museveni mshawishini sudan kusini wajenge bomba la mafuta kuelekea uganda

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,994
Kutokana na mradi wa bomba la mafuta linalotoka Uganda hadi tanga nilikuwa napendekeza Raisi Magufuli na Museveni waishawishi Sudani kusini ijenge bomba la mafuta kutoka Sudan kusini hadi uganda ili waunganishe na lile linalokuja Tanzania mafuta yao yaje yaondokee bandari ya Tanga .Bomba hilo likitumiwa na nchi hizo mbili litawasaidia Uganda pia kupunguza gharama za uendeshaji kwani watakuwa wana-share na sudan kusini,

Faida ya Sudan kusini kujenga hilo bomba kupitia Uganda ni kama ifuatavyo

1.Usalama wa hilo bomba kwani linapita maeneo ambayo raia wa sudan kusini na wale wa kaskazini mwa uganda ni ndugu.Wametenganishwa tu na mpaka.Bomba halitapita maeneo ya waasi au yenye tishio la Alshababu

2.Uhusiano wa Uganda,Tanzania na sudan kusini ni mkubwa na wa kuaminika
3.Kwa kupitisha mafuta eneo hilo Sudan kusini itaweza uza mafuta yake kwenye masoko makubwa ya Tanzania,Kongo,rwanda,burundi,Zambia,Malawi na kenya kirahisi pamoja na kusafirisha nje ya nchi kirahisi
4.Umbali wa Kujenga bomba kutoka sudan kusini hadi uganda ni karibu kuliko kulijenga kwenda bandari ya Lamu.Angalia Ramani

east_africa.jpg

yehodaya123@gmail.com
 
Kutokana na mradi wa bomba la mafuta linalotoka Uganda hadi tanga nilikuwa napendekeza Raisi Magufuli na Museveni waishawishi Sudani kusini ijenge bomba la mafuta kutoka Sudan kusini hadi uganda ili waunganishe na lile linalokuja Tanzania mafuta yao yaje yaondokee bandari ya Tanga .Bomba hilo likitumiwa na nchi hizo mbili litawasaidia Uganda pia kupunguza gharama za uendeshaji kwani watakuwa wana-share na sudan kusini,

Faida ya Sudan kusini kujenga hilo bomba kupitia Uganda ni kama ifuatavyo

1.Usalama wa hilo bomba kwani linapita maeneo ambayo raia wa sudan kusini na wale wa kaskazini mwa uganda ni ndugu.Wametenganishwa tu na mpaka.Bomba halitapita maeneo ya waasi au yenye tishio la Alshababu

2.Uhusiano wa Uganda,Tanzania na sudan kusini ni mkubwa na wa kuaminika
3.Kwa kupitisha mafuta eneo hilo Suda kusini itaweza uza mafuta yake kwenye masoko makubwa ya Tanzania,Kongo,rwanda,burundi,Zambia,Malawi kirahisi pamoja na kusafirisha nje ya nchi kirahisi
4.Umbali wa Kujenga bomba kutoka sudan kusini hadi uganda ni karibu kuliko kulijenga kwenda bandari ya Lamu.Angalia Ramani

east_africa.jpg

yehodaya123@gmail.com
Mkuu wazo lako nakubaliana nalo, lifikishe kwa walengwa pale wizara ya nishati na madini
 
mkuu,
sudan kusini wakijenga hilo bomba, itasaidia ktk kuexport mafuta miaka ijayo maana ukanda wa sudan wanayo mafuta.
 
Kinadharia ni wazo zuri lakini kiuchumi je? Total na wabia wenzake wanawekeza kwa mradi na tayari wameshasema uwezo wa bomba ni kusafirisha mapipa laki mbili kwa siku. Bomba lina kipenyo cha karibu nusu mita (inch 24)....ni bomba dogo. Ukileta bomba la Sudani Kusini maana yake linatakiwa kuwa dogo zaidi au sawa na la kutoka Uganda. Also, project economics needs to be revised afresh
 
Ni wazo zuri, ili lije kuunganika na bomba letu hapo uganda moja kwa moja hadi bandari ya tanga

Yaani likiungwa likafika Tanga Sudani kusini inaweza ua soko la mafuta yanayoagizwa uarabuni .Sudan Kusini kwa kuwa ana mafuta mengi sana atakamata soko la afrika mashariki na kati la mafuta.Tanga ni karibu kusafirisha kwa malori kupeleka mafuta hata kenya kupitia mombasa.Wakenya na malori yao ya mafuta watafurika Tanga
 
Sudan wana bomba linalotoka kusini mpaka bandar ya port sudan katika bahar nyekundu, sasa sijui tuwashawishije wageuze kusini/?
 
Habarr nyingine zambia walishagundua mafuta karibu na mpaka wa Angola labda tuwashashawishi wasigeuze bomba mpya Atlantic waunge na la tazama waya pumb east wards ni hayo tu
 
Kutoka juba hadi kampala ni km 112 tu, ile bil nne ya total inatosha kabisa kuanzia juba hadi Tanga, tutupe ndoana tu.
 
Kutoka juba hadi kampala ni km 112 tu, ile bil nne ya total inatosha kabisa kuanzia juba hadi Tanga, tutupe ndoana tu.

Raisi kwa kuwa anaenda Uganda nadhani ataongea na Salva KIIR na Museveni Kuhusu hilo swala.
 
Back
Top Bottom