Mawazo John
Member
- Dec 16, 2015
- 90
- 41
Tunatambua mchango mkubwa na nia ya dhati anayoionyesha Raisi wetu Mheshimiwa Dk. JPM katika kutokomeza na kupambana na kero zote zinazowakabili wananchi pamoja na janja janja za hapa na pale mjini na tunatambua na kukuamini kuwa Ukiamua jambo Halikushindi.
Lakini suala la madalali wengi haswa katika huduma za msingi na za kibinadamu kama makazi na malazi, nikimaanisha madalali wa nyumba na viwanja wanaozidi kuibuka na kuongezeka kwa kasi kubwa kila kukicha katika jiji la Dar es salaam na viunga vyake limezidi kufanya maisha kuwa magumu.
Kero hii si tu kwa vijana wanaoanza maisha bali hata kwa watu wa makamo na wazee wanaotaka kununua viwanja wamekuwa wakitoza asilimia kumi ya bei ambayo hailipiwi kodi ama watu wazima wanaopanga nyumba kutokana na kuhamia Dar kikazi ama kibiashara.
Kundi hili la madalali si tu limekuwa likifanya maisha kuwa magumu bali wanachochea huduma za nyumba kupanda bei kwa kuwashawishi wenye nyumba kupandisha kodi ili wapate fungu nono la malipo ya kodi ya mwezi mmoja wa dalali ambayo ni nje ya kodi ya mwenye nyumba(kama unalipa kodi ya mwaka uongeze iwe ya miezi 13).
Muda mwingine hata ikitokea kwa mfano unaishi Sinza na umeona nyumba ya jirani mpangaji akihama ukavutiwa kuhamia sehemu hiyo anayohama na mwenye nyumba unamfahamu fika, ukimfuata moja kwa moja mwenye nyumba atakuambia "lakini nina dalali wangu anzia kwake kwanza" ambae huenda akawa anaishi hata Chanika kabisa huko ila mchana anashinda Sinza.
Madalali hawa wamekuwa wakisaidia ukwepaji kodi katika mauzo ya bidhaa mbali mbali wanazozidalali huko mtaani pia, kuchochea mfumuko wa bei (inflation) katika bidhaa na huduma hizo, kero kwa wamiliki wa nyumba na viwanja kwa kuwa vin'gan'anizi na wasumbufu pale wanaposikia kuna sehemu inauzwa ama kupangishwa na hata wengine wamegeuka matapeli wakiwatapeli watu wanaojifanya kuwadalalia.
Ingawa uwepo wa madalali hawa umekuwa ukirahisisha upatikanaji wa nyumba au viwanja na bidhaa nyingine haraka lakini madhara yake katika mfumuko wa bei, utapeli na hasara kwa taifa kwa kukwepa kodi ni makubwa.
Hivyo basi kungewekwa utaratibu maalumu wa angalau kuwepo kwa dalali mmoja kwa kila kata/mtaa mfano mfano Sinza, Kimara, Ubungo, Magomeni, Mwenge ambaye atakuwa anatambulika kisheria na halmashauri za manispaa husika na kodi awe analipa kwa kile anachokipata kulingana na viwango na utaratibu mzuri utakaowekwa kabla ya kupewa leseni ya biashara hyo ya udalali kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea tofauti na hali ilivyo sasa ambapo unaweza kukuta Sinza pekee ina madalali 70-100.
Aidha baada ya kuwekwa utaratibu huo na idadi maalumu ya wenye leseni ya kufanya biashara hiyo ya udalali kulingana na taratibu na kanuni zilizowekwa, itangazwe biashara ya udalali Mitaani kiholela ni MARUFUKU na adhabu kali zitolewe kwa atakayebainika kukaidi amri hiyo.
Kwa kumtambua na kumpa kazi hiyo dalali mmoja aliyesajiliwa na kufahamika kisheria kwa mtaa mzima mfano Sinza nzima atahitaji nguvu kazi pia ambapo atakuwa na ofisi kubwa itakayoweza kutoa ajira kwa hao wengine waliopo lakini ikizingatiwa kuwa wanafuata taratibu zote na kanuni za zilizowekwa na si udalali wa kiholela wa kupandisha kodi za pango na bei za viwanja hovyo kila kukicha.
Tusaidie kwa hii kero ya muda mrefu kupitia Viongozi wako wa Wizara na mkoa Husika.