Hivi UKAWA wanafanyaje kuweze kuleta ukombozi wanaodai?[/QUOTE
Simple, ccm ikiwa chama kikuu cha upinzani ubadhirifu wa mali za umma utakuwa mdogo sana kwa kuwa wanafahamu mbinu zote walizotumia kufanya ufisadi, hawatakubali kuona viongozi wa serikali ya ukawa wanaanza kujineemesha kwa ufisadi, watapiga kelele kabla haujafanyika. Kodi zetu zitatumika inavyostahiki. Mishahara itaongezeka kwa kuwa pesa ya kulipa bila longolongo ipo, na miradi ya maendeleo itaongezeka, ajira pia.
Thamani ya shilingi itaongezeka kwa kuwa hatutategemea sana misaada kuendesha nchi yetu, mishahara itakutana. Kwa sasa wakishagawana kodi zetu wanatembeza bakuli nje ya nchi, no free lunch, wanazidi kudidimiza uchumi.
Tukirudisha sura zilezile kwenye uongozi baada ya miaka miwili wataanza kusema bil. 10 ni hela ya mboga, kwa mshahara upi? Baada ya miaka mitano watakuja na ahadi zingine kibao za uongo, ili waendelee kutuvuna. Tutakapohoji walichotufanyia tutaitwa wanywa gongo, sio viroba tena.
Je unafahamu kuwa asilimia 99 ya uchumi wa tanzania unamilikiwa na asilimia 1 ya watu?
Ukombozi utaletwa kwa kufanya asilimia 99 ya watanzania wanufaike na rasilimali za nchi yao, na ccm haiwezi kufanya hivyo, ingeshafanya. Danganya toto ni nyingi huku wanakula wao. Tutakufa tunadanganywa, tuamke, woga wetu ndio umaskini wetu.
Kwa kifupi ccm ikiwa chama kikuu cha upinzani ukombozi wa kweli wa wananchi utaanza kuonekana ndani ya miaka mitano, wanywa viroba kwa mawazo tutaanza kujua ladha ya mvinyo, sio mvinyo waujue wao tu.