Sisi Waafrika tuna safari ndefu sana kuendelea na tatizo kubwa ni kwamba hatuelewi jinsi capitalist economic system inavyofanya kazi na cha kusikitisha na kukatisha tamaa zaidi unakuta watu ambao hawaelewi capitalist economic system wanaishi Ulaya, Marekani au Japani kwa zaidi ya miaka 20!
Wewe unabeza kwamba hili jambo siyo muhimu na halipaswi kushughulikiwa na Raisi wa nchi, nchi kama Marekani kama kuna kiwanda kinafilisika na watu hamsini (50) tu wanapoteza kazi Raisi wa Marekani huwa anaongea na hawa ni watu 50 TU kwenye nchi ambayo unemployment rate iko chini ya 10% sasa ni ajabu sana kwenye nchi kama TanZania ambayo unemployment rate ni zaidi ya 80% nikimaanisha watu ambao wameajiriwa na kulipa Kodi (PAYE) na NSSF unaona kwamba mtu aliyeajiri watu 800 hana umuhimu wa kukutana na Raisi nchi? Hakuna kaya ambayo kuna mtu hatafuti TanZania!
Tanzania ina trade deficit kubwa sana yaani tunachoexport ni kidogo sana kulinganisha na import kwa kifupi hakuna tunacho export ukiachia chai na kahawa na hii nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 leo kuna mtu mwenye soko la Uhakika kuexport Maua Ulaya ana matatizo ambayo yanaweza kutatulika unaona hakuna haja ya yeye kukutana na Raisi wa nchi?
Nchi yetu ina export kwa mwaka 5.5 bilion US dollars tuna IMPORT 11.5 bilion dollars hiyo trade deficit ni kubwa sana yaani tuna import mara mbili zaid ya tunavyo export halafu kuna Mtu ambaye anaajiri watu 800 ana soko la uhakika Ulaya unampuuzia kwamba anaweza tu kukutana Waziri kilimo sasa Waziri wa kilimo anahusika nini na upatikanaji wa umeme au tax system ya nchi?
Halafu tunalalamika kwamba hata tooth picks zinatoka Uchina unafikiri ni kwa nini Uchina wanaweza kuexport toothpicks TanZania?
Siasa haziwezi kututoa hapa mambo ya kudakia sijui katiba bill of rights na upuuzi mwingine wa Marekani hauwezi kuendeleza Afrika hata kwa miaka 500 ijayo, hata mkichukuwa Katiba ya Marekani kama ilivyo hakuna kitu kitafanyika na bado miaka 50 baadaye tutakuwa hapa hapa kama siyo nyuma zaidi, kwa maana tatizo letu Afrika ni sisi Waafrika na siyo Mfumo tunaoutumia!