MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Wakati akiongea na wananchi wa Jiji la Arusha kwa maelfu ambao walimsimamisha kwa nguvu ili asikilize kero zao, Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu walidhani atashirikiana na majizi nchini, lakini kwa sasa wamekwama na atahakikisha anatumbua majizi yote ili nchi iwe kwa faida ya Watanzania wote na iweze kwenda mbele kwa haraka zaidi.
''Kuna majizi yalianza mpaka kuuza nyani na kama nyani wangemalizika, hata sisi tungeuzwa'' Alisema Rais Magufuli.
Aliendelea kusema, ''Uchaguzi umeisha na kinachotakiwa kwa sasa mshikamane kwa pamoja ili tuyatumbue haya majipu kwa nguvu zote. Ninasema, tutayatumbua kweli kweli''.
''Sitangalia unatoka chama gani, uwe CHADEMA, CCM, CUF au huna chama, tutakutumbua tu kama wewe ni jizi. Tunachotaka ni Tanzania yetu iende mbele zaidi'', Alisema.
Alimaliza kwa kusema, ''Haya majizi yamefaidi sana jasho la Watanzania, haitawezekana na haitawezekana waendelee kuiba''.
VIDEO: