Magufuli kulinda wizi wa Mkapa

abuu muhammad

Senior Member
Jul 29, 2015
161
39
July 17, 2015 JOHN Pombe Magufuli, ni mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyepitishwa kuwania nafasi hiyo ili kulinda maslahi binafsi ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa. Anaadika Saed Kubenea … (endelea).

Taarifa kutoka Dodoma na Dar es Salaam, zinaeleza kuwa Mkapa ndiye aliyemshawishi Magufuli kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais. Alisafiri hadi Chato kumtaka achukue fomu ya kuwania nafasi hiyo.

“Yule mzee (Benjamin Mkapa), alisafiri hadi Chato kumtaka Magufuli agombee urais. Unajua kwa nini? Anaogopa kushughulikiwa. Huyu mzee Mkapa ana vimeo vinne vinavyomsumbua. Hivyo anahofu ikiwa mgombea angepitishwa na CCM asingekuwa na uhakika wa kulinda machafu yake,” anaeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya CCM.

Anataja anachoita, “vimeo vya Mkapa” kuwa ufisadi katika ugawaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, nyumba za serikali, uuzaji wa NBC (Benki ya Taifa ya Biashara) na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya madeni ya nje (EPA), ndani ya Benki Kuu (BoT).

Kabla na baada ya kuondoka madarakani, Mkapa amekuwa akitajwa na kuhusishwa na baadhi ya tuhuma za ufisadi na utovu wa “utawala bora” wakati wa kipindi chote cha utawala wake – 1995 hadi 2005.

Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kupitia kampuni yake ya ANBEN anayomiliki na mkewe, Anna ikiwa miongoni mwa makampuni matano yaliyoingia ubia na kampuni ya TanPower Resources Company Limited.

Mkapa, kupitia TanPower Resources Limited, anahusishwa na dhamana ya serikali ya kupata mkopo wa Sh. 17.7 bilioni kutoka CRDB Bank kwa ajili ya kuendeleza mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira.

Kwanza, inadaiwa kuwa Mkapa alimiliki kampuni akiwa bado rais (ANBEN 1998) wa nchi na hivyo atakuwa alitumia nafasi yake kujinufaisha binafsi na kampuni yake.

Pili, kwa kuwa alikuwa bado madarakani na kwa kuwa uamuzi wa kuuza Kiwira ulifanyika ndani ya Baraza la Mawaziri aliloliongoza, basi uamuzi huo ulikuwa wa upendeleo kwa kampuni yake.

Tatu, hata waziri aliyejenga hoja mbele ya baraza la mawaziri, Daniel Yona ametokea kuwa mshirika katika umilikaji wa mgodi huo, jambo ambalo haliendani na utawala bora.

Nne, mkataba wa kampuni ya Mkapa kuuza umeme kwa Tanesco ulifungwa Mkapa akiwa madarakani (Septemba 2005), jambo linaloonyesha upendeleo kwa kampuni yake na utovu wa utawala bora.

Kwa mujibu wa mkataba huo, kampuni ya Mkapa ingelipwa (dola 3.65 milioni – sawa na zaidi ya Sh. 4 bilioni kila mwezi.

Tano, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imegundua mwanzoni mwa mwaka huu, kuwa fedha za mkopo zilizodhaminiwa na serikali (Sh. 17.7 bilioni) hazikutumika kama ilivyokusudiwa.

Kutokana na kutotumia fedha palipohitajika, jenereta moja ya kuzalisha umeme imechakaa kiasi cha kutoweza kufanya kazi; na nyingine ina uwezo wa kuzalisha megawati moja tu ya umeme kutoka megawati sita wakati mgodi unabinafsishwa.

Nyaraka zinaonyesha kuwa TanPower Resources Limited kimkataba ilitakiwa kuzalisha megawati 200 za umeme kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ni kuzalisha megawati 50 kufikia Julai 2007 na megawati 150 ifikapo Machi, mwaka huu. Yote hii sasa ni ndoto.

Uchakavu wa miundombinu umeathiri pia uzalishaji wa mkaa wa mawe na mwekezaji “ameuza baadhi ya vifaa vya mitambo kama vyuma chakavu,” wameeleza wafanyakazi mgodini.

Sita, TanPower Resources Limited imeshindwa kulipa wafanyakazi wake 1,632 kwa karibu mwaka sasa licha ya kuonyesha kwenye mchanganuo wake kwamba ilitenga Sh. 3.0 bilioni kwa ajili hiyo.

Mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira ulioanzishwa kwa msaada wa serikali ya China, Novemba 1988, ulitarajiwa kuzalisha tani 150,000 za mkaa ghafi kwa mwaka na kwamba uzalishaji ungekua hadi kufikia tani milioni moja kwa mwaka.

Nyaraka ambazo Mtendaji Mkuu wa Kiwira Coal and Power Limited (KCP), Francis Tabaro, amekabidhi bunge zinaonyesha Kiwira inamilikiwa na watu wa karibu na Mkapa.

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ilikuwa Kiwira tarehe 16 Januari 2009 katika hatua ya kutaka kujua usahihi wa mmiliki wa mgodi huo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mtoto wa kuzaa wa Mkapa, Nick (Nicholas) Mkapa na mkewe Foster Mkapa, ndio wametajwa kuwa wamiliki wa kampuni ya Fosnik Enterprises, moja ya makampuni yanayomiliki mgodi.

Mkurugenzi mwingine ambaye pia ni mmiliki ametajwa kuwa ni D. Mahembe.

Kampuni ya Mkapa ni miongoni mwa makampuni manne yaliyoungana na “kumilikishwa” mgodi wa Kiwira ambao ulikuwa mali ya serikali kwa asilimia 100. KCP ilianzishwa Julai 2005.

Taarifa hizi zimekuja wakati Mkapa akiwa tayari amewaambia wananchi kijijini kwao kuwa wapuuze tuhuma dhidi yake.

Mkapa alikana kumiliki Kiwira wakati alipoongea na wakazi wa Lupaso, wilayani Masasi, mkoa wa Mtwara, miaka sita iliyopita.

Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, serikali ilikiri bungeni kuwa mgodi wa Kiwira ulikuwa unamilikiwa na Mkapa; lakini ikasema, “mipango iko mbioni kuurejesha mgodi huo serikalini.”

Katika hatua nyingine, majina matano ya wasaka urais kupitia CCM, yalipatikana kabla ya vikao vya chama Dodoma. Majina hayo yaliandaliwa mahususi ili kumbeba Bernard Membe, aliyekuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo.

Taarifa kutoka makao makuu madogo ya CCM, Lumumba na Ikulu jijini zinasema, majina hayo matano yaliandaliwa na mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete na katibu wake mkuu, Abdulrahaman Kinana.

Mkakati wa kutenegeza majina hayo matano kabla ya vikao vya kikatiba vya uteuzi, ulikuwa na lengo la kumzuia Edward Lowassa ili asiweze kupenya ndani ya vikao vya chama hicho – Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC).

Lowassa anatajwa kuwa na uhasama mkubwa na baadhi ya viongozi wakuu wa CCM, akiwamo Kikwete, Kinana, Philip Mangula na Pius Msekwa.

Majina matano yaliyoandaliwa jijini na kufikishwa CC na badaye NEC, yalikuwa January Makamba, Membe, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi Amina Salum Ali na John Magufuli.

Habari zinasema, wapanga mkakati wa kumuengua Lowassa na kumbeba Membe, walijiridhisha kuwa iwapo chama hicho kingewasilisha majina mawili ya wanawake- Amina na Migiro, basi Membe angepenya kiulani.

Hoja iliyotumika ni kwamba January asingeweza kuteuliwa na wajumbe wa mkutano mkuu, huku Magufuli akitajwa kuwa ni mwanasiasa ambaye hakuwa na mtaji ndani ya chama
 
Last edited by a moderator:
Ni kawaida yetu Chadema kila Bunge lazima tuibue "Messi" mpya. Tunaongoza kwa kuvumbua vipaji ... After Slaa, Zitto, Lissu, Mnyika ... Now is your turn Kubenea.
 
Magamba ni yale yale, hakuna jipya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom