Mpalakugenda
JF-Expert Member
- Jun 2, 2015
- 3,880
- 4,115
Amani iwe kwenu wana JF,
Tanzania ni nchi sawa na nchi nyingine zilizopo,inamifumo ya kiutawala sawa na ambavyo nchi hizo zilivyo.
Historia yetu pia ni kama baadhi ya nchi hizo hii ni pamoja kutawaliwa ama na mataifa ya kigeni ama wao kwa wao kwa udikteta.
Wakoloni tunaambiwa katika historia sio walitunyanyasa tu na kutuibia malighafi zetu bali walifanya pia maendeleo ktk nchi yetu.
Tunafahamu kuna shule za mkoloni,hospitali,ofis mbalimbali,barabara pamoja na reli.
Tazama nchi zilizochelewa kupata uhuru walivyopiga hatua kwa sababu tu ya mkoloni.
Pamoja na yote mema ya maendeleo waliyokuwa wanajitahidi kufanya,bado hawakufaa kitu,TULIWAFUKUZA.
Miaka mingi imepita leo tunaye wewe,unafanya maendeleo kama ambavyo umenunua ndege, ujenzi wa hostel, na huu wa reli ya SGR na mengine mengi.
Lakini utawala wako usipokuwa wa haki,amani na kidemokrasia hautakuwa tofauti na mkoloni tuliyemfukuza. Wananchi hawhitaji kupanda lori wakati kuna luxury buses na coaster. Binadamu katika taifa huru wanahitaji kuwa huru,wafanye siasa safi,watoe maoni yao bila kutishwa wala kutekwa.
Pamoja tuifanya Tanzania sehemu salama ya kuishi kwa amani na maendeleo. Hapa kazi tu.