Magufuli hapo vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli hapo vipi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babu Lao, Apr 14, 2011.

 1. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kati ya barabara ambazo zimefanyiwa uchunguzi huo ni pamoja na barabara ya Mandela inayoendelea kukarabatiwa ambapo imegundulika kuwa barabara ya watembea kwa miguu maeneo ya Kituo cha Gereji kata ya Makuburi imegeuzwa kuwa gereji na maegesho ya magari makubwa.

  Cha kushangaza zaidi ni kwamba maegesho na gereji hizo zipo mbele ya Ofisi za Wakala wa Barabara nchini Mkoa wa Dar es Salaam (TANROADS) zilizopo katika Barabara ya Mandela.

  Imebainika kuwa wenye magari makubwa ndiyo wanaovunja sheria za barabarani katika eneo hilo na kugeuza kuwa maegesho na gereji bubu.

  Dar Leo limeshuhudia mara kadhaa magari makubwa yakiwa yamejipanga katika barabara hiyo kwa muda mrefu huku mengine yakiwa kwenye matengenezo.

  Mmoja wa mafundi waliokutwa na gazeti hili akitengeneza gari katika eneo hilo aliyejitaja kwa jina la Abadala Saidi alisema hawana maeneo ya kufanyia kazi hiyo na kwa kuwa wanatafuta riziki wameamua kutumia eneo hilo.

  “Kwa sababu tuna njaa tumeamua kufanya hivi kama unavyotuona. Tumesoma lakini bado ni masikini hatuwezi kukodi gereji za kutengenezea magari makubwa kama haya,”akasema Saidi.

  Akizungumza na Dar Leo jana, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo zilipo gereji na maegesho hayo, James Ngoitanile, amekiri kuwapo kwa tatizo hilo na kudai kuwa madereva hasa wa magari makubwa ndiyo waliogeuza barabara ya watembea kwa miguu kuwa maegesho na gereji bubu katika eneo hilo.

  “Nimeliona hilo na mara kadhaa nimeweza kuwafukuza na kuweka kalipio kali, lakini naona tabia hii inazidi kukua siku hadi siku, kitu ambacho kianweza kusababisha madhara kwa watembea kwa miguu kwa kuwa wanalazimika kupita kwa shida,” amesema Ngoitanile.

  Ngoitanile amewataka wenye magari hayo au wenye tabia ya kutumia barabara kama maegesho kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba kwa sasa anaandaa mkakati maalumu wa kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  kwa kweli hilo la maroli kwenye hiyo barbara ndio kero kubwa, mi nashangaa watu wananunua maroli pa kuyapaki hawana, yamejaakwenye hiyo barabarani kila eneo kuanzia buguruni mpaka external
   
Loading...