Magufuli hana hekima ya kuendesha uchumi

Kessy Wa Kilimanjaro

JF-Expert Member
Jan 23, 2016
327
208
Ambacho Magufuli haelewi ni kwamba anakimbiza wafanya biashara. Kwenye nchi zilizo endelea hauoni raisi yeyote anaye watisha wafanya biashara. Hii ni hatua itakayo fanya sukari iwe bei zaidi kabisa. Alafu ni serekali yenyewe iliyo zuiya sukari kutoka nje kuagizwa alafu sasahivi inaona madhara inajidai kuwa mbabe. Hiki ndo kinachotokea ukiwa na Raisi asiye wahi kusoma kuhusu biashara na uchumi. Tatizo siyo kwamba hamna sukari ya kutosha. Tatizo ni kwamba hamna wafanya biashara wenye uwezo wa kutengeneza hiyo sukari wakutosha. Jinsi ya kuwaongeza hao wafanya biashara ni kwa kuondoa sheria zinazo wazuia wafanya biashara wanje kutaka kuuza sukari yao hapa. Sheria kama za kuwalipisha kodi zisizo na maana wafanya biashara na sheria za kuwazuia wafanya biashara wanje kumiliki mali zinahitaji kuondolewa.
 
Nchi kamwe haiwezi kuendesha kwa staili ya watu kuhujumu uchumi afu ukatoka nyuma ukashabikia upuuuz huuu Biashara huria si kuruhusu mtu afanye anachotaka atatokea mtu na kufanya atakavyo na mtashabikia.
tusiruhusu akili zetu kwenda likizo.

kiongozi wa nchi sio kiongozi wa CHADEMA kwamba maamuz yanaweza fanyika chumban anafanya maamuz ya nchi baada ya kutafakari kwa kina na wataalamu Husika. walituchezea kwenye mafuta tukawashinda sasa kwenye sukari zama zimebadilika watashikwa pabaya
 
Unataka akumbatie wafanyabiashara ambao wanahujumu uchumi na kukwepa kodi ?
 
Biashara huria, soko huria, ushindani huria, bei ya sokoni na sheria za nchi lazima zifuatwe.
 
Itakuwa ukoo au family yako inahusika na sehemu au genge moja linalokamuliwa kipindi hiki,

Sisis wananchi tunamuunga mkono aendelee kukamua tena aongeze speed zaidi ya sasa
 
Biashara huria, soko huria, ushindani huria, bei ya sokoni na sheria za nchi lazima zifuatwe.
Biashara huria bila sheria hyo haipo dunia atatokea mtu anauza mavi nae atasema biashara huria ataangaliwa tu.
mnapo lalamika maisha yapo ghali mlitaka Rais asimamie wap???
 
Uzuri wa JF ni kwamba unakutana na watu wa aina nyingi kama siyo zote.

Jiulize, je sukari ya kutoka nje ilikuwa inaagizwa kiasi gani kwa mwezi?

Je, ilikiwawa inatumia USD ngapi?

Je, kuuza sana bidhaa zetu nje ya nchi na kununua sana bidhaa kutoka nje ya nchi ni kipi kinashusha dhamani ya shilingi yetu?
 
Watanzania walio wengi wanamatatizo nahisi ,kwakwel bado sija waelewa watu hao kwa kutoa kasoro kwenye utawala huu dah very sad kwa kweli.

Kwa style hii hata ashuke MALAIKA kutawal hamta ridhika .
 
Ambacho Magufuli haelewi ni kwamba anakimbiza wafanya biashara. Kwenye nchi zilizo endelea hauoni raisi yeyote anaye watisha wafanya biashara. Hii ni hatua itakayo fanya sukari iwe bei zaidi kabisa. Alafu ni serekali yenyewe iliyo zuiya sukari kutoka nje kuagizwa alafu sasahivi inaona madhara inajidai kuwa mbabe. Hiki ndo kinachotokea ukiwa na Raisi asiye wahi kusoma kuhusu biashara na uchumi. Tatizo siyo kwamba hamna sukari ya kutosha. Tatizo ni kwamba hamna wafanya biashara wenye uwezo wa kutengeneza hiyo sukari wakutosha. Jinsi ya kuwaongeza hao wafanya biashara ni kwa kuondoa sheria zinazo wazuia wafanya biashara wanje kutaka kuuza sukari yao hapa. Sheria kama za kuwalipisha kodi zisizo na maana wafanya biashara na sheria za kuwazuia wafanya biashara wanje kumiliki mali zinahitaji kuondolewa.

Kakojoe ulale.!
 
Uzuri wa JF ni kwamba unakutana na watu wa aina nyingi kama siyo zote.

Jiulize, je sukari ya kutoka nje ilikuwa inaagizwa kiasi gani kwa mwezi?

Je, ilikiwawa inatumia USD ngapi?

Je, kuuza sana bidhaa zetu nje ya nchi na kununua sana bidhaa kutoka nje ya nchi ni kipi kinashusha dhamani ya shilingi yetu?

Nime penda swali lako. Ukweli ni kwamba kutuma sukari yetu nje inaongeza thamani ya shillingi kwasababu watu watakuwa wananunua kutoka kwetu kupitia shilingi. Lakini tatizo ni kwamba kwetu hatuna viwanda vingi vya kutosha kutengeneza kiwango hicho cha sukari mpaka tuwe tuna tuma. Njia ya kuongeza viwanda ni kwa kurahisisha ufanya biashara wa aina hiyo no kuondoa vikwazo vilivyo wekwa na serikali juu ya wafanya biashara wote hata wa nje.

Cha pili hata kama tuna nunua sukari kutoka nje nyingi zaidi ya ile tunayo tengeneza, haimaanishi kwamba uchumi wetu haukui. Hiyo sukari inanunuliwa na wafanya biashara ili waiuze. Wakiuza wanapata faida na wana changia kwenye GDP. Ikiwa raisi kununua sukari kutoka nje kutakuwa na wafanya biashara wengi, kitu ambacho kitaongeza mashindano kwenye hiyo sekta na kushusha garama ya sukari.

Wauza sukari wanaweza kuongeza bei kwasababu ni wao pekeyao wanao uza hiyo sukari. Lakini tuki rahisisha wawe watu wengi wanao uza sukari tutaona bei inashuka gafla kwasababu ya mashindano.
 
Biashara huria, soko huria, ushindani huria, bei ya sokoni na sheria za nchi lazima zifuatwe.

Lakini unacho sema ni kwamba sheria iliyopo sahivi ni halali. Lakini ukiangalia maafa yanayo sababishwa na hiyo sheria kwenye uchumi na uwezo wa kuishi wa wananchi utaona kwamba haifai. Tatizo ni kwamba sheria yetu imeandikwa na socialist/communist wasio elewa uchumi. Hawajali haki za kumiliki mali na uhuru wa biashara na bila hizo haki hamna uchumi utakao kua.
 
Biashara huria bila sheria hyo haipo dunia atatokea mtu anauza mavi nae atasema biashara huria ataangaliwa tu.
mnapo lalamika maisha yapo ghali mlitaka Rais asimamie wap???

Na watakao nunua mavi utawazuia kisa wewe haupendi hayo mavi. Je unawazuiyaga watu wanao nunua sigara kisa wewe haupendi sigara. Au unawazuiaga watu ambao wanakula vyakula ambavyo hauvipendi kisa tu wewe hauvipendi na una uwezo wa kuwazuia. Unahitaji kuelewa kwamba chaguo la watu na jinsi wanavyo ishi maisha yao haikuhusu wewe. Kama mtu hamdhuru mwengine na wamekubaliana kufanya biashara sheria haitakiwi kuingilia.
 
Back
Top Bottom