Elections 2015 Magufuli hafai kuwa kiongozi mkubwa wa nchi, unaikumbuka hii

mandago shululu

Senior Member
Mar 24, 2013
124
34
TUTAKUWA WAKWELI KUSEMA UKWELI, WIZARA YA UJENZI IMEACHA DENI KUBWA KUZIDI WIZARA ZOTE.

JE,MAGUFURI ANATUFAA KUWA RAIS?

Hii ni sehemu ya taarifa na jinsi gani ufisadi katika wizara ya ujenzi iliyotolewa mbele ya Bunge Tarehe28/05/2014 Alhamisi.Bado tunakumbukumbu hatuwezi kamwe kumpa Nchi

Kuna ufisadi katika ununuzi wa kivuko cha Bagamoyo na wengine kueleza kuwa miradi iliyotajwa kwenye hotuba ya bajeti ilishatekelezwa miaka ya 80 na 90.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti, Profesa Juma Kapuya, deni linalodaiwa na makandarasi ni kati ya Sh850 bilioni na Sh900 bilioni.

"Kamati haijaridhishwa kabisa na hali hii kwani deni hili sasa ni kubwa kuzidi hata bajeti inayotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wizara hii, jambo ambalo linafanya bajeti hii kuonekana ni kiini macho tu," alisema Profesa Kapuya.

KAMBI YA UPINZANI

Katika taarifa yake, Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) ilimshutumu Waziri Magufuli kwa kuandika hotuba ndefu ili kuwachanganya wabunge, huku hotuba hizo zikitaja hata miradi ya barabara zilizojengwa miaka ya 80 na 90.
Akiwasilisha maoni ya hiyo, msemaji wa KUB - Wizara ya Ujenzi, Felix Mkosamali alisema Serikali ya Awamu ya Nne inajigamba kwa kujenga kilomita 13,000 za barabara, lakini kiasi hicho ni kidogo ukilinganisha na kilomita 86,000 zinazotakiwa kujengwa.

Alisema KUB inaelewa vizuri mtandao wa barabara nchini na sehemu kubwa ya barabara hizo zilikuwa zimeshajengwa wakati wa Rais Benjamin Mkapa na sehemu ndogo tu zilikuwa zimebaki kuunganishwa.
"Kuna mtandao wa barabara wa Dar - Kagera, Dar - Kigoma, Dar - Songea, Dar – Tunduma na Dar - Masasi zilikuwa na lami wakati Serikali ya Mkapa inamaliza muda wake, nyingine zilikuwa zimebakiza vipande vichache vya kuunganishwa," alisisitiza Mkosamali.

Alitoa mfano barabara ya Dar es Salaam – Chalinze yenye urefu wa kilomita 100, kuwa imetengewa Sh2.45 bilioni ambazo hatoshi kwa lolote.
Pia alihoji barabara ya Uyovu – Bwanga – Biharamulo, kilomita 112 ambayo imetengewa Sh4.97 bilioni bila ufafanuzi wa jinsi fedha hizo zitakavyotumika.

"Tutamwelewa Magufuli kama atatuambia ni shilingi ngapi zinajenga kilomita moja ya barabara kwa kiwango cha lami, kinyume cha hapo ni kupeana matumaini yasiyokuwepo," alisema Mkosamali ambaye ni mbunge wa Muhambwe (NCCR – Mageuzi

KIVUKO DAR - BAGAMOYO

Mkosamali alisema kivuko cha Dar es Salaam – Bagamoyo kilichonunuliwa kwa zaidi ya Sh8 bilioni ili kupunguza msongamano ni cha zamani na hakina uwezo.

Alilitaka Bunge kuunda tume kuchunguza ununuzi wa kivuko hicho kwa sababu ni kibovu na cha zamani na kilinunuliwa kwa gharama kubwa.

"Ni jambo la ajabu kununua kivuko cha kizamani au chakavu chenye spidi ndogo. Bakhresa ana meli inayotoka Dar kwenda Zanzibar kwa muda wa dakika 90 tu na inabeba abiria 500 na kwa taarifa tulizonazo inauzwa kati ya Sh4 bilioni na Sh5 bilioni tu," alisema.

"Mbwembwe na kelele za Magufuli kwamba watanunua meli kupunguza foleni zimegonga mwamba kwa kununua kivuko kibovu na cha kizamani kinachokosa abiria," alisema.

FOLENI DAR ES SALAAM
Mkosamali alisema Serikali haina dhamira ya kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam kwa sababu barabara za juu (flyovers) ambazo Dk Magufuli amekuwa akizisema, hazijajengwa licha ya kuwa wazo hilo lilitolewa katika hotuba yake ya bajeti ya 2011/12.

Alisema mpaka sasa, angalau ingekuwapo barabara moja ya juu na kueleza kushangazwa na taarifa ya Dk Magufuli kwamba mkataba kwa ajili ya ujenzi wa flyover ya Tazara utasainiwa Juni nchini Japan.

Suala hilo pia liliungwa mkono na Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu ambaye licha ya kukosoa bajeti kuwa haina lolote jipya, alisema wizara imeshindwa kujenga barabara za pembezoni mwa mji ambazo zingepunguza misongamano kwa kiasi kikubwa. Alisema suala hilo limekuwa likiwekwa kwenye bajeti katika miaka ya karibuni, lakini halitekelezwi na hali inazidi kuwa mbaya.

Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alisema ili kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam, Serikali inatakiwa kuwekeza katika usafiri wa reli ili kupunguza magari yanayobeba makontena bandarini.

Mbatia, ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema Januari 13, 2009, alimwandikia barua Waziri Mkuu kumshauri asitishe ujenzi wa maghorofa katikati ya jiji, na kusisitiza kuwa ujenzi wa majengo makubwa yasiyopangiliwa limekuwa chanzo cha foleni.

"Kila siku Taifa linapoteza Sh4 bilioni kutokana na msongamano wa magari. Hizo ni fedha nyingi ambazo zingeweza kutufikisha mbali. Eti fedha za barabara wanapeleka kwenye BVR, tangu lini fedha za barabara zikapelekwa kwenye BVR," alihoji mbunge huyo.

Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema wizara hiyo ndiyo pekee yenye deni kubwa na makandarasi wanashindwa kuendelea na kazi. Aliitaka serikali kulipa madeni hayo ambayo ni zaidi ya Sh850 bilioni.

Mandago.
K/tibu Chadema ( W) Kwimba
 
Umefunguka watanzania tumelogwa ni kama kuku akikamatwa kifaranga wake na kimbulu anasahau halafu anarudi palepale haya yote yalikuwepo mjengoni leo wamesahau yote Escrow .Richmond etc imebaki magufuli hivi tumelogwa?
 
Inashangaza sana kuona watanzania walivyo wepesi kusahau na wasiopenda kuchunguza uhalisia wa mambo, magufuli ni compromise candidate, mnufaika wa vita ya makundi na kwa sababu Amekuwa sehemu ya serikali iliyopo, hawezi kukwepa lawama kwa makosa yaliyotokea, Kwangu mimi doa kubwa sana litakalomuandama magufuli daima ni uuzwaji wa nyumba za serikali wakati wa utawala wa mkapa, na huyu mama samia ushiriki wake kwenye kuvuruga mchakato wa katiba unatusaidia kumjua ni mtu wa namna gani, mwaka huu watanzania wana hiari ya kuchagua mabadiliko ya kweli au kuendelea kupumbazwa na mihemko ya kisiasa na kuendelea na status quo.
 
1. Nyumba za Serikali
Kwa hakika hili ni doa kubwa sana kwa Magufuli. Ni katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ujenzi (awamu ya 3) alishawishi kwa nguvu na msukumo mkubwa sana mpaka kufanikiwa uuzaji wa nyumba za serikali.

Hii hatua ya Magufuli halina tofauti na kile alichokiita CAG Professor Assad “Political Entrepreneurship”. Professor Assad mara baada ya kuingia madarakani alisema wazi kwamba mradi wa Magufuli wa kuuza nyumba za serikali ni ufisadi mkubwa sana. Professor Assad alizidi kusema ya kwamba alichokifanya Magufuli yalikuwa kwa manufaa yake binafsi na ilikuwa ni “personal political entrepreneurship”.

Katika uamuzi huo, Magufuli alienda mbali zaidi mpaka kugawa bure baadhi ya nyumba kwa ndugu zake na mahawara zake. Kwa mfano Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel iliyopo Mwenge/Bamaga jijini Dar es Salaam. Dada Kabula ambaye hajawai kuwa mtumishi wa umma tokea awamu ya kwanza mpaka leo hii Ocampo ninaposhusha huu uzi alifanikiwa kuhongwa nyumba mbili zenye Plot No. MSM/201 na Plot No. MK/521 (Mikocheni na Msasani).

Kwa hatua hiyo Magufuli aliliingiza serikali hasara kubwa sana, na hayo machungu mpaka leo hayajaisha na serikali bado linaendelea kubeba mzigo. Katika kipindi hiki tumeshuhudia watumishi wengi (Majaji, na watendaji wakuu, makatibu wakuu) wamekuwa wakiishi hotelini, huku gharama za vyumba zikiwa za hali ya juu sana almost dola 1200-1500 kwa mwezi ambayo ni sawa na Millioni 27 kwa mwezi; kwa mwaka ni Millioni 324 kwa mtumishi moja.

2. Ujenzi wa Barabara
Eneo hili ni sehemu nyingine ambayo Magufuli amekuwa akijipatia fedha haramu. Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kusema kwamba ni TANROADS ndiyo wahusika wakuu katika barabara na siyo Magufuli. Ingawa hoja yao siyo ya kweli na haina mashiko.

Kiutaratibu na sheria barabara utakiwa kuwa na upana (width) wa 6.5m ila imegundulika barabara nyingi kipindi hichi cha Magufuli zimekuwa zikijengwa kwa 5.7m to 6m na siyo 6.5m, je fedha za hizo baki 0.5m to 0.8m zinakwenda wapi, ni wazi fedha hizo uingia mifukoni mwa Magufuli na washirika wake wa Tanroads. Vile vile ni kipindi kirefu sasa Highway Economic Assessment ya miradi ya barabara imekuwa hazifanyiki kitu ambacho kinapelekea barabara zetu nyingi kuwa chini ya viwango. Utafiti wa Ocampo unaonyesha kwamba barabara kuwa chini ya viwango ni swala la makusudi ambapo waziri na wasimamizi wa miradi husika wanakula na kugawana fedha za miradi….

3. Sakata La Bomoa Bomoa
Ni jambo la wazi ya kwamba sheria zimetumgwa ili zifuatwe, lakini kuwa na ubinadamu au utu ni zaidi ya sheria. Ni Magufuli huyu huyu alipigwa stop na Mh. Rais pale alipoona Magufuli anakiuka wazi haki za binadamu. Ubomoaji wa nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara umekuwa hauzingatii “UTU”. Ni jambo la wazi wanaanchi wengi waliobomolewa nyumba zao mpaka sasa wako katika hali ngumu ya maisha na hawana uelekeo baada ya kufanyiwa unyama usiyothimilika na Magufuli.

Either wataalamu wengi pale wizarani katika mahojiano wanasema Magufuli hana tabia ya kufata sheria na utaratibu, wakitolea mfano swala la kuvunjwa kwa jengo la TANESCO (Ubungo) na jengo la Millenium Towers. Kwa hakika ni jambo jema sana kuwa na Rias kama JK aliyediriki kumpiga stop Magufuli, hivyo basi ni wazi anapaswa apate mtu wa juu yake katika kufanya maamuzi, ila yeye ndiyo akiwa mtoa maamuzi walai nchi tutaipoteza (Tafakari kwa kina).

4. Shelly Ya Mwanza
Tukizidi kukumbuka sakata la Shelly ya Mwanza ndipo tunazidi kujua jinsi gani Magufuli ni mtu wa kukurupuka na mtu mwenye chuki. Kwa chuki zake binafsi kipindi cha awamu ya 3 akiwa waziri wa ujenzi aliamuru kuvunjwa kwa Shelly ya bwana Mansoor (mbunge wa Kwimba) iliyopo maeneo ya madaraka misheni jijini Mwanza. Baada ya ukiukwaji huo wa sheria bwana Mansoor alienda mahakamani na kisha kushinda kesi na hukumu kutolewa kwamba serikali imlipe Mansoor mabillioni ya fedha, sababu kubwa zikiwa ni chuki na kisasi cha Magufuli……

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki
Sifa zingine pekee za Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa. Hayo mambo yamepelekea hata utendaji kazi wa watumishi wa chini kuwa mgumu sana. Watumishi chini ya wizara yake wanasema Magufuli ni mtu mwenye majivuno sana, ni mtu mwenye chuki na ni mtu asiyepokea ushauri wa mtu yeyote yule zaidi ya mke wake na Kabula…

6. Umiliki wa Kebby’s Hotel
Kebby’s Hotel ni hoteli iliyopo Mwenge/Bamaga upande wa kulia kama unaenda posta/mjini. Kwa muda mrefu mmiliki wa hoteli hiyo amekuwa akijificha katika mgongo wa mtu mwingine ila ukweli ni kwamba mmiliki halali wa hoteli hiyo ni John Pombe Magufuli na siyo Dada Kabula.

Umiliki wa Hoteli kubwa kama Kebby’s ambayo kulala ni zaidi ya dola 60-90 inaonyesha wazi kwamba Magufuli ni fisadi wa kimya kimya kama yule jamaa mwingine aliyepiga za Escrow na vibali vya sukari au yule aliyechimbia fedha za Ghadafi kwenye mahandaki.

7. Kuvunja Ndoa
Katika maandiko Matakatifu, Kumbukumbu la Torati 27: 14 imeandikwa alaaniwe yule amtamaniye mke wa nduguye au jirani yake. Ila kinyume na hayo maandiko Matakatifu Magufuli amediriki kumtamani mke wa jirani yake mpaka kupelekea kuvunja ndoa ya mtu.

Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel, awali alikuwa mke wa Januarius Maganga ambaye ni mtumishi mwandamizi katika makampuni ya IPP Media. Swali la kujiuliza kama Magufuli kadiriki kuvunja ndoa ya mtu angali ni waziri wa kawaida tu, je akiwa Rias itakuwaje? Jibu nafkiri unalo…. Na sitaki unipe jibu.

Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kutolea mfano sakata la waziri mdogo wa Uingereza aliye onekana na kimada barabarani. Kwa tamaduni za hao wenzetu huo ulikuwa ukosefu mkubwa wa maadili mpaka ikapelekea kufukuzwa kazi na waziri mkuu wa wakati huo.

8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri
Ni jambo la wazi na ukweli usiopingika kwamba Taifa linatafuta Rais bora na kwa upande mwingine CCM kinatafuta mtu mwenye uwezo wa kushika kofia mbili kwa pamoja.

Magufuli ana utamaduni wa kutumia chama pale anapoitaji madaraka, ila pale tu anapoyapata hayo madaraka anakuwa ajiusishi na mkakati wowote wa kujenga chama. Historia inaonyesha Magufuli hajawahi kushika wadhifa au nafasi yoyote ile ndani ya chama, wanachama wa CCM wanauliza kwamba watamkabidhi vipi mtu asiye na background nzuri kwenye chama? Vile vile historia inaonyesha hajawahi kuchangia hata senti tano katika shughuli zozote zile zenye lengo la kujenga chama.

9. Sakata La Samaki
Katika muendelezo wa kukurupuka katika maamuzi, Waziri Magufuli mwaka jana tena aliliingiza Taifa na serikali kwa ujumla katika hasara nyingine. Ambapo serikali iliamuriwa na mahakama ilipe kiasi cha shilling Billioni 2.8 na kurudiha meli husika baada ya kukiuka sheria za kimataifa pale alipokamata Meli yenye vibali halali na iliyokuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Sasa kama ni waziri wa kawaida anadiriki kuvunja sheria za kimataifa, Je akiwa Rais si ni wazi anaweza kulipelekea Nchi ikatengwa na jumuiya za kimataifa….. we need to think kwa umakini sana wakuu…..

10. Sakata La Kivuko
Dhana ya ubinadamu siyo kuvaa nguo au kulala kwenye nyumba bali ubinadamu ni pamoja na kuwa na hekima, busara na kauli nzuri kwa binadamu wenzako; cha kushangaza Magufuli alidiriki kutumia lugha iliyotafsiriwa kama tusi kubwa sana na wananchi wa Dar es Salaam, pale alipoowambia wapige mbizi wakitaka kwenda Kigamboni. Ni jambo jema kwa kiongozi kuwa na msimamo ila msimamo wake uendane na lugha nzuri, ya uungwana na ya ubinadamu. Ni wazi kauli hiyo iliwauzinisha sana na kukasirisha wananchi wengi Dar es Salaam. Ubinadamu na utu ni kitu cha bure na siyo cha ulazima, hivyo ilitegemewa Magufuli awe na kauli nzuri na yenye hekina na busara kwa wananchi husika.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….

NB: Je kuna Magufuli Mwingine au ni huyu huyu?...............
 
magufuli ni tingatinga wapinzani wataisoma namba
 
Nchi hii inaitaji kiongozi bora atakaye weza kuitoa hapa ilipofikia kwani nchi inapumlia mashine.. Na kiongozi hyo hawezi kupatikana ndani ya ccm...
 
"Gunia la sukari haliwezi badili chumvi ya bahari".. Mfumo Fisadi wa CCM ni mgumu ukizigatia wanaowafadhili katika kampeni ni hao hao mafisadi. Je, JPM anaweza kata kiganja chake??? Stay tuned:majani7:
 
TUTAKUWA WAKWELI KUSEMA UKWELI, WIZARA YA UJENZI IMEACHA DENI KUBWA KUZIDI WIZARA ZOTE.

JE,MAGUFURI ANATUFAA KUWA RAIS?

Hii ni sehemu ya taarifa na jinsi gani ufisadi katika wizara ya ujenzi iliyotolewa mbele ya Bunge Tarehe28/05/2014 Alhamisi.Bado tunakumbukumbu hatuwezi kamwe kumpa Nchi

Kuna ufisadi katika ununuzi wa kivuko cha Bagamoyo na wengine kueleza kuwa miradi iliyotajwa kwenye hotuba ya bajeti ilishatekelezwa miaka ya 80 na 90.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti, Profesa Juma Kapuya, deni linalodaiwa na makandarasi ni kati ya Sh850 bilioni na Sh900 bilioni.

“Kamati haijaridhishwa kabisa na hali hii kwani deni hili sasa ni kubwa kuzidi hata bajeti inayotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wizara hii, jambo ambalo linafanya bajeti hii kuonekana ni kiini macho tu,” alisema Profesa Kapuya.

KAMBI YA UPINZANI

Katika taarifa yake, Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) ilimshutumu Waziri Magufuli kwa kuandika hotuba ndefu ili kuwachanganya wabunge, huku hotuba hizo zikitaja hata miradi ya barabara zilizojengwa miaka ya 80 na 90.
Akiwasilisha maoni ya hiyo, msemaji wa KUB - Wizara ya Ujenzi, Felix Mkosamali alisema Serikali ya Awamu ya Nne inajigamba kwa kujenga kilomita 13,000 za barabara, lakini kiasi hicho ni kidogo ukilinganisha na kilomita 86,000 zinazotakiwa kujengwa.

Alisema KUB inaelewa vizuri mtandao wa barabara nchini na sehemu kubwa ya barabara hizo zilikuwa zimeshajengwa wakati wa Rais Benjamin Mkapa na sehemu ndogo tu zilikuwa zimebaki kuunganishwa.
“Kuna mtandao wa barabara wa Dar - Kagera, Dar - Kigoma, Dar - Songea, Dar – Tunduma na Dar - Masasi zilikuwa na lami wakati Serikali ya Mkapa inamaliza muda wake, nyingine zilikuwa zimebakiza vipande vichache vya kuunganishwa,” alisisitiza Mkosamali.

Alitoa mfano barabara ya Dar es Salaam – Chalinze yenye urefu wa kilomita 100, kuwa imetengewa Sh2.45 bilioni ambazo hatoshi kwa lolote.
Pia alihoji barabara ya Uyovu – Bwanga – Biharamulo, kilomita 112 ambayo imetengewa Sh4.97 bilioni bila ufafanuzi wa jinsi fedha hizo zitakavyotumika.

“Tutamwelewa Magufuli kama atatuambia ni shilingi ngapi zinajenga kilomita moja ya barabara kwa kiwango cha lami, kinyume cha hapo ni kupeana matumaini yasiyokuwepo,” alisema Mkosamali ambaye ni mbunge wa Muhambwe (NCCR – Mageuzi

KIVUKO DAR - BAGAMOYO

Mkosamali alisema kivuko cha Dar es Salaam – Bagamoyo kilichonunuliwa kwa zaidi ya Sh8 bilioni ili kupunguza msongamano ni cha zamani na hakina uwezo.

Alilitaka Bunge kuunda tume kuchunguza ununuzi wa kivuko hicho kwa sababu ni kibovu na cha zamani na kilinunuliwa kwa gharama kubwa.

“Ni jambo la ajabu kununua kivuko cha kizamani au chakavu chenye spidi ndogo. Bakhresa ana meli inayotoka Dar kwenda Zanzibar kwa muda wa dakika 90 tu na inabeba abiria 500 na kwa taarifa tulizonazo inauzwa kati ya Sh4 bilioni na Sh5 bilioni tu,” alisema.

“Mbwembwe na kelele za Magufuli kwamba watanunua meli kupunguza foleni zimegonga mwamba kwa kununua kivuko kibovu na cha kizamani kinachokosa abiria,” alisema.

FOLENI DAR ES SALAAM
Mkosamali alisema Serikali haina dhamira ya kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam kwa sababu barabara za juu (flyovers) ambazo Dk Magufuli amekuwa akizisema, hazijajengwa licha ya kuwa wazo hilo lilitolewa katika hotuba yake ya bajeti ya 2011/12.

Alisema mpaka sasa, angalau ingekuwapo barabara moja ya juu na kueleza kushangazwa na taarifa ya Dk Magufuli kwamba mkataba kwa ajili ya ujenzi wa flyover ya Tazara utasainiwa Juni nchini Japan.

Suala hilo pia liliungwa mkono na Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu ambaye licha ya kukosoa bajeti kuwa haina lolote jipya, alisema wizara imeshindwa kujenga barabara za pembezoni mwa mji ambazo zingepunguza misongamano kwa kiasi kikubwa. Alisema suala hilo limekuwa likiwekwa kwenye bajeti katika miaka ya karibuni, lakini halitekelezwi na hali inazidi kuwa mbaya.

Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia alisema ili kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam, Serikali inatakiwa kuwekeza katika usafiri wa reli ili kupunguza magari yanayobeba makontena bandarini.

Mbatia, ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema Januari 13, 2009, alimwandikia barua Waziri Mkuu kumshauri asitishe ujenzi wa maghorofa katikati ya jiji, na kusisitiza kuwa ujenzi wa majengo makubwa yasiyopangiliwa limekuwa chanzo cha foleni.

“Kila siku Taifa linapoteza Sh4 bilioni kutokana na msongamano wa magari. Hizo ni fedha nyingi ambazo zingeweza kutufikisha mbali. Eti fedha za barabara wanapeleka kwenye BVR, tangu lini fedha za barabara zikapelekwa kwenye BVR,” alihoji mbunge huyo.

Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema wizara hiyo ndiyo pekee yenye deni kubwa na makandarasi wanashindwa kuendelea na kazi. Aliitaka serikali kulipa madeni hayo ambayo ni zaidi ya Sh850 bilioni.

Mandago.
K/tibu Chadema ( W) Kwimba

Alianza kuvuma Lowasa mkaibua mambo kebe ya escrow, akapigwa chini akavuma Membe mkavumisha muhindi wa dodoma akapigwa chini, saiv kavuma magufuli mshaanza vumisha, mlikuwa wap kueleza izo nyaraka za magufuli akati Lowasa au Membe wanavuma??? Yaan Hakuna raisi ataepita bika kuvumishiwa ata kikwete mliibua mambo kibao yakowap.....tushazoea Mmechelewa waungwana
 
1. Nyumba za Serikali
Kwa hakika hili ni doa kubwa sana kwa Magufuli. Ni katika kipindi alichokuwa Waziri wa Ujenzi (awamu ya 3) alishawishi kwa nguvu na msukumo mkubwa sana mpaka kufanikiwa uuzaji wa nyumba za serikali.

Hii hatua ya Magufuli halina tofauti na kile alichokiita CAG Professor Assad “Political Entrepreneurship”. Professor Assad mara baada ya kuingia madarakani alisema wazi kwamba mradi wa Magufuli wa kuuza nyumba za serikali ni ufisadi mkubwa sana. Professor Assad alizidi kusema ya kwamba alichokifanya Magufuli yalikuwa kwa manufaa yake binafsi na ilikuwa ni “personal political entrepreneurship”.

Katika uamuzi huo, Magufuli alienda mbali zaidi mpaka kugawa bure baadhi ya nyumba kwa ndugu zake na mahawara zake. Kwa mfano Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel iliyopo Mwenge/Bamaga jijini Dar es Salaam. Dada Kabula ambaye hajawai kuwa mtumishi wa umma tokea awamu ya kwanza mpaka leo hii Ocampo ninaposhusha huu uzi alifanikiwa kuhongwa nyumba mbili zenye Plot No. MSM/201 na Plot No. MK/521 (Mikocheni na Msasani).

Kwa hatua hiyo Magufuli aliliingiza serikali hasara kubwa sana, na hayo machungu mpaka leo hayajaisha na serikali bado linaendelea kubeba mzigo. Katika kipindi hiki tumeshuhudia watumishi wengi (Majaji, na watendaji wakuu, makatibu wakuu) wamekuwa wakiishi hotelini, huku gharama za vyumba zikiwa za hali ya juu sana almost dola 1200-1500 kwa mwezi ambayo ni sawa na Millioni 27 kwa mwezi; kwa mwaka ni Millioni 324 kwa mtumishi moja.

2. Ujenzi wa Barabara
Eneo hili ni sehemu nyingine ambayo Magufuli amekuwa akijipatia fedha haramu. Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakijaribu kusema kwamba ni TANROADS ndiyo wahusika wakuu katika barabara na siyo Magufuli. Ingawa hoja yao siyo ya kweli na haina mashiko.

Kiutaratibu na sheria barabara utakiwa kuwa na upana (width) wa 6.5m ila imegundulika barabara nyingi kipindi hichi cha Magufuli zimekuwa zikijengwa kwa 5.7m to 6m na siyo 6.5m, je fedha za hizo baki 0.5m to 0.8m zinakwenda wapi, ni wazi fedha hizo uingia mifukoni mwa Magufuli na washirika wake wa Tanroads. Vile vile ni kipindi kirefu sasa Highway Economic Assessment ya miradi ya barabara imekuwa hazifanyiki kitu ambacho kinapelekea barabara zetu nyingi kuwa chini ya viwango. Utafiti wa Ocampo unaonyesha kwamba barabara kuwa chini ya viwango ni swala la makusudi ambapo waziri na wasimamizi wa miradi husika wanakula na kugawana fedha za miradi….

3. Sakata La Bomoa Bomoa
Ni jambo la wazi ya kwamba sheria zimetumgwa ili zifuatwe, lakini kuwa na ubinadamu au utu ni zaidi ya sheria. Ni Magufuli huyu huyu alipigwa stop na Mh. Rais pale alipoona Magufuli anakiuka wazi haki za binadamu. Ubomoaji wa nyumba zilizopo pembezoni mwa barabara umekuwa hauzingatii “UTU”. Ni jambo la wazi wanaanchi wengi waliobomolewa nyumba zao mpaka sasa wako katika hali ngumu ya maisha na hawana uelekeo baada ya kufanyiwa unyama usiyothimilika na Magufuli.

Either wataalamu wengi pale wizarani katika mahojiano wanasema Magufuli hana tabia ya kufata sheria na utaratibu, wakitolea mfano swala la kuvunjwa kwa jengo la TANESCO (Ubungo) na jengo la Millenium Towers. Kwa hakika ni jambo jema sana kuwa na Rias kama JK aliyediriki kumpiga stop Magufuli, hivyo basi ni wazi anapaswa apate mtu wa juu yake katika kufanya maamuzi, ila yeye ndiyo akiwa mtoa maamuzi walai nchi tutaipoteza (Tafakari kwa kina).

4. Shelly Ya Mwanza
Tukizidi kukumbuka sakata la Shelly ya Mwanza ndipo tunazidi kujua jinsi gani Magufuli ni mtu wa kukurupuka na mtu mwenye chuki. Kwa chuki zake binafsi kipindi cha awamu ya 3 akiwa waziri wa ujenzi aliamuru kuvunjwa kwa Shelly ya bwana Mansoor (mbunge wa Kwimba) iliyopo maeneo ya madaraka misheni jijini Mwanza. Baada ya ukiukwaji huo wa sheria bwana Mansoor alienda mahakamani na kisha kushinda kesi na hukumu kutolewa kwamba serikali imlipe Mansoor mabillioni ya fedha, sababu kubwa zikiwa ni chuki na kisasi cha Magufuli……

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki
Sifa zingine pekee za Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa. Hayo mambo yamepelekea hata utendaji kazi wa watumishi wa chini kuwa mgumu sana. Watumishi chini ya wizara yake wanasema Magufuli ni mtu mwenye majivuno sana, ni mtu mwenye chuki na ni mtu asiyepokea ushauri wa mtu yeyote yule zaidi ya mke wake na Kabula…

6. Umiliki wa Kebby’s Hotel
Kebby’s Hotel ni hoteli iliyopo Mwenge/Bamaga upande wa kulia kama unaenda posta/mjini. Kwa muda mrefu mmiliki wa hoteli hiyo amekuwa akijificha katika mgongo wa mtu mwingine ila ukweli ni kwamba mmiliki halali wa hoteli hiyo ni John Pombe Magufuli na siyo Dada Kabula.

Umiliki wa Hoteli kubwa kama Kebby’s ambayo kulala ni zaidi ya dola 60-90 inaonyesha wazi kwamba Magufuli ni fisadi wa kimya kimya kama yule jamaa mwingine aliyepiga za Escrow na vibali vya sukari au yule aliyechimbia fedha za Ghadafi kwenye mahandaki.

7. Kuvunja Ndoa
Katika maandiko Matakatifu, Kumbukumbu la Torati 27: 14 imeandikwa alaaniwe yule amtamaniye mke wa nduguye au jirani yake. Ila kinyume na hayo maandiko Matakatifu Magufuli amediriki kumtamani mke wa jirani yake mpaka kupelekea kuvunja ndoa ya mtu.

Dada Kabula ambaye ni mmiliki hewa wa Kebby’s Hotel, awali alikuwa mke wa Januarius Maganga ambaye ni mtumishi mwandamizi katika makampuni ya IPP Media. Swali la kujiuliza kama Magufuli kadiriki kuvunja ndoa ya mtu angali ni waziri wa kawaida tu, je akiwa Rias itakuwaje? Jibu nafkiri unalo…. Na sitaki unipe jibu.

Nyerere katika moja ya hotuba zake aliwahi kutolea mfano sakata la waziri mdogo wa Uingereza aliye onekana na kimada barabarani. Kwa tamaduni za hao wenzetu huo ulikuwa ukosefu mkubwa wa maadili mpaka ikapelekea kufukuzwa kazi na waziri mkuu wa wakati huo.

8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri
Ni jambo la wazi na ukweli usiopingika kwamba Taifa linatafuta Rais bora na kwa upande mwingine CCM kinatafuta mtu mwenye uwezo wa kushika kofia mbili kwa pamoja.

Magufuli ana utamaduni wa kutumia chama pale anapoitaji madaraka, ila pale tu anapoyapata hayo madaraka anakuwa ajiusishi na mkakati wowote wa kujenga chama. Historia inaonyesha Magufuli hajawahi kushika wadhifa au nafasi yoyote ile ndani ya chama, wanachama wa CCM wanauliza kwamba watamkabidhi vipi mtu asiye na background nzuri kwenye chama? Vile vile historia inaonyesha hajawahi kuchangia hata senti tano katika shughuli zozote zile zenye lengo la kujenga chama.

9. Sakata La Samaki
Katika muendelezo wa kukurupuka katika maamuzi, Waziri Magufuli mwaka jana tena aliliingiza Taifa na serikali kwa ujumla katika hasara nyingine. Ambapo serikali iliamuriwa na mahakama ilipe kiasi cha shilling Billioni 2.8 na kurudiha meli husika baada ya kukiuka sheria za kimataifa pale alipokamata Meli yenye vibali halali na iliyokuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Sasa kama ni waziri wa kawaida anadiriki kuvunja sheria za kimataifa, Je akiwa Rais si ni wazi anaweza kulipelekea Nchi ikatengwa na jumuiya za kimataifa….. we need to think kwa umakini sana wakuu…..

10. Sakata La Kivuko
Dhana ya ubinadamu siyo kuvaa nguo au kulala kwenye nyumba bali ubinadamu ni pamoja na kuwa na hekima, busara na kauli nzuri kwa binadamu wenzako; cha kushangaza Magufuli alidiriki kutumia lugha iliyotafsiriwa kama tusi kubwa sana na wananchi wa Dar es Salaam, pale alipoowambia wapige mbizi wakitaka kwenda Kigamboni. Ni jambo jema kwa kiongozi kuwa na msimamo ila msimamo wake uendane na lugha nzuri, ya uungwana na ya ubinadamu. Ni wazi kauli hiyo iliwauzinisha sana na kukasirisha wananchi wengi Dar es Salaam. Ubinadamu na utu ni kitu cha bure na siyo cha ulazima, hivyo ilitegemewa Magufuli awe na kauli nzuri na yenye hekina na busara kwa wananchi husika.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari
Magufuli siyo mtu wa kawaida kabisa, ndani yake amejaa chuki na visasi. Ni mtu wa visasi vya ajabu, hii inanikumbusha alipogombea ubunge 1995 na bwana Ernest Nyororo. Baada ya kushindwa katika kura za maoni ila baadaye alipoteuliwa bila uwoga alianza kumshughulikia Nyororo mpaka ikampelekea Nyororo akapata shinikizo la moyo. Kumbuka Nyororo ni ndugu yake wa damu sasa sisi wengine itakuwaje, ni wazi hili jambo linaitaji tafakari ya kina. Kama ndugu yake anaweza kumshambulia kiasi hicho iweje watu wa kawaida….. Leo Ocampo nikiwa naandika huu uzi sisiti kusema ya kwamba hata hao viongozi wanaotaka Magufuli apitishwe naomba niwaambie kwa chuki na kisasi cha Magufuli kuna siku atawabadilikia tena sana sana. Huko mbeleni naomba msije mkasema Ocampo hakutuambia….. Nina hakika asilimia zaidi ya 100 Magufuli ana chuki na viongozi waandamizi wa sasa, chuki hiyo anasubiri kuilipiza muda ukifika….

NB: Je kuna Magufuli Mwingine au ni huyu huyu?...............

Mlikua wap kutoa hizo takwimu akat lowasa na membe wanavuma???? Lowasa mkavumisha escrow Membe mkavumisha muhindi wa dodoma saiv mmehamia uku, tushazoea mmechelewa waungwana
 
Alianza kuvuma Lowasa mkaibua mambo kebe ya escrow, akapigwa chini akavuma Membe mkavumisha muhindi wa dodoma akapigwa chini, saiv kavuma magufuli mshaanza vumisha, mlikuwa wap kueleza izo nyaraka za magufuli akati Lowasa au Membe wanavuma??? Yaan Hakuna raisi ataepita bika kuvumishiwa ata kikwete mliibua mambo kibao yakowap.....tushazoea Mmechelewa waungwana

'namna hii haitoki bali kwa kufunga na kuomba'
 
Stupid!
Lete na ripoti ya fedha ya CDM tuone hapa!
Slaa anapiga hela hapo CDM na mkewe hujaona umeona ya Magufuli???
Subirieni watu tuandae maandiko kuhusu Slaa, Mkewe na Mbowe kuhusu ufisadi then watu wataamua Fisadi ni nani Kati ya Magufuli na Slaa pamoja na Mbowe!
September - October sio mbali, subirieni tu!
 
Alianza kuvuma Lowasa mkaibua mambo kebe ya escrow, akapigwa chini akavuma Membe mkavumisha muhindi wa dodoma akapigwa chini, saiv kavuma magufuli mshaanza vumisha, mlikuwa wap kueleza izo nyaraka za magufuli akati Lowasa au Membe wanavuma??? Yaan Hakuna raisi ataepita bika kuvumishiwa ata kikwete mliibua mambo kibao yakowap.....tushazoea Mmechelewa waungwana

Hakuna alilovumishiwa hata moja hapo...tofauti yake na wengine ni kuwa yeye mambo yake mengi yalikuwa underground.

Afu anajua kula na vipofu...yaani anapiga sana kazi afu pia anaiba!
 
Back
Top Bottom