Magufuli dhibiti uingizaji wa chumvi kama ilivyo sukari

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
1,651
3,815
Tanzania viwanda vingi vya chumvi vimekufa kutokana na uingizaji wa chumvi kutoka nje hivyo kufanya soko la viwanda vingi vya chumvi kudorora.

Ili kuinua viwanda vingi nchini inatubidi kuanza na viwanda vinavyotengeneza bidhaa muhimu za mahitaji ya nyumbani ikiwemo chumvi kama alivyofanya kwenye sukari.

Udhibiti huu utafanya kuanza kwa uwekezaji wa mahitaji muhimu kama chumvi hivyo kuinua pato la nchi na upatikanaji wa ajira nchini.

Katika stage ya viwanda ni bora tuanze na viwanda vya mahitaji ya muhimu ya kila siku kuliko kuanza na viwanda vikubwa kama vya magari wakati soko lake ni dogo kutokana na level ya uchumi ya watanzania.

Kulikua na viwanda vingi vya chumvi now vimekufa.
 
Bwana Mwijage upooo! Mtoa bango naungana nawe kabisa. Hongera sana kwa kuwakumbusha wahusika. Chumvi nayo inatoa ajira kwa watanzania wengi sio sukari pekee. Au kwa vile wawekezaji wengi hawana pa kusemea kama walivyo wa sukari?
 
Back
Top Bottom