MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,997
Wakati akiongea na wananchi wa Jiji la Arusha, Rais Magufuli amesema biashara ya sukari inavyoendeshwa Tanzania ni kama biashara ya madawa ya kulevya kwa sababu inamilikiwa na kikundi cha watu fulani wachache ambao pia wanafanya kila linalowezekana ili wananchi wengine wasipate fursa ya kufanya biashara hiyo.
Rais ameenda mbele zaidi na kudai, ‘’kuna kikundi cha watu kimejipanga, watu fulani, group la watu fulani, kwamba wao ndio wafanyabiashara pekee wa sukari nchini’’.
Rais amewapa changamoto viongozi wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuangalia uwezekano wa kuanzisha viwanda vya sukari ili kuhakikisha nchi inaondokana na utegemezi wa vikundi vya watu fulani waliojipanga ili kumiliki biashara ya sukari nchini.
Rais alisema kwa mfano mifuko ya hifadhi ya jamii ingekuwa na viwanda vya sukari, leo hii watanzania wasingechezewa na hao wafanyabiashara wanaoficha sukari na hata kama ingepungua, tungewaambia ninyi muagize sukari ambayo ni bora.
Rais alisema, ''sukari hata ukiiagiza nje, bei yake haiwezi kuzidi shilingi mia nane kwa kilo na watu wakapata faida''.
''Hawa watu wanaoficha sukari hawana uchungu na maisha ya watanzania'' Rais alisema.
VIDEO: