Magufuli aunguruma BRELA!

Magufuli aunguruma BRELA!

Joined
Mar 27, 2009
Posts
75
Reaction score
5
Wana jamvi leo katika pitapita zangu za kuganga njaa nilijikuta nikiwa BRELA. Katika kupita huku na kule nikamuona Maghufuli akiwa na maafisa wa BRELA akistaajabu mafaili kuhifadhiwa hadi miguuni kwa maofisa wa Brela. Baadaye nikapata taarifa kuwa walimpa kisingizio kuwa hawana jengo na mafaili ni mengi sana. Nampongeza angalau kwa kuhoji ile hali kwani sijawahi kusikia waziri mwenye dhamana ya BRELA (WA VIWANDA NA BIASHARA) katembelea Agency hiyo nyeti serikalini. BRELA mtaendelea kuhifadhi mafaili kama maembe hadi lini? Mbona pesa mnakusanya?

NAWASILISHA!
 
its sad! inapunguza sana ufanisi, ukienda tu faili lako linachukua 2 hours kutafutwa, au unaambiwa utafute mwenyewe.wanapata pesa za kutosha walitakiwa wafanye computerazation .......tutafika tu mzee
 
Jamani kuna watu wanajituma.

Huyu Kaka yetu Mh. J.P.Maghufuli, kweli anafanya kazi. Kila anakopita anaacha ukumbusho, yaani ana-deliver kuliko wenzie wengi. 50% ya cabinet ingekuwa na watu wa aina yake, sijui tungekuwa wapi sasa.
 
Huwa najiuliza sana ninapopita nje ya baadhi ya majengo, na kuona kupitia madirisha ya vioo, mafaili yakiwa yamebebana na kujifinya kwenye vioo mpaka juu. Siachi kujiuliza kuwa shughuli huwaje pale faili la chini kabisa linapohitajika. Au je, ni rahisi kupata faili mtu analolihitaji kweli? Matokeo yake, muda mwingi si utapotea mtu akitafuta faili moja tu? Vinginevyo, si mtu atakwamisha shughuli zote zihusuzo faili fulani just because she/he can't be bothered kulitafuta?
 
Hivyo ndivyo nchi yetu ilivyo jamani sio huko BRELA tu ofisi nyingi hiyo ndo habari,hata mahospitalini ukienda habari ndo hiyo faili litatafutwa mpaka utakasirika,iliwahi kunitokea nimeenda hospital na nilikua nimekwenda kutoa nyuzi baada ya operation you know ilikuwaje,nimefika mapokezi nimetoa kadi ili kuwapa namba ya faili,ilikua shughuli faili lilitafutwa halikuonekana,kilichonisaidia alipita doctor ambae alikua ameni-attend siku ya operation aliponiona akakumbuka ni siku ya kutoa nyuzi alipoelezwa kuwa faili halionekani akaniambia twende ukapate huduma watakapolipata watalileta,faili lilikuja kuonekana baada ya saa moja na nusu,kwa hiyo jamani sijui tutrekebisha vipi hilo swala katika nchi yetu maana,
 
mazoea hujenga tabia,

kwan wana sababu yoyote ya maana ya kutoweka mafile ktk system nzuri?!!

upuuzi mwingi tu
bado natafuta nauli nikiipata huko mjini hapatatosha
 
Hawatakawia kusema Magufuri anaingilia ya wengine kama ilivyotokea kwa Lyatonga.
 
Wana jamvi leo katika pitapita zangu za kuganga njaa nilijikuta nikiwa BRELA. Katika kupita huku na kule nikamuona Maghufuli akiwa na maafisa wa BRELA akistaajabu mafaili kuhifadhiwa hadi miguuni kwa maofisa wa Brela. Baadaye nikapata taarifa kuwa walimpa kisingizio kuwa hawana jengo na mafaili ni mengi sana. Nampongeza angalau kwa kuhoji ile hali kwani sijawahi kusikia waziri mwenye dhamana ya BRELA (WA VIWANDA NA BIASHARA) katembelea Agency hiyo nyeti serikalini. BRELA mtaendelea kuhifadhi mafaili kama maembe hadi lini? Mbona pesa mnakusanya?

NAWASILISHA!

Washanga hilo? nenda pale central polisi station maelezo ya watuhumiwa yachukuliwa kwenye vipande vya mifuko ya cementi iliyotumika!!!!!!!!!
 
Last edited:
Sasa Magufuli nae kawa mkubwa sasa, kama kweli anauchungu na nchi yetu anaogopa nini upresidenti! Ajikaze tuu, aanze mchakato na mikakati ya nguvu ndani na nje ya chama mapema (lakini si kama alivyofanya Kikwete kuhonga watu). Tunaweza kupata kiongozi angalau wa maanamaana kiasi.
 
Bila shaka huyu shujaa hana uchu na madaraka ndiyo maaana hana haraka na hayo unayoyawaza ila anapokuwa kapewa jukumu hulitekeleza kwa ufanisi wa kutosha,na labda anaangalia wakati muafaka pia wa kuomba kugombea Urais,ILA NI MCHAPA KAZI SAHIHI,MIMI BINAFSI NAFURAHISHWA NA KUJITUMA KWAKE
 
... kwani sijawahi kusikia waziri mwenye dhamana ya BRELA (WA VIWANDA NA BIASHARA) katembelea Agency hiyo nyeti serikalini.

Sasa kama BRELA iko chini ya Viwanda na Biashara, waziri wa Uvuvi alienda kukagua BRELA kwa msingi gani?
 
Hivyo ndivyo nchi yetu ilivyo jamani sio huko BRELA tu ofisi nyingi hiyo ndo habari

Karibu ofisi zote za serikali sasa hivi zina computer lakini zinatumika kama typewriters tu! Secretary na boss wake wote wana computer na wangeweza kupunguza matumizi ya simu kwa kutumia programmes kama ya Skype wakawasiliana ndani na nje ya wizara kwa mazungumzo ya kawaida tu lakini hakuna hata wazo la kufanya hivyo wala kutumia computer walizo nazo kuhifadhi kumbukumbu za ofisi zao, tuna safari ndefu sana kwani Magufuli pekee hatoshi...
 
Jamani kuna watu wanajituma.

Huyu Kaka yetu Mh. J.P.Maghufuli, kweli anafanya kazi. Kila anakopita anaacha ukumbusho, yaani ana-deliver kuliko wenzie wengi. 50% ya cabinet ingekuwa na watu wa aina yake, sijui tungekuwa wapi sasa.

Wewee mamah, Magufuli ana tatizo moja kubwa, anafanya kazi kiukweli kuiwazidi mabosi wake kiasi cha kufikia kuwafunika. Hili ni kosa kubwa sana kwa siasa zetu za bongo. just consider coverage yake kwenye vyombo vya habari wakati wa Benjamini/Fredrick na wakati wa Jakaya /Edward. maana hata baada ya kkuondoshwa miundo mbinu na kupelekwa ardhi wakaona utendaji unazidi kuboreshwa wakaona wamtupe huku aliko sasa. ajabu anazidi kufanya makubwa.
 
Tungekuwa mbali ata kama ingekuwa ni 25% tu achilia mbali 50%
 
Wewee mamah, Magufuli ana tatizo moja kubwa, anafanya kazi kiukweli kuiwazidi mabosi wake kiasi cha kufikia kuwafunika. Hili ni kosa kubwa sana kwa siasa zetu za bongo. just consider coverage yake kwenye vyombo vya habari wakati wa Benjamini/Fredrick na wakati wa Jakaya /Edward. maana hata baada ya kkuondoshwa miundo mbinu na kupelekwa ardhi wakaona utendaji unazidi kuboreshwa wakaona wamtupe huku aliko sasa. ajabu anazidi kufanya makubwa.

Hii nchi sijui imelaaniwa!!!! Akitokea mtu kufanya yanayotakiwa na wengi watatafuta mbinu ili wammalize!!
 
Sasa kama BRELA iko chini ya Viwanda na Biashara, waziri wa Uvuvi alienda kukagua BRELA kwa msingi gani?
Iko hivi,huyu jamaa ana guest house yake huko Biharamulo alienda BRELA yeye mwenyewe kwaajili ya kusajili Business name ya hiyo biashara yake ndiyo akakutana na hiyo hali na akasema akitoka hapo ataenda kushughulikia TIN number TRA yeye mwenyewe na kufuatilia leseni pia ila ajionea mazingira ya hizo taasisi husika hadi atakapokamilisha anachofuatilia.
 
Kwa hiyo Magufuli anafanya biashara kinyume na maagizo ya mwajiri wake kwamba viongozi wachague moja.

Halafu anakwenda BRELA na TRA kwa shughuli zake binafsi lakini anaanza ``kuhoji`` na ``kujionea mwenyewe mazingira`` ya taasisi hizo japokuwa haziko chini yake.

Na alipataje access ya kuingia wanakohifadhi makabrasha? Alitakiwa asimame mbali, asisogee kabisa kwenye makabrasha kama alienda kwa shughuli binafsi. Kuna tatizo hapa, au taarifa ina tatizo. Au vyote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom