Napenda kumwambia Johnson Mbwambo, magufuli hawezi kushinda kwa haki hata afanye nini. CCM haiwezi kushinda kwa haki!!! Labda waibe, wakishindwa wamshurutishe mwenyekiti wa tume ya uchaguzi atangaze matokeo batili kama ilivyokuwa wa Kenya. Otherwise sio rahisi. Fanya utafiti rahisi tu, sehemu yoyote umekaa, iwe baa au hotel au kijiweni, angalia wastani wa watu wanaosapoti ukawa na wale wa CCM. Kwenye watu 10 wa ukawa watakuwa 8 na wa CCM 2 au mmoja. Hata kama kijijini wakaja na wastani wa 6 CCM, 4 ukawa. CCM hawawezi shinda. Unadanganywa na mafuriko ya CCM ya kubeba na malori. Lakini mambo yamebadilika. Na kwa taarifa yako, hao watu wa ukawa wanaojaza mafuriko wanapiga kura. Kama ulitegemea ni sawa na miaka mingine iliyopita watu wanashabikia upinzani na hawajajiandikisha, you must go and get your head examined. Tatizo unatumia muda mwingi upo nyuma ya keyboard ya computer, hujui hata hali halisi ya mtaani. Huna tofauti na mkapa aliesema wanaotaka mabadiliko ni wapumbavu na malofa. Kikundi cha watu wachache wanadhani wanajua sana watanzania wanataka nini.. Na wanataka kutuamulia pia. Don't insult our intelligence