Magufuli apongezwa kukusanya trilioni 1.4/-

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imempongeza Rais John Magufuli kwa kushirikiana na jumuiya hiyo, hivyo kufanikisha serikali kukusanya kiasi cha Sh trilioni 1.4.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Johnson Minja wakati akizindua tawi la JWT Mkoa wa Pwani.
Alieleza uundwaji wa kamati ya wafanyabiashara, umesaidia kupatikana kwa kiasi hicho kwa muda mfupi.
Minja alisema kamati hiyo ilisaidia kuonesha jinsi baadhi ya watendaji wa serikali walikuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu, kuikosesha mapato serikali.
“Tunamshukuru Dakta Magufuli kwa kuonesha ushirikiano pamoja na sisi, kwani ameamini kuwa nchi inaweza kujiletea maendeleo kwa kushirikiana na wafanyabiashara ambao ni sekta binafsi na matokeo ya ushirikiano yamezaa matunda,” alisema Minja.
Alisema kipindi cha nyuma, fedha nyingi za kodi zilikuwa zikiingia kwenye mifuko ya watendaji wasiokuwa waaminifu, badala ya kwenda serikalini.
Alisema mapato yaliyokuwa yakienda serikalini, yalikuwa kidogo.
“Wafanyabiashara si kwamba hawataki kulipa kodi, tatizo ni kwamba kodi nyingi zilikuwa za usumbufu na pia watendaji wa mamlaka za ukusanyaji, walikuwa wakijipatia fedha kwa maslahi binafsi, lakini Dakta Magufuli ameliona hilo na amewashughulikia wale waliokwepa kodi na kuwashirikisha wafanyabiashara,” alisema Minja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Pwani, Abdalla Ndauka alisema lengo la kuanzishwa jumuiya hiyo ni kuwaunganisha wafanyabiashara na kuwa na sauti moja ili kukabili changamoto zinazowakabili.
Ndauka alisema moja ya changamoto zao ni kuwa na kodi nyingi huku nyingine zikiwa siyo sahihi na nyingine zimekuwa ni kero, lakini pia lengo ni kuongeza walipa kodi kwa usajili wa wafanyabiashara ili wawe rasmi.
 
hakuna kitu uongo mtupu Tbc hawana hata centi moja huu uongo una mwisho
 
Back
Top Bottom