Magufuli aonesha vipaumbele vyake

m2me

Member
Jul 23, 2012
55
95
Baada ya kutangazwa kuwa mgombea uraisi kupitia CCM, Magufuli alishindwa kuonesha vipaumbele vyake na baadae kukazania kuwa anasubiri ilani ya chama na hata alipolazimika kutoa neno alijikita katika nyota iliyofifia ya JK kuwa "nitaendeleza ya JK" REJEA HII MAKALA

Jiulize, embe lililokua likiuzwa shilingi 50 pale sokoni Buguruni, leo linauzwa baina ya shilingi 500 hadi 1,000. Mara 20 zaidi. Kwa mtindo huu, ukitaka kujua bei ya embe miaka 10 ijayo chukua bei ya sasa (shilingi 1,000) halafu zidisha mara 20, utapata shilingi 20,000. Kwa hivyo, tukipata rais kama Rais Kikwete (Magufuli anajinasibu kuendeleza ya JK) , miaka 10 ijayo tutanunua embe moja kwa shilingi 20,000. Wallahi, itabidi tuwe na noti ya shilingi 100,000.

Kama embe limepanda bei mara 20 tangu mwaka 2005 hadi 2015, tutegemee lipande tena mara 20 kuanzia 2015 hadi 2025, ikimaanisha mwaka 2025 bei ya embe itakuwa 20,000. Ukitaka kununua embe kumi utakuwa unaenda na shilingi 200,000. Bila shaka wafanyabiashara wakubwa watalipa mabilioni kadhaa kwa fuso moja. Yaani unaenda kwa mkulima na fuso lako limejaa noti na mkulima anapakua noti akimaliza anapakia maembe.

Pia, Magufuli alishindwa kuelewa kuwa watanzania hawana tena muda wa kusoma ilani za vyama kwa sababu ukichukua ilani za uchaguzi za CCM zote zina mambo mazuri ila yamewekwa kapuni.

Kwa hatua hii ya kuanza kutoa ahadi ya Tsh.50, 000,000 kila kijiji, Laptop kwa kila mwalimu, wanafunzi na walemavu badala ya ‘kupiga mbizi' kusafiri bure kwenye vivuko n.k. ni jambo linaloonesha kuwa wewe ni mtu sikivu na uanyezingatia ushauri.

Na kwa kuwa unasikia na kuzingatia ushauri, naomba kukumbusha kuwa mtangulizi wako alitoa ahadi nyingi kama hizo ikiwemo meli ya kisasa Ziwa Victoria, kulikuwa na mamilioni ya jk ambayo hatukujua yalikuwa wanagawiwa vipi, hakuna mtoto wa maskini atakayekosa elimu juu kwa kigezo cha ada na mengine mengi.

Mbali na kutueleza hizo milioni 50 kwa kila kijiji zitatoka wapi na zitakuwa za kazi gani na walengwa watakuwa akina nani? Nashaauri kuwa jaribu kutafuiti kidogo kujua kama tatizo tulilonalo watanzania ni kupewa pesa mfukoni au kurahisishiwa mazingira ya kujitafutia wenyewe? Tatizo walilonalo walimu ni laptop au maslahi na mazingira bora ya kazi? Kama tatizo la walimu ni laptop, vipi sekta nyingine kama Polisi, wauguzi, madaktari, wamachinga, mama ntilie, waendesha bodaboda, mabasi na malori?

Naahidi kukupa kura yangu endapo utanithibitishia kuwa utakapokuwa rais mabenki yote yatatoa mikopo kwa mashariti nafuu kwa makundi yote ya kijamii pasipokuwa na ubaguzi wa kimatabaka, dhamana itakuwa uraia wako na siyo nyumba, shamba au kiwanja na pia riba haitazidi 10% kwa benk zote.

Kodi kandamizi zote zitaondolewa katika biashara isiyozidi mtaji wa milioni 10 na hakutokuwa tena na michango ya madawati, walinzi na uandikishwaji mashuleni ili elimu ionekane ni bure kweli kwa watoto wa maskini tofauti ba ilivyo hivi sasa ambapo tunaambiwa ada ya sekondari ni Tsh.10,000 lakini michango inafika 200,000.

Makampuni makubwa kama VODA, TIGO, AIRTEL, ZANTEL, Migodi n.k kadharika yatasajiliwa katika soko la hisa la Dar es Salaam na mapato yao yote yatawekwa wazi kwa manufaa ya kila mtanzania, matajiri hawataodhi ardhi kwa kununua viwanja vyote vinavyopimwa na halimashauri nchini n.k

Chanzo: Zanzibardaima
 

Awsom

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,085
0
Yaani Magufuli anachojua tu ni kusema sitawaangusha,na kumsifia mwanaume mwenzie...aibu hii kwakweli.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,383
2,000
Hivi kampeni zimeanza?? Maana jana nimeona ITV wakirusha kipindi cha kumuelezea Magufuli historia yake hadi kuteuliwa kwake kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Hii ni sawa au ni mfumo ule wa kibabe wa CCM?
Mimi nadhani Tume ya Uchaguzi inatakiwa kuwa makini na hizi double standards.
 

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
14,970
2,000
m2me
Kwa mfano huo wa embe nimekudharau, maana hujui kuwa tunda hlio ni la msimu.
Sikuendelea kusoma the rest, its too shallow!!
 
Last edited by a moderator:

chaikavu

JF-Expert Member
Apr 18, 2015
760
0
m2me
kama kuna mwalimu humu atuambie katika madai yao walishawahi kuorodhesha LAPTOPS kama madai yao juu ya serikali?

Hivi magufuli ana matatizo gani? ni walimu wa aina gani ambao anataka kuwapa laptops? je ni wale walimu wanaoishi vijiji visivyo na umeme wala sola energy au ni walimu wapi hao?

Hii nchi haitaendelea kama tutaendelea kuwa ccm wale wale wanao waza kama nyumbu. bora wangekuwa wanawaza kama swala
 
Last edited by a moderator:

ngudengude

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
1,178
1,500
haina shida maana ni mambo yaliyotokea na tulishayaona na kuyasikia jinsi mchakato ulivoenda, sio kampeni, ndio maana hata ukawa wakanunua vijana kutoka mikoani wawasindikizee kurudisha fomu ya mgombea fisadi EL

Hivi kampeni zimeanza?? Maana jana nimeona ITV wakirusha kipindi cha kumuelezea Magufuli historia yake hadi kuteuliwa kwake kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Hii ni sawa au ni mfumo ule wa kibabe wa CCM?
Mimi nadhani Tume ya Uchaguzi inatakiwa kuwa makini na hizi double standards.
 

awp

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,712
1,195
KOMBAJR umenichekesha sana siku ya leo na hivyo vipaumbe. nilinuna nimejikuta ninafuraha ghafla
 
Last edited by a moderator:

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
0
Hivi kampeni zimeanza?? Maana jana nimeona ITV wakirusha kipindi cha kumuelezea Magufuli historia yake hadi kuteuliwa kwake kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Hii ni sawa au ni mfumo ule wa kibabe wa CCM?
Mimi nadhani Tume ya Uchaguzi inatakiwa kuwa makini na hizi double standards.

Tume ipi? Sasa wenyewe wanakaribia 'kujikojolea' maana kilichoonekana wiki hii wakati EL aliyoibadili DAR, kiliwapa mshtuko wa asili na hawana la kuifanyia CCM ichomoke shimoni zaidi ya kuiachia tu ifanye itakalo kujiokoa!

Tume inajua Kampeni bado, ila Makufuli kutoa Ahadi za Milioni 50, kila kijiji, Laptop nk...sio kujitambulisha bali ni kuanza Kampeni, inaonekana? na hiyo ahadi ni bajeti ipi? na Sera ipi? ahadi walizotoa awali waanze nazo endapo ndoto za mchana zitawafanya washinde! ...tutawasahau soon!
 

Mc Tilly Chizenga

JF-Expert Member
Feb 7, 2012
4,530
2,000
Naahidi kukupa kura yangu endapo utanithibitishia kuwa utakapokuwa rais mabenki yote yatatoa mikopo kwa mashariti nafuu kwa makundi yote ya kijamii pasipokuwa na ubaguzi wa kimatabaka, dhamana itakuwa uraia wako na siyo nyumba, shamba au kiwanja na pia riba haitazidi 10% kwa benk zote.
........................................................................
watanzania tunapenda kudanganywa,hivi haya maneno hapo juu hata akiahidi kwa maneno unadhani yataweza kutekelezeka???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom