‘Magufuli anaua upinzani’

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
UTENDAJI wa Rais John Magufuli, umemkuna Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Tanzania, Dk. James Wanyancha, kiasi cha kumfananisha mkuu huyo wa nchi na sumu itakayoua nguvu ya vyama vya upinzani nchini.

Dk. Wanyancha aliyepata kuwa Mbunge wa Serengeti mkoani Mara na Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, anatabiri kwamba kifo cha nguvu ya upinzani kitatoa fursa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushika madaraka ya nchi hata kwa miaka 200 ijayo.

Anasema kwamba aina ya utendaji inayoonyeshwa na Rais Magufuli katika kukabili wezi na wabadhirifu wa mali ya umma na kutetea maslahi ya wanyonge, itaangamiza nguvu ya wapinzani kwa kuwakosesha cha kukichongea CCM kwa wananchi.

“Lakini kikubwa zaidi, Watanzania tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kumpata Rais huyu, atalipeleka Taifa letu kwenye mafanikio makubwa, watu watakuja kushangaa,” anasema Dk. Wanyancha katika mahojiano maalum na Raia Mwema wiki hii akitoa maoni yake kuhusu utendaji wa Rais Magufuli.

Anajivunia umakini wa chama chake cha CCM uliompatia Dk. Magufuli baraka ya kugombea urais mwaka jana, akisema kitendo hicho kimeudhihirishia umma wa Watanzania kwamba chama hicho kikongwe hakijafilisika watu waadilifu, waaminifu na wachapakazi mahiri.

“CCM ni chama kikubwa, si kweli kwamba wanachama wake wote ni mafisadi, bado kina watu wengi waaminifu na waadilifu, inategemea umemchagua nani… tungechagua fisadi mambo yangekuwa mabaya, lakini tunajivunia chaguo letu la Dk. Magufuli, ni kiongozi safi na tumaini la maendeleo ya kweli ya nchi yetu,” anasisitiza Dk. Wanyancha aliyepata pia kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika.

Kuhusu mtazamo wa watu wachache wanaodhani kasi ya utendaji aliyoanza nayo Rais huyo wa Awamu ya Tano itaishia kuwa nguvu ya soda, Dk. Wanyancha ambaye pia ni Mshauri wa Kujitegemea wa Uhifadhi wa Mazingira, anasema:

“Hao wanajidanganya, huyu Dk. Magufuli mimi ninamfahamu vizuri, alikuwa bosi wangu kwenye Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, yeye yuko hivyo siku zote, ni mchapakazi hodari na ni mtu wa kujituma na kujitolea.

“Ninaweza kusema kwamba Watanzania sasa tutarajie kuona nchi yetu inapata mafanikio makubwa zaidi kupitia uongozi wake, tutarajie kuona huduma nzuri za kijamii zinapatikana hapa nchini zikiwamo za afya, elimu, maji, barabara, umeme na mawasiliano.

“Ninasema hivyo kwa sababu Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha maisha ya Watanzania bila ubaguzi. Tukisimamia vizuri rasilimali zetu kama anavyoonyesha kiongozi wetu huyu, Tanzania itaweka historia ya kuwa miongoni mwa nchi tajiri sana duniani.
Nyangwine: Nchi iligeuzwa shamba la bibi

Naye mbunge wa zamani wa Tarime mkoani Mara, Nyambari Nyangwine, amesifu utendaji wa Rais Magufuli, huku akiibuka na hoja kwamba kabla ya kiongozi huyo kuingia Ikulu, nchi ilikuwa imekosa ulinzi thabiti mithili ya shamba la bibi.

“Ninaridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli, kwa kweli ameonyesha utendaji uliotukuka, ameimarisha uongozi wa nchi yetu iliyokuwa imegeuzwa kuwa kama shamba la bibi lisilo na mlinzi,” ameeleza Nyangwine.

Kada huyo wa CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni za Nyambari Nyangwine zinazochapisha na kusambaza vitabu vya kiada na ziada katika shule za sekondari, anamtazama Rais Magufuli kama tumaini halisi la kuifikisha Tanzania kwenye neema ya uchumi imara na maendeleo ya kutolea mfano mzuri.

“Tulikuwa tunataka kiongozi kama huyu hapa Tanzania, kiongozi mwenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu haraka, maana huko nyuma nchi yetu iliyumba kutokana na ukosefu wa maamuzi magumu yenye maslahi kwa umma na Taifa letu.”

“Kwa kweli kinachonifurahisha zaidi kwa Rais Magufuli ni ujasiri wake wa kufanya maamuzi magumu papo kwa hapo badala ya kusema ‘ngoja tuunde tume tuchunguze’, huyu ndiye Rais tuliyekuwa tunamhitaji kwa ajili ya kuimarisha uwajibikaji serikalini na maendeleo ya kweli nchini.

“Matumaini yangu ni kwamba mkuu huyu wa nchi ataendelea kuonyesha uongozi uliotukuka ikiwa ni pamoja na kuwezesha wananchi kiuchumi, tukiwa na uchumi imara, nchi yetu itapiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali,” anasema Nyangwine.

Pamoja na hatua nyingine zenye mwelekeo wa kudhibiti wizi na ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka serikalini, kwa nia ya kuwezesha unafuu wa maisha kwa wananchi wa hali ya chini, Rais Magufuli ameshawavua madaraka na kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa katika kipindi kifupi kinachokaribia miezi minne sasa.

Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu kwamba kiongozi huyo angebanwa na chama chake, CCM, kiasi cha kukosa uthubutu wa kuwashughulikia vigogo wasiyo waadilifu serikalini, utendaji wake umewashangaza wengi, hasa kutokana na msimamo wake kuchukia ufisadi na rushwa, huku akiegemea zaidi kwa wananchi wa tabaka la chini.

Msukumo wa Rais Magufuli umeweka rekodi ya kuongeza ukusanyaji wa mapato mara dufu na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima serikalini. Amefanikisha mambo mengi ya kitaifa kwa muda huo mfupi kwa kutumia kauli mbiu ya ‘kutumbua majibu’ katika idara na taasisi za umma.

Itakumbukwa kwamba siku chache baada ya kuapishwa kushika madaraka ya nchi Novemba 6, mwaka jana, Rais Magufuli alifanya ziara zikiwamo za kushitukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), miongoni mwa idara nyingine, ambapo alichukua hatua za kinidhamu na kutoa maelekezo machungu yaliyowagusa baadhi ya watumishi wakiwamo wakiwamo makada wa CCM.

Lakini pia katika hali ambayo ilidhaniwa na baadhi ya wananchi kwamba haitawezekana, kiongozi huyo wa nchi amefungua ukurasa mpya kwa kufanikisha utekelezaji wa ahadi ya chama chake ya utoaji wa elimu ya msingi hadi kidato cha nne bure kuanzia Januari mwaka huu.

Raia Mwema
 
Kumbe aliyesema hayo ni mwanaCCM mwenzenu (Wanyancha). Me nilijua ameongea mtu toka upinzani au raia wa nchi za kigeni. Sasa kwa huyo Wanyancha ulitarajia amponde Magufuli kweli!? Unachotakiwa kujua ni kwamba katika kipindi cha kuelekea muongo wa tatu wa karne ya 21, CCM imechokwa katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo Dar ambapo wananchi wamedhamiria kuifuta kabisa ifikapo 2020. Hivi wewe Singidadodoma hujiulizi kwamba kila ufanyikapo uchaguzi mkuu, CCM ndiyo hupoteza majimbo huku Upinzani ukiongeza idadi? Umewahi kujiuliza swali hilo? Jiulize 2010 Chadema walikuwa na wabunge wangapi na leo hii wana wabunge wangapi, hali kadhalika kwa CUF. Jiulize, mkoa wa Mtwara, Lindi, Morogoro na Kilimanjaro walikuwa na majimbo mangapi yaliyoongozwa na upinzani, je kwenye mikoa hiyo hali ikoje kwa sasa? Kwa hakika CCM si chama endelevu tena.
 
  • Thanks
Reactions: cmp
AGENDA ZA UPINZANI MPAKA SASA ZAIDI MIEZI 4
1.MFUMO
2.BABU SEYA
3.BANK YA MAMA NTILIE
4.BANK YA BODABODA
5.KIINGEREZA
6.ZANZIBAR.........................
 
Usikute nae ana-kijipu anakificha kwa kumpamba Magu. Hakuna mwana-CCM aliyekuwa ndani ya serikali asiwe na Kijipu.
 
AGENDA ZA UPINZANI MPAKA SASA ZAIDI MIEZI 4
1.MFUMO
2.BABU SEYA
3.BANK YA MAMA NTILIE
4.BANK YA BODABODA
5.KIINGEREZA
6.ZANZIBAR.........................
Wewe bado ni mdogo kudadavua!
ImageUploadedByJamiiForums1457000504.454415.jpg
 
UTENDAJI wa Rais John Magufuli, umemkuna Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Tanzania, Dk. James Wanyancha, kiasi cha kumfananisha mkuu huyo wa nchi na sumu itakayoua nguvu ya vyama vya upinzani nchini.

Dk. Wanyancha aliyepata kuwa Mbunge wa Serengeti mkoani Mara na Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, anatabiri kwamba kifo cha nguvu ya upinzani kitatoa fursa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushika madaraka ya nchi hata kwa miaka 200 ijayo.

Anasema kwamba aina ya utendaji inayoonyeshwa na Rais Magufuli katika kukabili wezi na wabadhirifu wa mali ya umma na kutetea maslahi ya wanyonge, itaangamiza nguvu ya wapinzani kwa kuwakosesha cha kukichongea CCM kwa wananchi.

“Lakini kikubwa zaidi, Watanzania tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kumpata Rais huyu, atalipeleka Taifa letu kwenye mafanikio makubwa, watu watakuja kushangaa,” anasema Dk. Wanyancha katika mahojiano maalum na Raia Mwema wiki hii akitoa maoni yake kuhusu utendaji wa Rais Magufuli.

Anajivunia umakini wa chama chake
cha CCM uliompatia Dk. Magufuli baraka ya kugombea urais mwaka jana, akisema kitendo hicho kimeudhihirishia umma wa Watanzania kwamba chama hicho kikongwe hakijafilisika watu waadilifu, waaminifu na wachapakazi mahiri.

“CCM ni chama kikubwa, si kweli kwamba wanachama wake wote ni mafisadi, bado kina watu wengi waaminifu na waadilifu, inategemea umemchagua nani… tungechagua fisadi mambo yangekuwa mabaya, lakini tunajivunia chaguo letu la Dk. Magufuli, ni kiongozi safi na tumaini la maendeleo ya kweli ya nchi yetu,” anasisitiza Dk. Wanyancha aliyepata pia kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika.

Kuhusu mtazamo wa watu wachache wanaodhani kasi ya utendaji aliyoanza nayo Rais huyo wa Awamu ya Tano itaishia kuwa nguvu ya soda, Dk. Wanyancha ambaye pia ni Mshauri wa Kujitegemea wa Uhifadhi wa Mazingira, anasema:

“Hao wanajidanganya, huyu Dk. Magufuli mimi ninamfahamu vizuri, alikuwa bosi wangu kwenye Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, yeye yuko hivyo siku zote, ni mchapakazi hodari na ni mtu wa kujituma na kujitolea.

“Ninaweza kusema kwamba Watanzania sasa tutarajie kuona nchi yetu inapata mafanikio makubwa zaidi kupitia uongozi wake, tutarajie kuona huduma nzuri za kijamii zinapatikana hapa nchini zikiwamo za afya, elimu, maji, barabara, umeme na mawasiliano.

“Ninasema hivyo kwa sababu Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha maisha ya Watanzania bila ubaguzi. Tukisimamia vizuri rasilimali zetu kama anavyoonyesha kiongozi wetu huyu, Tanzania itaweka historia ya kuwa miongoni mwa nchi tajiri sana duniani.
Nyangwine: Nchi iligeuzwa shamba la bibi

Naye mbunge wa zamani wa Tarime mkoani Mara, Nyambari Nyangwine, amesifu utendaji wa Rais Magufuli, huku akiibuka na hoja kwamba kabla ya kiongozi huyo kuingia Ikulu, nchi ilikuwa imekosa ulinzi thabiti mithili ya shamba la bibi.

“Ninaridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli, kwa kweli ameonyesha utendaji uliotukuka, ameimarisha uongozi wa nchi yetu iliyokuwa imegeuzwa kuwa kama shamba la bibi lisilo na mlinzi,” ameeleza Nyangwine.

Kada huyo wa CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni za Nyambari Nyangwine zinazochapisha na kusambaza vitabu vya kiada na ziada katika shule za sekondari, anamtazama Rais Magufuli kama tumaini halisi la kuifikisha Tanzania kwenye neema ya uchumi imara na maendeleo ya kutolea mfano mzuri.

“Tulikuwa tunataka kiongozi kama huyu hapa Tanzania, kiongozi mwenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu haraka, maana huko nyuma nchi yetu iliyumba kutokana na ukosefu wa maamuzi magumu yenye maslahi kwa umma na Taifa letu.”

“Kwa kweli kinachonifurahisha zaidi kwa Rais Magufuli ni ujasiri wake wa kufanya maamuzi magumu papo kwa hapo badala ya kusema ‘ngoja tuunde tume tuchunguze’, huyu ndiye Rais tuliyekuwa tunamhitaji kwa ajili ya kuimarisha uwajibikaji serikalini na maendeleo ya kweli nchini.

“Matumaini yangu ni kwamba mkuu huyu wa nchi ataendelea kuonyesha uongozi uliotukuka ikiwa ni pamoja na kuwezesha wananchi kiuchumi, tukiwa na uchumi imara, nchi yetu itapiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali,” anasema Nyangwine.

Pamoja na hatua nyingine zenye mwelekeo wa kudhibiti wizi na ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka serikalini, kwa nia ya kuwezesha unafuu wa maisha kwa wananchi wa hali ya chini, Rais Magufuli ameshawavua madaraka na kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa katika kipindi kifupi kinachokaribia miezi minne sasa.

Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu kwamba kiongozi huyo angebanwa na chama chake, CCM, kiasi cha kukosa uthubutu wa kuwashughulikia vigogo wasiyo waadilifu serikalini, utendaji wake umewashangaza wengi, hasa kutokana na msimamo wake kuchukia ufisadi na rushwa, huku akiegemea zaidi kwa wananchi wa tabaka la chini.

Msukumo wa Rais Magufuli umeweka rekodi ya kuongeza ukusanyaji wa mapato mara dufu na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima serikalini. Amefanikisha mambo mengi ya kitaifa kwa muda huo mfupi kwa kutumia kauli mbiu ya ‘kutumbua majibu’ katika idara na taasisi za umma.

Itakumbukwa kwamba siku chache baada ya kuapishwa kushika madaraka ya nchi Novemba 6, mwaka jana, Rais Magufuli alifanya ziara zikiwamo za kushitukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), miongoni mwa idara nyingine, ambapo alichukua hatua za kinidhamu na kutoa maelekezo machungu yaliyowagusa baadhi ya watumishi wakiwamo wakiwamo makada wa CCM.

Lakini pia katika hali ambayo ilidhaniwa na baadhi ya wananchi kwamba haitawezekana, kiongozi huyo wa nchi amefungua ukurasa mpya kwa kufanikisha utekelezaji wa ahadi ya chama chake ya utoaji wa elimu ya msingi hadi kidato cha nne bure kuanzia Januari mwaka huu.

Raia Mwema

Nyekundu ndo inapandisha upinzani baada ya kuuwa maana 2020 upinzani utasaidiwa na nguvu ya ndani ya kwenye chama iliyochagizwa na wanaotumbuliwa majipu, kwa muda mfupi JPM amazalisha upinzani wa ndani kuliko rais yoyote.

Sisi wapinzani 2010 tutakuwa tunasukuma mlevitu
 
Mnazungumzia nguvu ya serikali ya magufuli ya kufoji zuio la mahakama na vyombo vya usalama kukunja mkia kama mbwa koko au?
 
UTENDAJI wa Rais John Magufuli, umemkuna Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Tanzania, Dk. James Wanyancha, kiasi cha kumfananisha mkuu huyo wa nchi na sumu itakayoua nguvu ya vyama vya upinzani nchini.

Dk. Wanyancha aliyepata kuwa Mbunge wa Serengeti mkoani Mara na Naibu Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, anatabiri kwamba kifo cha nguvu ya upinzani kitatoa fursa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushika madaraka ya nchi hata kwa miaka 200 ijayo.

Anasema kwamba aina ya utendaji inayoonyeshwa na Rais Magufuli katika kukabili wezi na wabadhirifu wa mali ya umma na kutetea maslahi ya wanyonge, itaangamiza nguvu ya wapinzani kwa kuwakosesha cha kukichongea CCM kwa wananchi.

“Lakini kikubwa zaidi, Watanzania tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kumpata Rais huyu, atalipeleka Taifa letu kwenye mafanikio makubwa, watu watakuja kushangaa,” anasema Dk. Wanyancha katika mahojiano maalum na Raia Mwema wiki hii akitoa maoni yake kuhusu utendaji wa Rais Magufuli.

Anajivunia umakini wa chama chake cha CCM uliompatia Dk. Magufuli baraka ya kugombea urais mwaka jana, akisema kitendo hicho kimeudhihirishia umma wa Watanzania kwamba chama hicho kikongwe hakijafilisika watu waadilifu, waaminifu na wachapakazi mahiri.

“CCM ni chama kikubwa, si kweli kwamba wanachama wake wote ni mafisadi, bado kina watu wengi waaminifu na waadilifu, inategemea umemchagua nani… tungechagua fisadi mambo yangekuwa mabaya, lakini tunajivunia chaguo letu la Dk. Magufuli, ni kiongozi safi na tumaini la maendeleo ya kweli ya nchi yetu,” anasisitiza Dk. Wanyancha aliyepata pia kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika.

Kuhusu mtazamo wa watu wachache wanaodhani kasi ya utendaji aliyoanza nayo Rais huyo wa Awamu ya Tano itaishia kuwa nguvu ya soda, Dk. Wanyancha ambaye pia ni Mshauri wa Kujitegemea wa Uhifadhi wa Mazingira, anasema:

“Hao wanajidanganya, huyu Dk. Magufuli mimi ninamfahamu vizuri, alikuwa bosi wangu kwenye Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, yeye yuko hivyo siku zote, ni mchapakazi hodari na ni mtu wa kujituma na kujitolea.

“Ninaweza kusema kwamba Watanzania sasa tutarajie kuona nchi yetu inapata mafanikio makubwa zaidi kupitia uongozi wake, tutarajie kuona huduma nzuri za kijamii zinapatikana hapa nchini zikiwamo za afya, elimu, maji, barabara, umeme na mawasiliano.

“Ninasema hivyo kwa sababu Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya kweli ya kuboresha maisha ya Watanzania bila ubaguzi. Tukisimamia vizuri rasilimali zetu kama anavyoonyesha kiongozi wetu huyu, Tanzania itaweka historia ya kuwa miongoni mwa nchi tajiri sana duniani.
Nyangwine: Nchi iligeuzwa shamba la bibi

Naye mbunge wa zamani wa Tarime mkoani Mara, Nyambari Nyangwine, amesifu utendaji wa Rais Magufuli, huku akiibuka na hoja kwamba kabla ya kiongozi huyo kuingia Ikulu, nchi ilikuwa imekosa ulinzi thabiti mithili ya shamba la bibi.

“Ninaridhishwa na utendaji wa Rais John Magufuli, kwa kweli ameonyesha utendaji uliotukuka, ameimarisha uongozi wa nchi yetu iliyokuwa imegeuzwa kuwa kama shamba la bibi lisilo na mlinzi,” ameeleza Nyangwine.

Kada huyo wa CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni za Nyambari Nyangwine zinazochapisha na kusambaza vitabu vya kiada na ziada katika shule za sekondari, anamtazama Rais Magufuli kama tumaini halisi la kuifikisha Tanzania kwenye neema ya uchumi imara na maendeleo ya kutolea mfano mzuri.

“Tulikuwa tunataka kiongozi kama huyu hapa Tanzania, kiongozi mwenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu haraka, maana huko nyuma nchi yetu iliyumba kutokana na ukosefu wa maamuzi magumu yenye maslahi kwa umma na Taifa letu.”

“Kwa kweli kinachonifurahisha zaidi kwa Rais Magufuli ni ujasiri wake wa kufanya maamuzi magumu papo kwa hapo badala ya kusema ‘ngoja tuunde tume tuchunguze’, huyu ndiye Rais tuliyekuwa tunamhitaji kwa ajili ya kuimarisha uwajibikaji serikalini na maendeleo ya kweli nchini.

“Matumaini yangu ni kwamba mkuu huyu wa nchi ataendelea kuonyesha uongozi uliotukuka ikiwa ni pamoja na kuwezesha wananchi kiuchumi, tukiwa na uchumi imara, nchi yetu itapiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali,” anasema Nyangwine.

Pamoja na hatua nyingine zenye mwelekeo wa kudhibiti wizi na ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka serikalini, kwa nia ya kuwezesha unafuu wa maisha kwa wananchi wa hali ya chini, Rais Magufuli ameshawavua madaraka na kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa katika kipindi kifupi kinachokaribia miezi minne sasa.

Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu kwamba kiongozi huyo angebanwa na chama chake, CCM, kiasi cha kukosa uthubutu wa kuwashughulikia vigogo wasiyo waadilifu serikalini, utendaji wake umewashangaza wengi, hasa kutokana na msimamo wake kuchukia ufisadi na rushwa, huku akiegemea zaidi kwa wananchi wa tabaka la chini.

Msukumo wa Rais Magufuli umeweka rekodi ya kuongeza ukusanyaji wa mapato mara dufu na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima serikalini. Amefanikisha mambo mengi ya kitaifa kwa muda huo mfupi kwa kutumia kauli mbiu ya ‘kutumbua majibu’ katika idara na taasisi za umma.

Itakumbukwa kwamba siku chache baada ya kuapishwa kushika madaraka ya nchi Novemba 6, mwaka jana, Rais Magufuli alifanya ziara zikiwamo za kushitukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), miongoni mwa idara nyingine, ambapo alichukua hatua za kinidhamu na kutoa maelekezo machungu yaliyowagusa baadhi ya watumishi wakiwamo wakiwamo makada wa CCM.

Lakini pia katika hali ambayo ilidhaniwa na baadhi ya wananchi kwamba haitawezekana, kiongozi huyo wa nchi amefungua ukurasa mpya kwa kufanikisha utekelezaji wa ahadi ya chama chake ya utoaji wa elimu ya msingi hadi kidato cha nne bure kuanzia Januari mwaka huu.

Raia Mwema
Wengi walitabiri kifo cha vyama vya upinzani kabla yako lakini ndio kwanza vimeongeza wabunge, hata Kikwete walimfananisha na Mtume, njia ya kumaliza upinzani ni kutenda haki na kuwa mkweli pale panapotokea mgogoro kati ya ccm na vyama vingine lakini kwa mtindo huu unaofanyika Zanzibar,umeya dar na kuzuia mikutano ya vyama pinzani na Makufuli kukaa kimya upinzani utazidi kuimarika
 
Back
Top Bottom