Magufuli anashindwa nini ku fix haya TRA?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,282
117,232
Niseme tu pamoja na mapungufu mbalimbali ya awamu ya tano
lakini lile la Magufuli 'kurekebisha haraka' uteuzi wa Maswi TRA lilinifurahisha sana

Angalau 'uthubutu' wa kurekebisha kwa haraka bila kuogopa 'wakosoaji'
tutasema nini....ulionekana....na kusaidia 'maslahi ya Taifa'

Sasa kuna haya mawili huko TRA nashindwa kuelewa why Magufuli
na serikali yake kwa ujumla hawayaoni kuwa yanahitaji
'marekebisho ya haraka saana'.....bila kuchelewa

La kwanza ni kosa la kutangazia wafanyabiashara mashine za EFD zitatolewa bure
huku bajeti yake kumbe ni kubwa saana na haikuwa tayari....

Leo Kaimu Kmishna wa TRA ni kama alikuwa 'anajikanyaga' kuhusu hiyo issue
na mwishowe anakuja kusema hizo mashine zitatolewa bure kwa wafanyabiashara
wa chini tu....ina maana sio bure tena kama ilivyo tangazwa

Ni vizuri Rais akaisaidia TRA kwa 'kubadili maamuzi'
mashine zile ziuzwe tu lakini itazamwe bei.....ikiwezekana
hizo mashine kuwe na supplier zaidi ya mmoja
waziuze direct tu kwa wafanyabiashara
au serikali iruhusu kampuni nyingi sana zishindane kuwauzia
wafanyabiashara........hii itasaidia TRA na serikali kiujumla

La pili ni kuendelea kuwa na 'kaimu kamishna' hapo TRA...
kwa nafasi yake hapo TRA kukaimu tu sio sawa
atashindwa kufanya maamuzi yoote yanayotakiwa kufanya
atashindwa kusema ukweli iwapo wanasiasa wataleta maamuzi ya kisiasa
ili tu 'asije kosa hiyo nafasi'

Ili Kamishna aweze kufanya maamuzi yanayotakiwa ikiwemo na kusema
ukweli kwa uhuru kipi sahihi na kipi sio sahihi ni vizuri ateuliwe haraka...

haya maamuzi yafanyike haraka....kuchelewa ni kuifanya TRA ilegelege....

Ila pia awe na teuzi sahihi si kukurupuka

Pia waache tabia ya kutuletea siasa kwenye kodi ,walitangaza mwezi November wamekusanya trillion 1.4 na kumpongeza kaimu kamishana Philip mpango na kumpandisha cheo kuwa waziri, ili hali alimteuwa tarehe 27 November, akafanya kazi kuanzia 30 November, sasa anayetakiwa kupongezwa ni yupo rished bade au Philip mpango?
Pia kama kumbukumbu zenu zipo sahii walisema walikusanya December 1.5 trillion ,January trillion 1 ,sasa Leo wanatuambia eti wamefikia lengo kwa asilimia 99? Mimi binafsi sielewi hizo takwimu kabisa .....

SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.

Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.

Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.

Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.

Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari. Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli. Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya ishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.

Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18.Chanzo: Habari Leo

Ama kweli binaadamu tunatofautiana ! mi sijayaona hayo mapungufu MENGI ya awamu ya 5 bado..

La kwanza ni kosa la kutangazia wafanyabiashara mashine za EFD zitatolewa bure
huku bajeti yake kumbe ni kubwa saana na haikuwa tayari....

Leo Kaimu Kmishna wa TRA ni kama alikuwa 'anajikanyaga' kuhusu hiyo issue
na mwishowe anakuja kusema hizo mashine zitatolewa bure kwa wafanyabiasha ....
Huyo jamaa amejikanyaga sana.
Uko sahihi

Sasa haya maelezo kuwa zitolewe bure yakoje?
na why leo inasemwa zitatolewa kwa wafanyabiashara wa chini tu peke yake?

Hata mwanzo ilikuwa bure
Sema shida ununue kisha urudishiwe kwenye return zako

Na ndio njia iliyofanya wengi wajifiche huko kwamba hawana pesa ya kununulia

Hata mwanzo ilikuwa bure
Sema shida ununue kisha urudishiwe kwenye return zako

Na ndio njia iliyofanya wengi wajifiche huko kwamba hawana pesa ya kununulia

Awaache TRA wafanye wanachoona sahihi
hili wanalifanya sababu tu ni amri ya Rais
ukweli ni kwamba linawakwaza
ungemuona kaimu kamishna leo anavyo liongelea ....ungeona hili ni siasa

Sasa haya maelezo kuwa zitolewe bure yakoje?
na why leo inasemwa zitatolewa kwa wafanyabiashara wa chini tu peke yake?
Halafu serikali hii haikuelewa kilio kikuu cha wafanya biashara juu ya hizo MASHINE ilikua ni nini....

Wengi hawakulilia ziwe bure but specifications na masharti ya TRA kwa hizo devices ndo ilikuwa kasheshe....

Wangeruhusu ushindani wa biashara ktk hizo kungeleta mwanya wa kuingizwa bora zaidi kuliko hizo wanazowalazimisha wanunue kufidia hasara ya Mpiga dili.....

Hizo mashine hazina faida kwa serikali wala wafanyabiashara kwanza zinaharibika haraka kwa matumizi ya kila siku labda kungekuwa tu na Cash Register Mashine kama zinazotumika nchi zingine badala ya hizi

Back
Top Bottom