Magufuli amchana Mkulo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli amchana Mkulo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Dec 23, 2011.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Jana wakati Bw. pombe anasaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi Dar, alimuwashia moto Bw. Mkulo kuwa wizara yake inachelewesha malipo ya wakandarasi na kufanya miradi ichelewe kumalizika. alisema ""

  "Na hili nalisema hapa kutokana na mwakilishi wa Ofisi ya Waziri wa Fedha kuwa mahali hapa," alisema Magufuli na kumgeukia ofisa huyo wa Wizara ya Fedha na kumwambia:

  "Mwambie Waziri Mkulo awalipe fedha makandarasi wanaodai, salamu hizo mfikishie huko aliko, makandarasi wanaidai serikali," alisema.
  Bila kutaja kiasi ambacho serikali inadaiwa, Magufuli alimtaka Waziri Mkulo kulichukua jambo hilo kwa uzito wa kipekee na kuanza kulipa madeni ya makandarasi kuanzia sasa, ili Wizara ya Ujenzi iweze kuwabana vizuri pale wanaposhindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati.''

  source: TANZANIA DAIMA YA LEO


  Ina maana hawa jamaa hata kupigiana simu hawawezi mpaka wavuane magamba kwenye TV??? Kazi ni kwake baba riz.
   
 2. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ni bora jembe limesema ukweri,maana angeanza kupewa lawama juu ya barabara zisizokamilika,kumbe Mh wa fedha afanyi vile inavyotakiwa

  safiii sana jembe Dr wa ukweri,wewe kamua hata kama upande wa pili unakukatisha tamaa,ni vyema anavyosema wazi inatufanya kuelewa nani anamkwamisha Dr wa ukweri
   
 3. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Magufuli siyo Jembe bali hiyo ndiyo style yake ya kung`arisha jina lake ili wananchi wamuone yeye ndiyo mkweli na mchapakazi pekee. Hakuna ambacho huyu Pombe hakijui juu ya ukata unaoikabili hazina.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mawaziri wengi wa Kikwete wanajitahidi kuchafuana kwenye media, hasa wale wenye nia ya kugombea urais 2015. Na Pombe ni mmoja wa hao wanaojikakamua kusafisha njia kwa kuwavua wenzake nguo!
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  I doubt - Inawezekana Pombe anajitafutia umaarufu wa kisiasa!
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kinachosikitisha hapa sio nani kasema uwongo au ukweli shida ni kwamba tunayo serikali ya namna gani ambayo haina mfumo unaoeleweka wa mawasiliano?
  Sio kitu cha kushabikia hiki, naamini bado mnayakumbuka yaliyojiri bungeni kuhusu posho kila mtu anasema lake hii ni hatari sana kuweza kupata tafsiri sahihi ya kitu kiitwacho "uwajibikaji wa pamoja".
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hivi hayo malori ya quality group yatapita barabara ipi maana zilizopo zina foleni mbaya..
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Wengine watasema amefanya vizuri kwa kuwa muwazi na labda hili litasaidia kufanya mambo yaende kasi.

  Wengine watasema this is undiplomatic, haheshimu collective responsibility, na alikuwa na njia nyingi tu za kuongea na Mkullo moja kwa moja, anatengeneza tension inayoweza kuleta confrontation.
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,742
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Magufuli in action a typical populist.
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  watanzania bana
  hivi umeyasikia jana UGANDA?
  Raisi msevi anamweleza waziri wake mbele ya vyombo vya habari kuwa alitakiwa kuwajibika kwa kutojua baadhi ya pesa zilikokwenda,lakini wakati huohuo waziri anasema mbele ya vyombo vya habari kuwa tatizo ni Raisi ndio aliyetoa madaraka yote juu ya mfanyabiashara aliyesababisha upotevu wa pesa ,

  leo maguri kasema anaonekana anatafuta umaarufu wa kisiasa,sasa mlitaka afanyaje kama njia nyingine zimeshindikana?
   
 11. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Akili ya Magufuli inafanana na ya Lyatonga Mrema.
   
 12. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndo askari wetu huyo.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,144
  Trophy Points: 280
  ..sidhani kama Mawaziri wanapaswa kuwasiliana namna alivyofanya Magufuli.

  ..this is a veteran minister, kwanini afanye hivyo?

  ..mnakumbuka ile sakata ya maboti yaliyotakiwa kwenda lake victoria alivyokuwa anamshambulia Prof.Mwandosya?
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  we dada utahangaika sana na mimi juu ya hizi ri za kipogoro,ndio zimenifikisha huku nakula kodi za wazungu wezi wa mali ghafi zetu,
  utahangaika sana kurekebisha,lakini kiukweri ndizo zinazo nipa maisha majuu
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Duh,

  Ushawabatiza majina "Msevi" na "Maguri".

  Serikali inayoendeshwa kwa rais kufokeana na waziri in the open kama watoto haina discipline wala collective responsibility. Kimsingi serikali yote inatakiwa kufanya kazi kama kitu kimoja, serikali ya CCM. Sasa tukiona Waziri mmoja anamtupia lawama mwingine sisi hatujui cha Magufuri wala Mkullo, tunachoona ni kwamba serikali ya CCM inashindwa kazi.

  Magufuri kwa upande mmoja yuko sawa, kwa sababu sijui kachukua hatua gani mwanzo huko, huenda kashindwa kote kaona amshitaki kwenye court of public opinion.

  Lakini typically haya ni mambo ya Magufuri, Mkullo na Kikwete kuongea kwenye cabinet meetings.

  Sijui hata kama hizo cabinet meetings zinakalika.
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  tantalila tu hizo
  kwani hawakutani kwenye vikao?
  kwa nini asimuulize akiwa huko?
   
 17. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ....ufalme ukifitinika...
   
 18. k

  kalokolaVIII JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  what do you mean by "populist"??? this terminology is highly abused in the west and now I see even in Tanzania. Have you ever known any, I underline ANY,politician who is not POPULIST??? Let's forget about demagogy and cheap rhetoric thence call a spade a.......SPADE!!!
  all politicians are populist(S)...period!!!!!
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Ron Paul is not a populist, he adopts some very controversial positions that defies the American political orthodoxy in a way that threatens his chances.

  Huwezi kusema mwanasiasa anayeadvocate general legalization ya marijuana na prostitution, abolishing the Federal Reserve na kusimamisha vita zote abruptly ni "populist". Hizi si popular positions.
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Dec 23, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,144
  Trophy Points: 280
  Kiranga,

  ..inawezekana wanakwenda kwenye cabinet meetings lakini hakuna cha maana wanachojadili.

  ..kama unavyomjua mwenyekiti wao, akianza kujenga hoja anazunguka weee mwisho hata hoja yenyewe hajengi.

  ..lakini pia tunamjua Magufuli na tabia zake za kuropoka-ropoka.
   
Loading...