Rafiki yangu ambaye ni mkuu wa wilaya aliwahi kuniambia wakuu wa wilaya wanapositaafu au kutoteuliwa tena au wakiambiwa msemo maarufu wa mzee watapangiwa kazi nyingine hulipwa kiinua mgongo cha Tsh milioni 80. Hii hajalishi unapandishwa kuwa mkuu wa mkoa au unahamishiwa wilaya nyingine. Ili mradi miaka mitano imeisha inahesabika umesitaafu.
Leo nchi yetu ina wilaya 171, kwa utaratibu huo wakuu wa wilaya 171 wanatakiwa kulipwa au wameshalipwa kiinua mgongo cha mil 80 kila mmoja! Hapo hujaesabu magari ya kifahari 171 ambayo hakuna linalopungua sh mil 300! na mshahara wa mil 3.8 kwa kila mkuu wa wilaya. Huu ni ubadhilifu!
Ningemuelewa rais wetu kama angewaacha hawa waliopo waendelee wakati anatafakari kukubaliana na rasmu ya Warioba ya kuundoa mfumo huu. Ikiwa rais atafanya uteuzi wa wakuu wa wilaya kitu ambacho najua atafanya, basi aache kutwambia ana adhima ya kubana matumizi.