Magufuli ajenge CCM upya

Daniel Limbu

Member
Jun 12, 2016
8
2
MAGUFULI AJENGE CCM MPYA.

Tarehe 23.7.2016 Chama cha Mapinduzi CCM kitaingia katika zama mpya ya kuongozwa na M/kiti mpya Mh John P.Magufuli. Naita ni zama mpya kwani ni mategemeo yangu na wanachama wenzangu wa Chama hiki bora Afrika kuwa mfumo mpya wa Chama chetu ni lazima uanzishwe au urejeshwe kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

Chini ya uongozi mpya wa Rais JPM kama M/kiti wetu natarajia CCM kujinoa na kuandaa wanachama wake kuwa makada halisi wa Chama si mashabiki tu wa vyama.

Kada wa chama ni tofuti na shabiki wa chama kwani Kada halisi wa Chama kwa namna yeyote ile ni lazima awe anajua nini anachokipigania katika chama chake .

Kada husimamia misingi ya chama chake tofauti na shabiki ambaye hushabikia mtu hata kama hana sifa za kuwa kiongozi ndani ya Chama au kupitia chama ili kushika hatamu ya kushika dola.

Tukumbushane dhidi ya hoja hii ilivyojitokeza 2015 katika mchakato wa kumpata mgombea wa Urais kupitia CCM wajumbe takribani wote waliokuwepo Dodoma walibeba agenda za Ushabiki wa watu wala si misingi ya Chama.Ushahidi ulionekana dhahiri Mara baada ya wagombea watano kubaki ndani ya tano bora huku kinara wa machafuko dhidi ya ushabiki wa watu Edward Lowasa akiongoza vurugu dhidi ya Kanuni za chama chetu kupitia kundi lililokuwa limejiandaa kumpitisha kwa namna yeyote bila kujali misingi ya uadilifu na uwajibikaji wa chama chetu.Nashukuru wajumbe wengi walisimamia misingi na hawakuogopa vitisho vya wapambe.

M/kiti mpya ajaye yaani Mh Dkt John P.Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analo jukumu kubwa la kukirejesha chama chetu katika misingi na dhamira ya kuanzishwa kwake.Magufuli lazima ajenge chama chenye watu wanaojua mambo yafuatayo.

1. Itikadi ya chama.
2. Falsafa ya chama.
3. Misingi ya Chama.
4. Kanuni za Chama.
5. Miongozo ya Chama
6. Katiba ya Chama.
7. Maelekezo mbalimbali ya chama.
8. Imani ya Chama.Bila kuwa na wanachama wanaojua vitu hivi vizuri

Tutaendelea kuwa na wanachama walio na kadi tu pia wakiwa ni wanachama wa misimu ya uchaguzi huku wakikiacha chama kikidorora na kupoteza uhai wake mbele ya upinzani.

Sasa ni wakati wa kukijenga chama upya hivyo viongozi wa chama pamoja na wanachama walio na upeo na masuala ya kisiasa waelimishwe ili kuchukua hatamu za kufungua madarasa ya itikadi katika maeneo yao nyakati za jioni baada ya kazi.Tusiogope gharama kwani Uhai wa Chama chetu ni muhimu sana kuliko fedha ambazo tutazitumia kukijenga chama.

Dkt Magufuli haya yanakukabili ukiupata Uenyekiti nikutakie utekelezaji mwema katika ujenzi mpya wa chama chetu.Kidumu Chama cha Mapinduzi.Mwl Daniel Malemi Limbu, Kada wa CCM.
 
Haelewi hata ataanzaje!! Atampa Mangula aendeshe Chama! Yeye abakie kukimbiz serikali!! Nje anaogopa kwenda! Na chama hatakiweza!! Miaka 10 mwendo ndio huooo!!!

Binadamu siku zote huwa ni wagumu kupokea mabadiliko, na hivyo mabadiliko yana gharama zake.
Mh. Mwenyekiti wetu mtarajiwa ajiandae kufanya mabadiliko huku akipuuzia vilio vya watakaokuwa wanatumbuliwa
 
Acheni uoga Na kuishi kwa mazoea Mabadiliko yanagharama zake.
 
Pia mh.Raisi asimamie kauli yake ya kuwataka wabunge waache ushabiki wa kiitikadi,kupigana vijembe bungeni na kuacha kupigania maslahi yao badala yake wawapiganie wanyonge walio wapeleka bungeni.
Wabunge kama yule anaetaka sanamu ya msanii wa muziki iwepo badala ya askari wetu wapigania uhuru hana tofauti na wapinga maendeleo,akina Ghasia,Kangi wasiotaka kukatwa kodi zao wanaenda kinyume na ilani ya chama wadhibitiwe
 
MAGUFULI AJENGE CCM MPYA.

Tarehe 23.7.2016 Chama cha Mapinduzi CCM kitaingia katika zama mpya ya kuongozwa na M/kiti mpya Mh John P.Magufuli. Naita ni zama mpya kwani ni mategemeo yangu na wanachama wenzangu wa Chama hiki bora Afrika kuwa mfumo mpya wa Chama chetu ni lazima uanzishwe au urejeshwe kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

Chini ya uongozi mpya wa Rais JPM kama M/kiti wetu natarajia CCM kujinoa na kuandaa wanachama wake kuwa makada halisi wa Chama si mashabiki tu wa vyama.

Kada wa chama ni tofuti na shabiki wa chama kwani Kada halisi wa Chama kwa namna yeyote ile ni lazima awe anajua nini anachokipigania katika chama chake .

Kada husimamia misingi ya chama chake tofauti na shabiki ambaye hushabikia mtu hata kama hana sifa za kuwa kiongozi ndani ya Chama au kupitia chama ili kushika hatamu ya kushika dola.

Tukumbushane dhidi ya hoja hii ilivyojitokeza 2015 katika mchakato wa kumpata mgombea wa Urais kupitia CCM wajumbe takribani wote waliokuwepo Dodoma walibeba agenda za Ushabiki wa watu wala si misingi ya Chama.Ushahidi ulionekana dhahiri Mara baada ya wagombea watano kubaki ndani ya tano bora huku kinara wa machafuko dhidi ya ushabiki wa watu Edward Lowasa akiongoza vurugu dhidi ya Kanuni za chama chetu kupitia kundi lililokuwa limejiandaa kumpitisha kwa namna yeyote bila kujali misingi ya uadilifu na uwajibikaji wa chama chetu.Nashukuru wajumbe wengi walisimamia misingi na hawakuogopa vitisho vya wapambe.

M/kiti mpya ajaye yaani Mh Dkt John P.Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analo jukumu kubwa la kukirejesha chama chetu katika misingi na dhamira ya kuanzishwa kwake.Magufuli lazima ajenge chama chenye watu wanaojua mambo yafuatayo.

1. Itikadi ya chama.
2. Falsafa ya chama.
3. Misingi ya Chama.
4. Kanuni za Chama.
5. Miongozo ya Chama
6. Katiba ya Chama.
7. Maelekezo mbalimbali ya chama.
8. Imani ya Chama.Bila kuwa na wanachama wanaojua vitu hivi vizuri

Tutaendelea kuwa na wanachama walio na kadi tu pia wakiwa ni wanachama wa misimu ya uchaguzi huku wakikiacha chama kikidorora na kupoteza uhai wake mbele ya upinzani.

Sasa ni wakati wa kukijenga chama upya hivyo viongozi wa chama pamoja na wanachama walio na upeo na masuala ya kisiasa waelimishwe ili kuchukua hatamu za kufungua madarasa ya itikadi katika maeneo yao nyakati za jioni baada ya kazi.Tusiogope gharama kwani Uhai wa Chama chetu ni muhimu sana kuliko fedha ambazo tutazitumia kukijenga chama.

Dkt Magufuli haya yanakukabili ukiupata Uenyekiti nikutakie utekelezaji mwema katika ujenzi mpya wa chama chetu.Kidumu Chama cha Mapinduzi.Mwl Daniel Malemi Limbu, Kada wa CCM.
Ujumbe murua kabisa uliotolewa kwa hekima ya hali ya juu
Namtakia kheri mtarajiwa mwenyekiti utendaji uliotukuka kama ambavyo anaendelea kulitumikia taifa kwa uadilifu wa hali ya juu na ni imani yangu kuwa atafanya hivyo kwa kuwatumikia watanzania wanachama wa Ccm
Nawatakia kikao chenye mafanikio hapo julai 23
Mungu ibariki Afrika Mungu bariki Tanzania
 
Back
Top Bottom