MAGUFULI AIKONGA SEKTA YA AFYA
Sekta ya afya ni muhimu na nyeti mno kwakua inagusa kila hatua ya maisha ya mwanadamu. Kwa mfano mtu hawezi kufanya vema kazi yake kama hana afya nzuri hata Mh. Rais hawezi kutekeleza majukumu yake vizuri kama hana afya imara.
Kwa kuliona hili Mh. Magufuli ameamua kuja na sera bora ya afya itakayomfanya kila Mtanzania kuwa na uhakika na afya yake hatimaye kumuwezesha kufanya kazi zake vema na kuinua uchumi wa nchi. Haina maana kwamba haya aliyoadhimia kuyafanya Mh. Magufuli hayakuonekana na viongozi waliotangulia, la hasha bali kila kiongozi hutatua tatizo sugu zaidi lililopo kwenye kipindi chake cha utawala.
Mh. Magufuli ameamua kufanya yafuatayo ili kuhakikisha afya za Watanzania zinaimarika:-
Kuandaa utaratibu utakaomuwezesha kila Mtanzania kupata bima ya afya kwajili ya kupata matibabu hata ule wakati ambao hana pesa kabisa
Kuongeza idadi ya waganga na wauguzi pamoja na kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyote vya tiba. Sasa wananchi wanakaribia kusahau suala la kuambiwa wakapate huduma fulani kwenye hospitali binafsi kisha warejee kwenye hospitali ya serikali kuendelea na tiba.
Sambamba na hilo Mh. Magufuli ameapa kupambana na watumishi wa sekta ya afya wanaohujumu upatikanaji wa dawa kwenye hospitali za serikali pamoja na vituo vya afya; ameyasema hayo akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaomba kura Wananchi wa Katavi.
Pia Mh. Magufuli amedhamiria kuboresha makazi ya wahudumu wa sekta ya afya hususani vijijini pamoja na kupambana na madawa ya kulevya ili kutengeneza nguvu kazi bora ya taifa.
Ni ushauri wangu kwa Watanzania wote tumchague Mh. Magufuli ili aweze kutekeleza haya na hatimaye kupata maendeleo kwa kasi zaidi
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Magufuli
#Hapa kazi tu