Magufuli Afunga kazi Sumbawanga Mjini

Magufuli Afunga kazi Sumbawanga Mjini

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini tayari kuwahutubia wakazi wa mji huo.
​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini.
​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hilaly .
​
Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya akiwahutubia wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Nelson Mandela.


​
Umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
​
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akimtambulisha mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini hapo.
​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atawatumikia kwa nguvu zake zote, na hatokuwa na simile na watendaji wazembe.
​
Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hilaly akihutubia wakazi wa Sumbawanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela ambapo CCM ilikuwa ikifanya mkutano mkubwa wa kunadi sera na mikakati yake kwa wananchi.
​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaonyesha ishara ya ushindi wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.


​
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
 
attachment.php
 
6.jpg


hivi haya nayo ni mafuriko mbon naona kama anongea na team ya mpira>>>>
 
Mbona Diamond Simuoni... au Pesa aliyodai Kampeni Nzima CCM hawana? sielewi wanashindwa Kutumia Nyota Yake...
 
g18.jpg


cheki majukwaa uwanja mtupu kabisa hamna watu majukwaani kama mngekuwa na nyomi mngepiga na drone aerial photograph sio mnapiga vipicha vya timing kiubavu-ubavu kurusha roho watu kwenye hamna.
6.jpg
 
g18.jpg


cheki majukwaa uwanja mtupu kabisa hamna watu majukwaani kama mngekuwa na nyomi mngepiga na drone aerial photograph sio mnapiga vipicha vya timing kiubavu-ubavu kurusha roho watu kwenye hamna.
g6.jpg
 
pombe mwisho bar...
Acha kujidanganya. Nyie wapinzani huu ni muda muafaka wa kukusanya nguvu zenu zote na kukabiliana na chama tawala kimikakati, badala ya kuendeleza kebehi zisizo na tija. La sivyo mwisho wa siku mtabaki kugalagala, kulia na kusaga meno.
 
Back
Top Bottom