Magreat Thinkers ninaowafeel...........

Thanks for the compliments kwa niaba ya washairi kama kina Michelle, Pakajimmy, Magulumangu na wengineo tunahitaji ushirikiano wenu adhimu kwenye fani hii.

Shukran sana.
 
Nimeongeza hii beti....

Ewe nawe The Finest usinung'unike,
Tena uingie ndani nawe ufarijike,
Utuambie amkeni, wanajamvi tubadilike
Tushikane kwa imani wabnajamvi tunusurike.

Duh!!! Watu mna hatari nyie anyways nimegundua kuna watu mahiri kama 7 hivi upande wa mashairi
 
PJ mzee sikuwezi banaa
 
Hilo shairi twangoja, ulitoe hadharani,
Usijefanya viroja, utuache mataani,
Ulijazie na hoja, lipambwe na umakini

Siku litakapokuja, twaomba tuwe hewani,
Lituletee faraja, kama ile ya manani,
Litujengee Umoja, tusiwe mahayawani
Sijui kwa nini nilikua nakacha somo la ushairi....
dah na uzee huu sijui kama ntaweza...
 
mkuu usinisahau hizo beti zingine..lol

nice stuff though
 
Sihaba hebu waambie, Wiselady mwana gani,
Pakajimmy tupasulie, wenzetu wambaini,
Ikibidi wapekulie, uwatoe usingizini.
Kumbe bibie mchagga, ndugu yetu wa milimani!
 
Thanks for the compliments kwa niaba ya washairi kama kina Michelle, Pakajimmy, Magulumangu na wengineo tunahitaji ushirikiano wenu adhimu kwenye fani hii.

Shukran sana.

Michelle hana lolote kwenye ushairi,nilijaribu tu siku ile kumjibu Magulumangu......lol
 
mkuu usinisahau hizo beti zingine..lol

nice stuff though

Nilishakuambia siku ukieleweka unacheka au unalia utafaidi sana,

Watu wanaogopa wakikuweka kweny mashairi utazidisha kulia sijui kucheka itakuwa tabu.......embu njoo nikufundishe kucheka na kulia..lol
 
kha!umeamua kuniua kabisa!ntakata huu mzizi wa fitna,,btw i never knew u have this precious talent,,lol
 
mkuu usinisahau hizo beti zingine..lol

nice stuff though

Ombi lako limesikaka na nime edit na kuingiza hiki kipande 🙂

Mwenzetu huyu si mgeni, Samora10 mwamjua
Mwenzetu si limbukeni, kusema anayoyajua
Samora10 hana utani, kwenye uovu hufichua,
Ni kijana muadilifu si kijana wakuchakachua.

Nilishakuambia siku ukieleweka unacheka au unalia utafaidi sana,

Watu wanaogopa wakikuweka kweny mashairi utazidisha kulia sijui kucheka itakuwa tabu.......embu njoo nikufundishe kucheka na kulia..lol

Lol.. niko njiani naja:car:
 
Sihaba hebu waambie, Wiselady mwana gani,
Pakajimmy tupasulie, wenzetu wambaini,
Ikibidi wapekulie, uwatoe usingizini.
Kumbe bibie mchagga, ndugu yetu wa milimani!

huyu paka aitwae jimmy usimskilize sana,,huwa hapendi maslahi yangu.
 
Ombi lako limesikaka na nime edit na kuingiza hiki kipande 🙂

Mwenzetu huyu si mgeni, Samora10 mwamjua
Mwenzetu si limbukeni, kusema anayoyajua
Samora10 hana utani, kwenye uovu hufichua,
Ni kijana muadilifu si kijana wakuchakachua.

naaaaam hapo umenitendea haki mkuu
 
huyu paka aitwae jimmy usimskilize sana,,huwa hapendi maslahi yangu.

Wasi wasi wa nini, Tabia zako makini.
umelelewa kijijini, wewe sio wamjini.
mnakoga mitoni, maji yenu sio mabombani.

Kule kwenu milimani, hamna doa la uhuni
munafanya mema kwa imani, munamuogopa manani.
hamwendi videoni, mwisho wetu shambani.
Analosema PJ, ni kukumbusha asili..............
 
Wiselady m'baya, ninasema hadharani,
Hatufai kwenye kaya, amekosa shukurani
Ameikosa hidaya, si mtu mwenye ubani

Na ukuu wa wilaya, haupati asilani
Atabaki anagwaya, hata aende shambani,
Hata aende Ulaya, atakuwa kisirani

Kabila yangu Mhaya, Bukoba napatamani,
Akipenda kuwa yaya, simpeleki nyumbani,
Atakuja sota waya, atoe jasho kwapani,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…