Magoli kumi bora ya kifo katika soka

DavidNgemela

Member
May 24, 2014
6
0
Goli la kifo au goli la dhahabu, Hili ni goli linalofungwa kwenye dakika thelathini za nyiongeza baada ya 90 kukamikika timu zikiwa suluhu, Mechi huwa inamalizika baada ya goli kupatikana na timu iliyofunga inakua imeshinda mechi.

Sheria ya goli la kifo ilianzishwa mwaka 1993 na kufutwa mwaka 2002 baada ya kombe la dunia. Hii sheria ilianzishwa ili kufanya muda wa nyiongeza uwe wa kuvutia zaidi na kuleta burudani kwenye soka, Waliamua kuifuta kwa sababu timu zilikua zinajilinda sana kuliko kushambalia pindi inapofika hatua ya dakika 30 za nyiongeza. Hiyo ilipelekea mechi nyingi kuamuliwa kwa matuta.

Sheria ya goli la dhahabu ilitumika kwa miaka 9 kwenye soka, Ndani ya miaka 9, Yafuatayo ni magoli 10 bora ya dhahabu ambayo hayawezi kusahaulika.

FRANCE v PORTUGAL (Euro 2000) Zinedine akifunga kwa penati dakika ya 117 kuipa ushindi Ufaransa dhidi ya Ureno, Ureno walipata goli la mapema kupitia kwa Nuno Gomez kabla ya Thiery Henry kuisawazishia Ufaransa na ikaamuliwa kwenye dakika 30 za nyiongeza. Hii ni mechi iliyokutanisha watu wenye vipaji vya hali ya juu kama Joao Pinto, Didier Deschamps, Xavier, Emmanuel Petit, Luis Figo, Marcel Desaily, Victor Baia, Sergio Conceisao, Zidane, Lilian Thuram na wengine wengi.

GERMANY v CZECH REPUBLIC ( Euro 96) Bierhoff akiwa na urefu wa ft 6.3 , Ilimaanisha Germany walikua na mtu sahihi wa kuwawezesha kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kucheza mipira ya juu na hiki ndicho kilichowapa ushindi baada ya Bierhoff kuingia akitokea benchi kwenye dimba la Wembley.

Ilipigwa Free kick nje kidogo na dimba la Czech, Bierhoff akiwa amebanwa na mabeki alitumia vizuri urefu wake na uwezo wa kupiga vichwa na kuisawazishia Germany na mechi ikaenda kwenye dakika 30 za nyiongeza. Kwa mara nyingine tena, Bierhoff alichukua mpira akampa Klinsman, ambaye alitulia na kupiga krosi kwa kwa Bierhoff ambaye alifanikiwa kufunga goli la dhahabu kwenye dakika ya 110.

SOUTH KOREA v ITALY (2002 World Cup) South Korea wakiwa nyumbani walifanikiwa kuwatoa Italy kwenye mechi iliyojaa utata mwingi. Meneja wa Italy, Giovani Trapattoni alilia sana.Refa wa mechi hiyo alikua ni Byron Moreno wa Ecudor, Alionekana wazi akifanya maamuzi ya kuwabeba South Korea. Alikataa goli la wazi la Italy na kumpa kadi nyekundu nyota wa Italia francesco Totti.Mechi iliamuliwa kwa goli la dhahabu lililofungwa na Ahn wa South Korea zikiwa zimebaki dakika tatu waende kwenye matuta.

REAL MADRID v GALATASARAY( 2000 Uefa Super Cup) Kwenye dimba la Stade Louis II (Monaco) fainali ya Super cup. Baada ya dakika za mchezo timu zilitoka suluhu baada ya kufungana 1-1 kila timu ikipata bao kwa njia ya penati. Mario Jardel hakufanya makosa kwenye dakika 103 akiunganisha shuti lililopigwa na Fatih Akyel na kumuacha kipa Iker Casillas asijue la kufanya na kupeleka shangwe Uturuki kwa goli la dhahabu.

ITALY v FRANCE (Euro 2000) Dakika ya 112, Mfaransa Robert Pires akiwa upande wa kushoto wa uwanja aliandika historia akiwaacha walinzi watatu wa Italia, akampa Nesta alafu ngoma ikamkuta Trezeguet ambaye hakufanya makosa, Akamtungua Toldo kwa staili ya goli la kifo. Wafaransa wakawa mabingwa wa ulaya mwaka 2000 baada ya kuchukua World Cup 98, Les blues(Wabluu) walikua hawakamatiki.

LIVERPOOL v DEPORTIVO ALAVES(2001 UEFA cup) Shukrani ziende kwa Delfi Geli aliyejifunga na kuwapatia Liverpool goli la dhahabu lililowapa ushindi na kutwaa UEFA Cup wakikamilisha makombe matatu, Baada ya kutwaa kombe la FA na Football league cup.

CAMEROON v FRANCE (2003 Confederations Cup) Fainali ya Confederations cup, Cameroon wakiwa wamevaa jezi zenye jina, tarehe ya kuzaliwa na tarehe ya kufa ya Marc-Vivien Foe aliyefariki uwanjani wakicheza na Columbia nusu fainali. Mechi ya fainali ilikua imepoa sana kutokana na majonzi ya kumpoteza kiungo Marc-Vivien Foe, Dakika 90 ziliisha ikiwa bila bila. Goli la dhahabu lilifungwa na Thiery Henry na kuipa Ubingwa France kwa mara nyingine tena.

FRANCE v PARAGUAY (98 World Cup) Ni kwenye hatua ya 16 bora, Laurent Blanc akifunga goli dakika ya 113 na kuipa ushindi france na kuandika historia yakuwa goli la kwanza la dhahabu kwenye fainali za kombe la dunia.

SENEGAL v SWEDEN (2002 World Cup) Senegal walifika robo fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 wakicheza mpira wa kuvutia sana. Waafrika walikutana na Sweden katika hatua ya 16 bora, Walijikuta wako nyuma kwa 1-0 kwa goli la mapema la Henrik Larsson. Kwenye dakika ya 37, Henri Camara akaisawazishia Senegal. Matokeo yakawa 1-1 mpaka dakika 90 zinakamilika.

Kwa mara nyingine tena, Henri Camara alifanya kile Waafrika walichotaka kifanyike baada ya kufunga goli ikiwa imebaki dakika moja waende mapumziko kwene dakika 30 za nyiongeza.

SENEGAL v TURKEY( 2002 World Cup) Baada ya senegal kuwaondoa Sweden kwa goli la kifo, sasa ilikua zamu yao kuondolewa kwa goli la kifo lililofungwa na Ilhan Mansiz na kupeleka shangwe Uturuki na kilio senegali. Lilikuwa ni bao lililofuta ndoto za senegal kufika nusu fainali.

Imeandikwa na David Ngemela -0768195348.
Mwanafunzi chuo kikuu St John's.
 

Gumilapua

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
745
500
safi sana David Ngemela, umenikumbusha baadhi ya matukio yalivuta hisia zangu enzi hizo.
Ila binafsi unapoongelea goli la kifo ni mechi ya nusu fainali ya olympic kati ya Nigeria Vs Brazil ndio huwa naikumbuka. Mfungaji alikuwa ni Nwanko Kanu kipindi hicho bado akiwa Ajax ilikuwa ndio dakika kama 2 kabla ya muda wa nyongeza haujaisha. Katika mchezo huo nakumbuka mpaka half time Nigeria ilikuwa Nyuma kwa 3-1, kipindi cha pili substitute Victor Ikpeba akafunga na Kanu akasawazisha ikawa 3-3. Zikaongezwa dk 30, wakati kila mtu akiamini kifuatacho ni matuta and taking into account we had already missed a penalt in normal time, Kanu akatuinua vitini!
Miaka 18 imepita sasa but the face of Brazilian star by then Bebeto wearing pain and frustration and on the other hand specutacular goal celebration by Kanu are still vivid and fresh in my mind!
 

DavidNgemela

Member
May 24, 2014
6
0
safi sana David Ngemela, umenikumbusha baadhi ya matukio yalivuta hisia zangu enzi hizo.
Ila binafsi unapoongelea goli la kifo ni mechi ya nusu fainali ya olympic kati ya Nigeria Vs Brazil ndio huwa naikumbuka. Mfungaji alikuwa ni Nwanko Kanu kipindi hicho bado akiwa Ajax ilikuwa ndio dakika kama 2 kabla ya muda wa nyongeza haujaisha. Katika mchezo huo nakumbuka mpaka half time Nigeria ilikuwa Nyuma kwa 3-1, kipindi cha pili substitute Victor Ikpeba akafunga na Kanu akasawazisha ikawa 3-3. Zikaongezwa dk 30, wakati kila mtu akiamini kifuatacho ni matuta and taking into account we had already missed a penalt in normal time, Kanu akatuinua vitini!
Miaka 18 imepita sasa but the face of Brazilian star by then Bebeto wearing pain and frustration and on the other hand specutacular goal celebration by Kanu are still vivid and fresh in my mind!

kweli ndugu, hilo ni bao kali pia. ila olibidi niandike mabao kumi tu. safi sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom