Kwanza mtoa mada, sio Erest Kawau ni Orast Kawau Mr. OK.
Mimi kama mpenzi wa kipindi cha Morning Magic ya Magic FM, ambacho ni kipindi bora cha asubuhi ambacho ni mewahi kukisikia kwa Radio za Tanzania, hasa kile kipande cha kupaka rangi, jamaa wana tia nyama za kutosha kwenye mjadala.
Salum Mkambala, hili ni JIPU, sio tu kwamba hajui analazimisha ucheshi ambao unapelekea kumchukia.
Aidha kwa Mery Edward tatizo lake kubwa ni kuchapia sana (kukosea utamkaji wa maneno), Orest Kawau Mr. OK huyu yuko vizuri tatizo lake anatuongelesha kingereza ambacho yeye mwenyewe hakijui. Kibwana Datchi huyu ni Mr. GOOGLE kweli kweli anajua kama Farid Qubanda FQ yaani anajua mpaka anaboa..
Ahsante